Nilizaa na Housegal

Muoe tu huyo msichana, kaanze kumsomesha hata veta, inaonekana unampenda sana, ila unaona tu aibu kwamba ni HG
kwani hawa wafanyakazi wa ndani wanatofauti gani na wadada wa ofisini kama siye?mbona tukienda ulaya na sie huwa tunakuwa watumishi tu wa ndani?au inakuwaje, hamuoni mifano hata kwenye tamthilia, wakaka wengi tu wanaoa watumishi wa ndani, aaaarghhh,, wasichana sijui watadhalilishwa mpaka lini
 
The best man is one who take care of his wife and chilldren ole wao wafanyao zinaa na kuwafanya wengine waangamie kwa maovu yao Baba yetu hatakuwa na huruma kwa watu hawa bali kwa kuomba msamaha kwa wale waliowakosea na hata kuwatendea mema wasibaki wakijuta kwa maumivu waliyopata..... huwezi kumwoa... unataka malezi ya baba na mama kwa mtoto..... mtendee mtoto wako haki ya malezi ya wazazi wake wote
 
je unaendelea kimapenzi na huyo dada?
Je huyo dada anaelewa msimamo na hisia zako?
Usioe m2 kwa sababu umezaa nae bali kwa sababu unampenda. Je wampenda? Je wataka awe mkeo? Usije mwoa na ukamwathiri mtotdn kwa familia isiyo na mapenzi na kujaa mafarakano.

Pia watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu, mshukuru mlee na kumpenda mwanao, spend muda mwingi nae. Wanaotaka kukufanya usimlee mwanao usiwasikilize, huwezi kumridhisha kila m2 duniani, mwanao ndo 1st priority
 
Imenichukua muda kuisimulia hii hadithi iliyo ya kweli..

Nahisi ni mie mwenyewe katika dunia hii nilokumbwa na mkasa huu wa aibu na ambao sitausahau maishani..
Ama kweli sikusikia la mkuu na hayo yakanitokea na mpaka leo najutia..

Sikupenda iwe hivyo hadi leo wewe usome habari yangu hii lakini natazama na kwa mbali, maji yalishamwagika.

Walezi wangu waliniamini tangu nikiwa mdogo kuwa kijana mwema, hakika hawakukosea.

Kunipeleka shule nikatoe ujinga na kusoma elimu ya dini walinipatia.

Sikuwa mgomvi, mtukani wala jeuri ila kimoja tu kilinifanya kuangamia,

Dhakali iliyo ktk maungo yangu ilinitia topeni ikanichafua..

Kipindi hicho namaliza kidato cha sita binti mrembo nyumbani akaingia..

Si kwamba aliletwa nimweke gambani na kunililia..

Bali awe Dada wa kazi nyumbani kutusaidia..

Tamaa za tupu ya mbele zikanizidia, baadaye nikamwingilia..

Zikapita siku za kufurahia.. Aah kumbe machungu yaningojea..

Kaniita siku moja huyo dada/mpenzi akaanza kunambia..

Nimejaa my dia nataka kuitoa..

Wote nyumbani wakajua, nkabaki kuchukia binti kawa harufu mbaya sitaki hata akisogea..

Wote wakagundua vikao kukaliwa..

Binti akasanua ati mie ndo nilokamua,

sina la kuamua tusubiri kumpokea..

Mpaka sasa naongea mwana yu miaka tano..

Nimetaabika sana moyo wangu ukiungua..

Kumwoa sikupanga je? Nifanyeje kumlipia!

Nampenda mwanangu aishi kwa ulezi wa baba na mama..

MAMAYE KUMWOA SINTAWEZA...

Ushauri wenu utanifungua mawazo..

Wasalaam..

Shairi lako zuri sana.BIG UP UNAJUA
 
Muowe awe mke wako unasemaje?Umesha muharibia maisha yake, Hata kwa Mungu una makosa wewe ukimuacha Solelemba.

