Nimeachana na mke wangu

Mkuu kwani hiyo ni mimba ya ngapi tangu muoane, yaani huyo ndo mtoto wa kwanza unaye tarajia kumpata?

Kama jibu ni ndiyo basi unatakiwa uzoee hiyo hali maana ni kawaida sana kwa wanawake wajawazito.
 
Achana na Dada yake wote lao moja- speaking from experience.

Cha muhimu umeupiga mwingi sana umeweza kutemana naye.

Mtihani wa mwisho kwako ni baada ya mtoto kuzaliwa,je hutamfeel na kuona anahitaji mapenzi ya baba na mama?
 
Mkuu wewe bado learner kwenye ndoa….tena inabidi ubandikwe L kubwaaa kabisa mgongoni mwako!!
 
Mambo ya kuoa bila kujifunza. Iko vipi mwanamke ni mtu wa hisia...na anapokuwa na mimba anapokuwa na mimba anataka wakati wote uwe naye...yaani uwe karibu naye awe anakutuma niletee limao unaenda unaleta, kaniletee kuku wa kuchoma akauke vizuri ...unaenda unaleta...fanya hiki unafanya. Hivyo ndivyo wanapenda.

Lakini bahati mbaya hiyo haiwezekani kwa sababu inatakiwa utafute fedha na maisha yaendelee. Kwa hiyo haya mambo mengi yanachangiwa na hali yake.... Unachotakiwa kufanya ni kuonyesha ukaribu kwake hata kama uko mbali na unapopata muda kiwa karibu naye. Onyesha ukaribu kwa kumjulia hali mara kwa mara, kumpa zawadi za supprise kwa mfano unataka kula nini leo...unamtuma boda boda ana mpelekea hata kama uko mbali n.k.

Kikawaida Mwanaume ni mtu wa logic na vitendo na mwanamke ni mtu wa hisia na maneno. Mwanamke anaweza kujenga nyumba kwa maneno na hisia na akaridhika kabisa kwamba hata ukifanya lolite yeye nyumba anayo. Kumbe ni hisia na maneno.

Punguza kujibishana na mwanamke, hautamuweza kwa maneno.

Mwanamke akiongea sikiliza...halafu muulize umemaliza. Au msikilize sema tu ...nimekusikia basi. Iwe ni kweli, au siyo kweli, ina mantiki au haina mantiki usijibishane naye. Nyamaza tu mwisho wa siku atajiona yeye mjinga.
 
Ulishawahi kumzibua makofi?Msingefika huku
 
Ukiwa mjamzito unaweza kufanya vitu mpk ukajishangaa mwenyew kama ndio wew tena unavifurahia na kujisikia aman kweli moyoni, hivyo vibweka anavyokufanyia ni homoni hizo zinampeleka resi anashindwa hata kujizuia.

Kuna mimba zingine tangu ziingie zinapenda magomvi tu sasa usipokuwa mvumilivu sana aisee unakata tamaa.

Nachokusihi usimuache wew kaa zako tu huko uliko ila jua una mke na anakupenda sana tu, hali yake ndio imemjia hvyo
 
Ila nimekufukunyua,nimegundua wewe ni mpuuzi tu,ni dhaifu sana na unatupotezea mda tu. Ona hizi nyuzi zako,drama drama kama sio wa kiume. Kila la heri

1. Sijui kwanini namchukia mke wangu
2. Nina wasiwasi na mke wangu...
3. Tangu nimehamishiwa Mkoani mwenza wangu amekuwa Mkorofi
 
HIVI MKIAMBIWA WANAWAKE WAKIWA WAJAWAZITO HIZO NI MAMBO ZA KAWAIDA...

NA NIMEGUNDUA NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA WAKATI WAKE WAKIWA WAJAWAZITO.

Mwanaume tujivunze kuwa na SUBRA.
 
Mke akiwa mjamzito kama Hana Mungu ndani yake utapimwa matukio, lakini akijifungua atarudi kawaida mrudishe tu
 
Wanawake wa design hiyo wapo wengi. Mimi nimeshuhudia, NI WIVU tu wanakuwa na hisia unakuwa na wanawake wengine.

Kuna vitu inabidi ujirekebishe ambavyo vinampa wasiwasi kama kampani zako ni za namna gani zinamfanya asikuamini, Mambo ya mitandaoni , WhatsApp yako, epuka Sana kuzungumzia habari za wanawake wengine kikubwa jifunze jinsi ya kumbebeleza na jishushe Sana kama unampenda badae atabadilika.

HUYO WIVU TU ULIOPITILIZA ANATULIZWA TAFUTA WANASAIKOLOJIA WAKUSHAURI NAMNA YA KUMTULIZA

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ni mood swings za mimba. Akijifungua atakaa sawa mkuu. Achana na masuala ya talaka. Wanawake wakiwa na mimba wanapitia mvurugiko mkubwa sana wa mfumo wa miili yao hivyo ni matokeo ya mimba tu hayo mkuu, relax.

Sawa mkuu nimekuelewa
 
Hayo ndo maamuzi ya kiume , mwanaume popote kambi, ilikuwa kidogo tuu akuwekee Sumu kwenye chakula ,wanawake wa mjini ni ng'ombe haswaa

Weacha tu mkuu wacha niishi maisha mapya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…