Nilizaa na Housegal

Swahilian

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
591
65
Imenichukua muda kuisimulia hii hadithi iliyo ya kweli..

Nahisi ni mie mwenyewe katika dunia hii nilokumbwa na mkasa huu wa aibu na ambao sitausahau maishani..
Ama kweli sikusikia la mkuu na hayo yakanitokea na mpaka leo najutia..

Sikupenda iwe hivyo hadi leo wewe usome habari yangu hii lakini natazama na kwa mbali, maji yalishamwagika.

Walezi wangu waliniamini tangu nikiwa mdogo kuwa kijana mwema, hakika hawakukosea.

Kunipeleka shule nikatoe ujinga na kusoma elimu ya dini walinipatia.

Sikuwa mgomvi, mtukani wala jeuri ila kimoja tu kilinifanya kuangamia,

Dhakali iliyo ktk maungo yangu ilinitia topeni ikanichafua..

Kipindi hicho namaliza kidato cha sita binti mrembo nyumbani akaingia..

Si kwamba aliletwa nimweke gambani na kunililia..

Bali awe Dada wa kazi nyumbani kutusaidia..

Tamaa za tupu ya mbele zikanizidia, baadaye nikamwingilia..

Zikapita siku za kufurahia.. Aah kumbe machungu yaningojea..

Kaniita siku moja huyo dada/mpenzi akaanza kunambia..

Nimejaa my dia nataka kuitoa..

Wote nyumbani wakajua, nkabaki kuchukia binti kawa harufu mbaya sitaki hata akisogea..

Wote wakagundua vikao kukaliwa..

Binti akasanua ati mie ndo nilokamua,

sina la kuamua tusubiri kumpokea..

Mpaka sasa naongea mwana yu miaka tano..

Nimetaabika sana moyo wangu ukiungua..

Kumwoa sikupanga je? Nifanyeje kumlipia!

Nampenda mwanangu aishi kwa ulezi wa baba na mama..

MAMAYE KUMWOA SINTAWEZA...

Ushauri wenu utanifungua mawazo..

Wasalaam..
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,815
5,232
Si lazima uishi nae kama huna mapenzi na mama yake.

Unachotakiwa kufanya awali ya yote, ni kuhakikisha unatoa huduma zote kwa mtoto, na kumwambia kuwa wewe ni baba yake. Hakikisha pia unamchukua nyumbani kwenu ili kuwajua jamaa zako pia.
 
Hilo nalifanya sana kaka, japo sifanyi kama vile mie nilifanyiwa..
Namtembelea mara chache sana na namwona anaathirika kisaikolojia, japo anasoma shule sasaa..!
Huwa natamani nimchukue lakini watu wananshauri nimwache kwa mamaye na nadhani wako sahihi..
Kuhusu kumtambulisha kwa jamaa na ndugu, ndio nimefanya ingawa ni kwa baadhi tu wale ambao naelewana nao vizuri.
Wapo ambao hawataki hata kusikia..! Inaniumiza sana as ni watu/ndugu wa karibu sana kwangu..
Hata pale niombapo msingi au msaada fulani husema hadi uachane na kumjali mtoto na huyo mwanamke..
Hapo huwa hatuendi sawa nao..
 
Muhimu ni kujua kuwa unachofanya ni jambo sahihi; kwako na kwa Mungu wako. Huwezi kuwaridhisha binaadamu wote daima dawamu

Wewe jitahidi uende kuonana nae zaidi ili mtoto ajue kuwa ana baba anaemjali. Mtoto wa miaka mitano si mdogo kuwa haelewi, mfahamishe kuwa wewe ni baba yake lakini huishi na mama yake lakini unampenda sana. Mara moja moja take him out just the two of you apate kukuzowea.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

yees.! Thats what i do..
He also knows..
But guilty consiousness of wha i did past kills me slowly kaka!

Lini nitaliona jambo nilofanya ni la kupita/kawaida?
Hapo ndio pagumu kwangu...
But thanks@ Gaijin
 
Swahilian

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
591
65
Muowe awe mke wako unasemaje?Umesha muharibia maisha yake, Hata kwa Mungu una makosa wewe ukimuacha Solelemba.

