Nilizama katika mapenzi mazito,,,,,,

Nilizama katika mapenzi mazito,,,,,,

Rjmdaki

Member
Joined
Dec 14, 2012
Posts
20
Reaction score
2
Habari zenu wana jf, nimefurahi kupata sehemu ambayo naweza kusema imenisaidia kujua mawazo ya watu na jinsi gani tunaweza kusaidiana katika masuala mazima tunayokabiliana nayo katika maisha yetu ya kila siku. Ni mara yangu ya kwanza kupost humu na ntafurah kama mtanisaidia ktk hili suala linalontatiza...
Nilizama ktk mapenzi mazito ya msichana ambaye jina lake naomba nilihifadhi, yeye ndie alikua wa kwanza kunitamkia kuwa ananipenda, na kwakua hakua mgeni machoni mwangu, na tulishazoeana hapo mwanzo kama mtu na rafiki yake, ilibidi nikubali kuwa naye, nilimpatia mapenzi mazito na tulikua watu wenye furaha sana katka mapenzi yetu, hakuchoka kutabasamu kila alipokutana na mimi. Nilimsimulia story nzuri pamoja na kumpatia zawadi kama inavotakiwa kwa wapenzi. Naye pia hakusita kunipatia zawadi mbalimbali ambazo zilinifanya nijione ni mimi tu katika dunia ya mapenzi. Katika mwezi wa 1 mwaka 2013, aliweza kuchukuliwa na kwenda kwa Baba mkubwa wake mkoani Shinyanga, alipokua huko tuliweza kuwasiliana kupitia simu kila mara. Na aliporudi mapenzi yetu yaliendelea kama kawaida___. Huku nyumbani alikua anaish na wazazi wake mdogo wake pamoja na kaka yake, sikuzoeana kivile na kaka yake. Pia kulikua na dada mmoja hivi ambae yeye (Mpenzi wangu) aliweza kunitambulisha kuwa ni dada yake, nami niliamini. Na haikuchukua muda kumzoea kwani alikua mchangamfu, mkarimu na mpenda kusali, na aliweza kunishauri mara kwa mara kwenda kusali naye ila sikuwah kufanya hivyo,,, Lakini wakati anarudi kutoka Shinyanga, dada huyo aliyeniambia ni dada yake aliondoka pale kwao na kwenda kwa wazazi wake. Hivyo basi kumbe hakua dada yake na wala hawana mahusiano yoyote.
Sasa alipokuwa hapa nyumbani huyo Mpenzi wangu mimi, hakua na muda wa kutosha wa kukutana na mimi kama alivyokua akisema mwenyewe. Nikiwa naongea naye anaondoka, kifupi ni kuwa alionesha kunichoka, mimi sikukata tamaa, nikijaribu kumpatia zawadi kama zamani, hapo alikua anaonesha tabasamu. Kitu kingine anadai kuwa kuna watu walimfuata na kumwambia aachane na mimi, na hicho ndicho kitu ambacho kinanisumbua na sijawahi fanya kitu kama hicho. Na yeye anajua jins gani nampenda, siku hizi amebadilika na akiniona anatafuta njia nyingine ya kwenda, zile romantic moments tulizokuanazo zamani sasa hazipo.
Sijui amepatwa na jinamizi gani, nikiongea naye anaonesha kama amechoka flan mi hata simuelewi, lakn mimi bado nampenda.
Na sasa yule dada, ambaye aliniambia ni dada yake kumbe hawana udugu wowote anatumia muda mwingingi kunifariji na kunipa moyo na kuniambia huenda labda mungu hajanipangia bado mtu wa kuwa naye. Ananifariji na kunipa moyo kiasi kwamba najikuta namsahau mpenzi wangu.
***
Ambacho naomba mnisaidie ni kuwa ni muache mpenzi wangu wa zamani, niende kwa huyu dada, ambaye ananifanya nasahau matatizo nilo nayo? Au nimvumilie kwa kuamini kua ipo siku atabadilika na kuwa kama zamani? Manake nilimfanya kweli ajione mwanamke, na sikumfosi kufanya kitu alichowahi kuniambia hakimpendezi au kitu ambacho hakujiskia kufanya kwa wakati niliokuanaye.
Ningependa kumaliza kwa kusema nakushukuru wewe ambae umetumia muda wako kwa kusoma post hii, naomba ushauri wako tafadhali. Nifanyeje?
 
