Nimeacha kusikiliza Wasafi Fm kwa sababu ya Zembwela

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,310
12,607
Zimbwela bwana.

Amenifanya nimeacha kusikiliza Redio ya Wasafi asubuhi.

Huyu jamaa anafanya comedy hata kwenye serious issues, anatengeneza kelele masikioni na kupoteza muda wa wasikilizaji wake akidhani kuwa wasikilizaji wako tayari kusikiliza kila kitu anachosema na kufanya kwenye studio, ananiboa.

Hata bidhaa anazozitangaza ninaziona kama zisizo na ubora kwa namna anavyopitiliza kuzinadi. Anasahau kuwa "kizuri kinajiuza na kibaya kinajitembeza na kupambwa mno".

Anachohitaji mtu kwenye bidhaa ni kujua jina la bidhaa, aina na ubora wake dhidi ya bidhaa nyingine zilizoko kwenye soko ova!

Sijui kama hii inanipata mimi tu.
 
Back
Top Bottom