Maisha ni kweli nimemuharibia japo nami nimepata athari kutokana na kwayo,

Lakini katika suala la dhambi hilo kiimani kila mtu ana mbinu zake za kuomba msamaha...
Kumwoa hakika sintaweza kwakua bado nina kumbukumbu mbaya iliyokuja baadaye..
Yeye pia anajua na yuko radhi mie nipatapo mtu nimwoe,.@Mzizi
 
SOBY

JF-Expert Member
Sep 19, 2011
1,268
456
Kama alivyosema Gaijin,
Jaribu kadri uwezavyo kumuona na kutumia muda mwingi uwezavyo na mwanao.
Baada ya muda mtapendana tu!!...it's so natural!
Usimfiche, mwambie mimi ni baba yako, nakupenda kwa moyo wote ila sintaweza kuishi na mama yako, ila namweshimu sana kwa kukubeba wewe kwa miezi tisa(au kumi...whatever).
Akikua.....nduguzo hawatamtupa, watamkubali tu.
Mwisho ndugu yangu, wala usijute..... mtoto ni baraka. Ila ashiki yako uihusishe na mapenzi, kwani ngono bila mapenzi ni sawa na besheni tu!
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,546
5,674
Unataka mwanao aishi na malezi mama na baba, ila hautaki kumuoa mama yake. Hakuna njia ya kufikia lengo lako isipokuwa kumuoa huyo Mke.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
28,291
26,575
Kwanin unakua na kumbukumbi mbaya kwake?
Hiyo ni bahati mbaya tu kaka,
Niandikapo hapa nami nilizaa na mdada jirani yetu kipindi nikiwa form 4 miaka 11 iliyopita,
Yakapita yaliyopita but now naishi na mwanangu vizuri tu akiwa na msichana wa kazi.
Usiite kumbukumbu mbaya bwana, we chukulia poa tu!!
 
charndams

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
436
126
kwa nini hutaki kumwoa huyo dada? kwa kuwa umesoma naye hakubahatika unaona sasa sio wa class yako sio? pupa zako zilimharibia malengo dada wa watu huenda maisha yake yangekua mazuri baadae sasa unaona haya kumuoa kisha una elimu kumliko. tafdhali hebu tafakari kisha uchukue hatua. japo kwa kiasi unampenda mwanao kumbuka machozi ya huyo dada yatakufuata mpaka kaburini na katika maisha yako yote hutokuwa na raha. hadithi hii imenisikitisha sana kuona wanawake wanafanywa kama carpet/dust bin/dekio kukidhi mahitaji ya wanaume wasiokua na huruma. Jamani ukimuoa huyo dada utapungukiwa na nini? kama ni kusoma unaweza kumsomesha akafikia kiwango utakacho.
haipendezi hata kidogo. mwonee mwanao huruma pamoja na mamake. nakusihi sana fikiria mara mbili.
yangu macho tu.
 
Margareth

New Member
Sep 12, 2011
4
2
Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ndio kosa...sasa naona wewe unataka kulirudia...please muoe huyo dada ili mtunze huyo mtoto. Usiwe selfish kaka mfikirie na yeye...umemuharibia future yake...angefanya mangapi ya maendeleo hadi sasa bila ule ujauzito na mtoto aliyezaa...dhihiriisha uungwana wako kaka ... just marry her... mapenzi huja baadae... manake ht waliooana wanapendana baadhi yao ndo hawa tunakutana nao mahakamani wanadai au kutoa talaka zao...
 
lolyz

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
338
197
Unasema huna mapenzi naye je tangu mmeanza mahusiano ulishamuona au kuskia kuwa ana mwanaume mwingine? je ni mwaminifu kwako? sio kwamba nasapot ww kujichanganya na mdada ila mlishakuwa na wadada wangapi hapo kwenu is she the first one?if not may be there's somthing btn u two,mke mwema mtu hupewa na bwana haijalishi watu wanasemaje ila cha msingi tambua kuwa wote mlikosea na huna haja ya kuendelea kumchukia you need to start over.Kaka yangu yaliwahi kumkuta hayohayo na mdada akafukuzwa imagine kaka alikuwa haonekani home kumbe akawa amempashia chumba somewhere huko na akampa mtaji akawa na biashara ndogo,the girl was smart,alikuwa anamshauri kaka mambo mengi tu ila baada ya wazazi kugundua walinyan'ganya mtoto mradi tu kaka asiende huko na kweli yule mdada akaolewa na mwanaume mwingine na sasa hivi kaka yangu yupoyupo tu mara leo ana huyu kesho huyu ..sometime wazazi wanajuta niliwahi kuwaskia wakisema bora tungemsomesha yule binti. You will never know what future holds for you ,kama yeye anakupenda pls think twice kama anaendelea na mambo yake i think thats fine you may carry on also but its good to raise your son with his mom.
 