Maisha ni kweli nimemuharibia japo nami nimepata athari kutokana na kwayo,

Lakini katika suala la dhambi hilo kiimani kila mtu ana mbinu zake za kuomba msamaha...
Kumwoa hakika sintaweza kwakua bado nina kumbukumbu mbaya iliyokuja baadaye..
Yeye pia anajua na yuko radhi mie nipatapo mtu nimwoe,.@Mzizi

Kama alivyosema Gaijin,
Jaribu kadri uwezavyo kumuona na kutumia muda mwingi uwezavyo na mwanao.
Baada ya muda mtapendana tu!!...it's so natural!
Usimfiche, mwambie mimi ni baba yako, nakupenda kwa moyo wote ila sintaweza kuishi na mama yako, ila namweshimu sana kwa kukubeba wewe kwa miezi tisa(au kumi...whatever).
Akikua.....nduguzo hawatamtupa, watamkubali tu.
Mwisho ndugu yangu, wala usijute..... mtoto ni baraka. Ila ashiki yako uihusishe na mapenzi, kwani ngono bila mapenzi ni sawa na besheni tu!

Unataka mwanao aishi na malezi mama na baba, ila hautaki kumuoa mama yake. Hakuna njia ya kufikia lengo lako isipokuwa kumuoa huyo Mke.

kwa nini hutaki kumwoa huyo dada? kwa kuwa umesoma naye hakubahatika unaona sasa sio wa class yako sio? pupa zako zilimharibia malengo dada wa watu huenda maisha yake yangekua mazuri baadae sasa unaona haya kumuoa kisha una elimu kumliko. tafdhali hebu tafakari kisha uchukue hatua. japo kwa kiasi unampenda mwanao kumbuka machozi ya huyo dada yatakufuata mpaka kaburini na katika maisha yako yote hutokuwa na raha. hadithi hii imenisikitisha sana kuona wanawake wanafanywa kama carpet/dust bin/dekio kukidhi mahitaji ya wanaume wasiokua na huruma. Jamani ukimuoa huyo dada utapungukiwa na nini? kama ni kusoma unaweza kumsomesha akafikia kiwango utakacho.
haipendezi hata kidogo. mwonee mwanao huruma pamoja na mamake. nakusihi sana fikiria mara mbili.
yangu macho tu.

Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa ndio kosa...sasa naona wewe unataka kulirudia...please muoe huyo dada ili mtunze huyo mtoto. Usiwe selfish kaka mfikirie na yeye...umemuharibia future yake...angefanya mangapi ya maendeleo hadi sasa bila ule ujauzito na mtoto aliyezaa...dhihiriisha uungwana wako kaka ... just marry her... mapenzi huja baadae... manake ht waliooana wanapendana baadhi yao ndo hawa tunakutana nao mahakamani wanadai au kutoa talaka zao...

Unasema huna mapenzi naye je tangu mmeanza mahusiano ulishamuona au kuskia kuwa ana mwanaume mwingine? je ni mwaminifu kwako? sio kwamba nasapot ww kujichanganya na mdada ila mlishakuwa na wadada wangapi hapo kwenu is she the first one?if not may be there's somthing btn u two,mke mwema mtu hupewa na bwana haijalishi watu wanasemaje ila cha msingi tambua kuwa wote mlikosea na huna haja ya kuendelea kumchukia you need to start over.Kaka yangu yaliwahi kumkuta hayohayo na mdada akafukuzwa imagine kaka alikuwa haonekani home kumbe akawa amempashia chumba somewhere huko na akampa mtaji akawa na biashara ndogo,the girl was smart,alikuwa anamshauri kaka mambo mengi tu ila baada ya wazazi kugundua walinyan'ganya mtoto mradi tu kaka asiende huko na kweli yule mdada akaolewa na mwanaume mwingine na sasa hivi kaka yangu yupoyupo tu mara leo ana huyu kesho huyu ..sometime wazazi wanajuta niliwahi kuwaskia wakisema bora tungemsomesha yule binti. You will never know what future holds for you ,kama yeye anakupenda pls think twice kama anaendelea na mambo yake i think thats fine you may carry on also but its good to raise your son with his mom.

tatizo ulimpenda kwa ajili ya kumaliza haja zako na tayari ulikuwa na mapenzi nae sasa yamekuja matokeo unaanza kumuona mchafu .... acha tabia za ajabu kaa chini mjipange jinsi ya kulea mtoto

honestly Swahilian nashindwa kukuelewa,are you feeling guilty kwa kuzaa kabla ya kuoa au una feel guilty kwa kuzaa na house girl? if it is the latter kwangu litakuwa jambo la kusikitisha sana maana ina maana ungezaa na airhostess au nesi basi usingefeel guilty? huo sasa utakuwa ni ni unyapapaa ambao haukubaliki.Kiila siku tunaimba humu mmu tujifunze kuwathamini watu si kwa sababu ya taaluma zao au pesa zao bali kwa sababu ya utu wao,umenipata Mkuu?Always remember housegirl ni mwanamke kama mwanamke mwingine yeyote na ana haki ya kupendwa na kuenziwa just like any woman!

Muoe tu huyo msichana, kaanze kumsomesha hata veta, inaonekana unampenda sana, ila unaona tu aibu kwamba ni HG
kwani hawa wafanyakazi wa ndani wanatofauti gani na wadada wa ofisini kama siye?mbona tukienda ulaya na sie huwa tunakuwa watumishi tu wa ndani?au inakuwaje, hamuoni mifano hata kwenye tamthilia, wakaka wengi tu wanaoa watumishi wa ndani, aaaarghhh,, wasichana sijui watadhalilishwa mpaka lini

The best man is one who take care of his wife and chilldren ole wao wafanyao zinaa na kuwafanya wengine waangamie kwa maovu yao Baba yetu hatakuwa na huruma kwa watu hawa bali kwa kuomba msamaha kwa wale waliowakosea na hata kuwatendea mema wasibaki wakijuta kwa maumivu waliyopata..... huwezi kumwoa... unataka malezi ya baba na mama kwa mtoto..... mtendee mtoto wako haki ya malezi ya wazazi wake wote
Hapa nimekusanya tu baadhi ya dondoo ambazo Wana JF wanakushauri. Maoni yangu ni kama ya hawa walonitangulia. Ninachokushauri uzipitie tena hizi, bbadaye mwenyewe utaamua.
 
Kaka kwanza mshukuru mungu kwa kupata mtoto kuna watu wanatafuta sana watoto hawapati, pili wape wote huduma, mtoto na mama yake coz mwanamke ukishamzalisha (tena mwenye maisha ya chini) ni sawa na kumuharibia maisha yake kwani si rahisi sana akapata mwanaume atakayemthamini.
Tatu, wala usijiskie vibaya, kwani alikubaka? si ulimtamani na mkaenjoy tunda pamoja? iyo ndo result, ipokee kama zawadi, hakuna haja ya kufeel guilty hapo, na wewe sio wa kwanza (hata mahita alizaa na hg hahahaa), we jua tu "SHIT HAPPENS"
 
Maisha ni kweli nimemuharibia japo nami nimepata athari kutokana na kwayo,

Lakini katika suala la dhambi hilo kiimani kila mtu ana mbinu zake za kuomba msamaha...
Kumwoa hakika sintaweza kwakua bado nina kumbukumbu mbaya iliyokuja baadaye..
Yeye pia anajua na yuko radhi mie nipatapo mtu nimwoe,.@Mzizi

Kumbukumbu gani mbaya hiyo mkuu? funguka 2weze kukushauri.
 
Imenichukua muda kuisimulia hii hadithi iliyo ya kweli..

Nahisi ni mie mwenyewe katika dunia hii nilokumbwa na mkasa huu wa aibu na ambao sitausahau maishani..
Ama kweli sikusikia la mkuu na hayo yakanitokea na mpaka leo najutia..

Sikupenda iwe hivyo hadi leo wewe usome habari yangu hii lakini natazama na kwa mbali, maji yalishamwagika.

Walezi wangu waliniamini tangu nikiwa mdogo kuwa kijana mwema, hakika hawakukosea.

Kunipeleka shule nikatoe ujinga na kusoma elimu ya dini walinipatia.

Sikuwa mgomvi, mtukani wala jeuri ila kimoja tu kilinifanya kuangamia,

Dhakali iliyo ktk maungo yangu ilinitia topeni ikanichafua..

Kipindi hicho namaliza kidato cha sita binti mrembo nyumbani akaingia..

Si kwamba aliletwa nimweke gambani na kunililia..

Bali awe Dada wa kazi nyumbani kutusaidia..

Tamaa za tupu ya mbele zikanizidia, baadaye nikamwingilia..

Zikapita siku za kufurahia.. Aah kumbe machungu yaningojea..

Kaniita siku moja huyo dada/mpenzi akaanza kunambia..

Nimejaa my dia nataka kuitoa..

Wote nyumbani wakajua, nkabaki kuchukia binti kawa harufu mbaya sitaki hata akisogea..

Wote wakagundua vikao kukaliwa..

Binti akasanua ati mie ndo nilokamua,

sina la kuamua tusubiri kumpokea..

Mpaka sasa naongea mwana yu miaka tano..

Nimetaabika sana moyo wangu ukiungua..

Kumwoa sikupanga je? Nifanyeje kumlipia!

Nampenda mwanangu aishi kwa ulezi wa baba na mama..

MAMAYE KUMWOA SINTAWEZA...

Ushauri wenu utanifungua mawazo..

Wasalaam..

MKUU, nimesoma mkasa wako ulio ktk mtindo wa utenzi lakini nimeshindwa kukuelewa!!!!!! Utenzi wako unanionesha kwamba unajisikia hatia kuliko maelezo!!! Ningekuelewa kidogo kama ungesema ulikuwa na mke wako lakini ukazaa na housegal na sasa unajisikia hatia maradufu kutokana na kuisaliti ndoa yako!!!!! KIMSINGI, si-support hata chembe suala la wewe kutembea na housegal wenu (hata kama usingezaa nae) kv huwa si-support watu ambao ni opportunists!! Hata hivyo, am very concerned na vile unavyojikuta vile ulivyo na hatia kupitiliza!!!! Tell me, ni kv umezaa nje ya ndoa au kv umezaa na housegal?! Your child is FIVE years, na kutokana na maelezo yako, it's like hadi sasa hujaoa!! Then, tell me something bro; unataka kuniambia kwamba kwa muda wote huo hujawahi kutembea na msichana mwingine?! Kama YES, the well and good na una kila sababu ya kujiona very guilty kutokana na tukio la kuzaa na huyo housegal!!!! Kama umewahi, au bado unafanya; then tell me, hiyo hatia yako unayoihisi kwa kiwango kikubwa kiasi hicho inatoka wapi?! Jibu ninalopata ni kwamba unajihisi mwenye hatia maradufu kv sio kv ulizaa na housegal wenu; bali kv ulizaa na housegal.....it sound like she's nobody kuweza kuzaa na ww na ndio maana hutaki hata kumuoa!!! Kama hivyo ndivyo; unaweza kukwepa lawama kwamba ua opportunist?! I don' like the way u cry like ua a very innocent man; i don' like it coz' ua not but rather opportunist ambae una-take advantage of inferior women!!! Don' cry like a very innocent man while ua not! take things easy coz' ua not alone; even Omary Mahita, ex-IGP amezaa na housegal tena akiwa ndani ya ndoa; na amenyukwa faini ya millions of TZS baada ya kutaka kukataa!!!
 
Watoto wa shule za dini ndo zao.....kubanwa banwa ona sasa anatembea na hg. Nashauri amuoe dada huyo najua anachokataa labda ni muonekano wa dada, elimu, uwezo wa kifedha, nk. Vijana bwana, utaendelea kujuta tu kijana unapoteza muda. Tafuta kimeo kingine utacheki, kitazidi kukuchoma choma moyo. Tafuta mwanachuo ndo ulie mpaka ufe. Yaani unamtoto hutaki mama...dhambi gani hii?????
 
kaka kwanza mshukuru mungu kwa kupata mtoto kuna watu wanatafuta sana watoto hawapati, pili wape wote huduma, mtoto na mama yake coz mwanamke ukishamzalisha (tena mwenye maisha ya chini) ni sawa na kumuharibia maisha yake kwani si rahisi sana akapata mwanaume atakayemthamini.
Tatu, wala usijiskie vibaya, kwani alikubaka? Si ulimtamani na mkaenjoy tunda pamoja? Iyo ndo result, ipokee kama zawadi, hakuna haja ya kufeel guilty hapo, na wewe sio wa kwanza (hata mahita alizaa na hg hahahaa), we jua tu "shit happens"

cha ajabu unakuta huyo binti atapata mume na ndo jamaa linarudi tena mkia nyuma kutaka kutembea naye.....vijana bwana, dawa yao viboko tu pumbafu sana
 
Kaka usiwaze tulikua pamoja mi nilikua nadhani kwamba nipo peke yangu,ahaaha hhhhhhhh.sema mi wakati nipo form three ndio nilifanya tendo hilo aisee mtoto ni mkubwa na yule beki tatu alishaolewa kitambo na hatuna mawasiliano hata kidogo zaidi ya kuwasiliana na wazazi wa yule beki tatu tuuu.kaka angalia mbele ...............
 
Hapa nimekusanya tu baadhi ya dondoo ambazo Wana JF wanakushauri. Maoni yangu ni kama ya hawa walonitangulia. Ninachokushauri uzipitie tena hizi, bbadaye mwenyewe utaamua.

Nimepitia kila neno ambalo ndugu zangu mumenishauri, japo mengine yamekuwa ya ukali sana kwangu na wengine wamenisononesha sana kwa kunilaumu au hata kudhani sitaki kumwoa binti huyo ati kwasababu alikuwa housegal.
I believe in human kind and respekt to all, mie ni nani wa kujifanya ati ni binadamu bora?
Nilitenda hvyo nikijua ni housegal japo matokeo yalikuwa ya kuumiza zaidi kwangu na hasa kwake..
Nampenda na ntaendelea kumpenda siku zote kwa kunizalia na mpaka sasa kumlea mwanangu japo si kwa hali ile ya wengi tunavyoamini.
Napata huzuni hasa kwa kuzaliwa nje na pia mwanangu naye kupitia njia ile ile.
Najiamini mie ni mtu ninaejali sana utu heshima na haki za wanawake, japo kwa huyo nilimkosea sana..
Nawashukuru sana kwa urhauri wenu wa kujenga.
Nisameheni mwenzenu na nihukumuni kwa ubinadamu usio kosa kasoro.

'Man still a man wether rich or poor what we look is wether him good or evil.
Bless Idrens..!
Much love!
 
The best man is one who take care of his wife and chilldren ole wao wafanyao zinaa na kuwafanya wengine waangamie kwa maovu yao Baba yetu hatakuwa na huruma kwa watu hawa bali kwa kuomba msamaha kwa wale waliowakosea na hata kuwatendea mema wasibaki wakijuta kwa maumivu waliyopata..... huwezi kumwoa... unataka malezi ya baba na mama kwa mtoto..... mtendee mtoto wako haki ya malezi ya wazazi wake wote

thanks,
i like the way umeyapanga mawazo na kuhusianisha na mistari ktk vitabu tukufu..
Niko katika kipindi cha fikra kuu..
Nadhani nahitaji muda zaidi wa kuomba na kukaa kitako juu ya nini hatma ya suala hili.
Nategemea ntafanikiwa na ntakuja kuwapa nini ambacho nimeamua..
 
sometimes THE PAST CAN ENCOURAGE THE FUTURE

but sometimes THE PAST CAN DISCOURAGE THE FUTURE

kazi kwako
 
Kama unampenda penda mwoe.kama huna hisia nae mweleze kwa utaratibu akuelewe.na pia umsaidie katika maisha(katika kumsomesha au kumpa msingi wa biashara).kuhusu mwanao kumlea usijali.akipata mama mdogo mbona huwa wanaadapti malezi ya mama wapya mapema tu.ili mradi apewe upendo kutoka kwa huyo mama mdogo.wewe sio wa kwanza kuzaa na beki3 na hautakuwa wa mwisho.fanya kile hisia ya moyo zinakutuma.usije mwoa ukaishi maisha yote kwa kusononeka kuwa kama singezaa singemwoa.
 
Kipindi hicho namaliza kidato cha sita binti mrembo nyumbani akaingia..

Hivi inakuwaje wakati ajapo ulimuona binti mrembo halafu leo bila aibu unatwambia huwezi kumuoa!
Ni nini kinachokufanya usimuoe, si unajua umuhimu wa malezi ya baba na mama kwa mtoto? Unless...
 
Back
Top Bottom