^^
Mwanaume akimpenda mwanamke amekosa yote.
Mwanamke akimpenda mwanaume amepata yote.
^^
 
Achana nao wote.....!utakuja changanyikiwa zaid kwa maana hujui chanzo cha mpenz wako kubadilika.
Huenda huyohuyo mfariji ndo kidudu mtu......lol.
 
Mi huwa siamini kama kuna mapenzi ya milele. Nimeshuhudia watu waliokuwa wakipendana sana na baadae kuwa maadui wakubwa. Mapenzi yana muda halafu huchuja, hata mpendane vipi!!! Hayo ya kwenu yameshachuja kwa upande wa huyo dada. Fantasize on the best moments you had in the past, but usipofuke. Unaweza pata mwingine ambaye anaweza kupa raha kuliko hata huyo anaekuringia sasa. Angalia mbele piga hatua. Kwenye viatu vyako ningejipoza na huyo anaekufariji sasa. USijaribu sana kuimplement mapenzi ya kwenye novel, zile ni imaginations za author, si lazima ziwe kweli.
 
Mkuu inabidi kutulia sana aisee na kuacha papara..

Inategemeana na umri wa huyo bidada maana yawezekana pia foolish age imo bado na ikawa kikwazo sana katika mahusiano yenu na ndio chanzo cha kukuchoka. Mwanamke anapokua na options nyingi katika mahusiano au anapohisi ana options nyingi humpelekea kuwa na nyodo nyingi na kuingia upofu wa kutokujua nani hasa anayempenda.
Hii humfanya kuruka mkojo na kukanyaga mav*, na hapa ndipo kosa lao kubwa sana linapokua.

Hapa una options kubwa mbili ambazo unaweza kuzitumia ukiwa kama mwanaume
  • Kama umri wake ni mdogo ie below 24 au 25 (kwa wengine) inabidi umuachie uhuru tu wa kucheza cheza maana bado utoto ni mwingi sana kichwani na anaona unampotezea muda wa kufaidi ubinti wake hasa kama kuanzia ausubuhi mpaka jioni unaongelea ndoa tu wakati yeye bado anataka kula maisha na kuufaidi ujana
  • Kama ni mtu mzima yawezekana amepata mahala anasifiwa sifiwa na vijana wa mjini(ie kapata mwingine anayetoa love moto moto) kw hiyo unaonekana uko old fashioned sana. Unachotakiwa hapa ni kukimia mbio za marathoni yaani mdogo mdogo kama haupo lakini upo (slow but sure) mwisho wa siku atarudi tuu, Time always tell the truth
Cha msingi ni kumuacha kwanza akukuruke na
 
^^ Mwanaume akimpenda mwanamke amekosa yote. Mwanamke akimpenda mwanaume amepata yote. ^^
Hapana, muda mwingine mwanamke anaachiwa apate kwa malengo flan flan, si siku zote mwanamke ni mtu wa kupata Mr. Himidini
 
Nashukuru sana kwa ushauri wenu, tauzingatia na kuufanyia kazi. Mungu awabariki
 
tulia kaka yangu subira yavuta heri me yalinikuta nikatulia kumbe mpenzi kabadilika cz ya maneno ya watu wa karibu alivyogundua wanamdanganya hadi leo karudi kwangu na kaganda
 
Mkuu inabidi kutulia sana aisee na kuacha papara.. Inategemeana na umri wa huyo bidada maana yawezekana pia foolish age imo bado na ikawa kikwazo sana katika mahusiano yenu na ndio chanzo cha kukuchoka. Mwanamke anapokua na options nyingi katika mahusiano au anapohisi ana options nyingi humpelekea kuwa na nyodo nyingi na kuingia upofu wa kutokujua nani hasa anayempenda. Hii humfanya kuruka mkojo na kukanyaga mav*, na hapa ndipo kosa lao kubwa sana linapokua. Hapa una options kubwa mbili ambazo unaweza kuzitumia ukiwa kama mwanaume
  • Kama umri wake ni mdogo ie below 24 au 25 (kwa wengine) inabidi umuachie uhuru tu wa kucheza cheza maana bado utoto ni mwingi sana kichwani na anaona unampotezea muda wa kufaidi ubinti wake hasa kama kuanzia ausubuhi mpaka jioni unaongelea ndoa tu wakati yeye bado anataka kula maisha na kuufaidi ujana
  • Kama ni mtu mzima yawezekana amepata mahala anasifiwa sifiwa na vijana wa mjini(ie kapata mwingine anayetoa love moto moto) kw hiyo unaonekana uko old fashioned sana. Unachotakiwa hapa ni kukimia mbio za marathoni yaani mdogo mdogo kama haupo lakini upo (slow but sure) mwisho wa siku atarudi tuu, Time always tell the truth
Cha msingi ni kumuacha kwanza akukuruke na
Nashukuru sana mkubwa, huyo dada ni mkubwa tu, ni 18, kama unavosema labda anataka kutumia uschana wake vizur
 
Hapana, muda mwingine mwanamke anaachiwa apate kwa malengo flan flan, si siku zote mwanamke ni mtu wa kupata Mr. Himidini

^^
Hukuelewa vema nilichomaanisha,,ni hivi anaepata mateso ya kukupata anajua thamani ya kukutunza.Lakini anaejua utamfuata hajui thamani yake.
Kuhusu mwanamke ni mtu wa kupata,,nusu kweli nusu si kweli.
Ni kweli kwa sababu women live with plan B,,si kweli kwa sababu they smile but their smiles are artificial.
^^
 
nowdays.. love is all about uncertainty and risk
 
Achana nao wote.....!utakuja changanyikiwa zaid kwa maana hujui chanzo cha mpenz wako kubadilika. Huenda huyohuyo mfariji ndo kidudu mtu......lol.
Hivo unanishauri nitafute mwingine tofauti na hao?
 
Ma boy emb cool down kwanz,kuna uwezekan mkubwa ukawa umewekwa kwenye mtego, huyo unaeona anakupoza kwa upand wangu naon n kama mtu hatar xana.

Ckwambi uanza mchukia bt be care, Halaf kuhusu huyo wa nyodo kaa zako punguza kmtumia sms,kumpigia taratibu bdae utaacha kabsa.

Bt ucmchukie kuwa 2 wa kawaida ila uliyepoteza matumain kwake
 
Mi huwa siamini kama kuna mapenzi ya milele. Nimeshuhudia watu waliokuwa wakipendana sana na baadae kuwa maadui wakubwa. Mapenzi yana muda halafu huchuja, hata mpendane vipi!!! Hayo ya kwenu yameshachuja kwa upande wa huyo dada. Fantasize on the best moments you had in the past, but usipofuke. Unaweza pata mwingine ambaye anaweza kupa raha kuliko hata huyo anaekuringia sasa. Angalia mbele piga hatua. Kwenye viatu vyako ningejipoza na huyo anaekufariji sasa. USijaribu sana kuimplement mapenzi ya kwenye novel, zile ni imaginations za author, si lazima ziwe kweli.
Mapenz ya milele hamna ila tunajitahidi kuyafanya yadumu, lakini wapenz wetu ndo wanaotuangusha
 
Back
Top Bottom