Rubuye123

JF-Expert Member
Dec 18, 2009
2,319
1,836
asasa hapa bwa mdogo.........unataka kuifikia pepo bila kufa!!hii ni sawa na kusema haiwezekani.ila kwa mtoto fanya kila alichoshauri mwalmu Gaijin na zaidi!!hajakosea lolote yule,ni mitamaa yenu tu.so mfanye ajue ana baba anaempenda sana na tengeneza maisha yake ya kesho.hao ndugu wengine wasiomtaka wala wasikupe presha.dogo ' akitoka' baadae na wakaona hawezi kuwa mzigo kwao tena wao au hata watoto wao watatafuta tu kujiunganisha nae.

Nampenda mwanangu aishi kwa ulezi wa baba na mama..

MAMAYE KUMWOA SINTAWEZA...

Ushauri wenu utanifungua mawazo..
 
Rubuye123

JF-Expert Member
Dec 18, 2009
2,319
1,836
Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ndio kosa...sasa naona wewe unataka kulirudia...please muoe huyo dada ili mtunze huyo mtoto. Usiwe selfish kaka mfikirie na yeye...umemuharibia future yake...angefanya mangapi ya maendeleo hadi sasa bila ule ujauzito na mtoto aliyezaa...dhihiriisha uungwana wako kaka ... just marry her... mapenzi huja baadae... manake ht waliooana wanapendana baadhi yao ndo hawa tunakutana nao mahakamani wanadai au kutoa talaka zao...

i beg to differ madam!ndugu mwanzisha mada hii ni grave mistake utafanya.usifanye maamuzi magumu kama kuishi na mtu(ndoa)bila kuwa certain na uamuzi unaoufikia jhamaa!'umeharibu future'..........kama ni kosa mlilifanya pamoja,sidhani kwamba alikuwa mdogo wa kutokujua matokeo yanayoweza kufuata alichokuwa akikifanya...na zaidi sana naamini hukumbaka!.'.dhihirisha uungwana wako kaka....just marry her'....usioe kwasababu unamuonea huruma binti aisee...UTAJUTA! you DONT JUST MARRY her..pliz!you marry her baada kuwa na uhakika ni yeye HASWA unaemuhitaji........'mapenzi huja baadae'......sijui kama na wewe mtoa mada unaamini hivi ila binafsi naamini MAPENZI HUITANGULIA NDOA!

kinyume na hapo utafanya kosa/makosa mengi mno kama au zaidi ya lile moja ambalo mpaka sasa unalijutia!!

senti zangu mbili tu hizo mkuu!
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,760
572
tatizo ulimpenda kwa ajili ya kumaliza haja zako na tayari ulikuwa na mapenzi nae sasa yamekuja matokeo unaanza kumuona mchafu .... acha tabia za ajabu kaa chini mjipange jinsi ya kulea mtoto
 
Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
9,965
yees.! Thats what i do..
He also knows..
But guilty consiousness of wha i did past kills me slowly kaka!

Lini nitaliona jambo nilofanya ni la kupita/kawaida?
Hapo ndio pagumu kwangu...
But thanks@ Gaijin
honestly Swahilian nashindwa kukuelewa,are you feeling guilty kwa kuzaa kabla ya kuoa au una feel guilty kwa kuzaa na house girl? if it is the latter kwangu litakuwa jambo la kusikitisha sana maana ina maana ungezaa na airhostess au nesi basi usingefeel guilty? huo sasa utakuwa ni ni unyapapaa ambao haukubaliki.Kiila siku tunaimba humu mmu tujifunze kuwathamini watu si kwa sababu ya taaluma zao au pesa zao bali kwa sababu ya utu wao,umenipata Mkuu?Always remember housegirl ni mwanamke kama mwanamke mwingine yeyote na ana haki ya kupendwa na kuenziwa just like any woman!
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom