Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Mimi ni muumini wa maisha mengine na majini. Stri hii nilikuwa naanza kuimini hadi ulipandika mwaka wa kufika Wajerumani Tanzania kuwa ni 1076. Wakati hu hakukuwa hata na Ujerumani! Wazungu wengi walikuwa wanaishi mapangni! Uliksea kutaipu?
 
Hicho kitabu Arsis alishakiongelea kwangu sana tu. Nikumbushe nilete katika safu mpya zinazokuja za "vionjo vya Arsis".

Ngoja nitafute mkanda wake.
Udafo: Si kweli kuwa Sunni wanawachukulia Sufi kuwa watu wasio na akili. Wanawaheshimu sana.
 
Nisahihisheni kama nakosea, lakini sisemi hivi kwa mihemuko, ila baada ya kufanya utafiti.
'Nimekuta Wakristo wengi Waafrika ni wajinga kupita kiasi, hasa inapokuja kwenye Uislamu, ambao uko kando yao tu. Ni kiasi cha kusoma tu. Badala yake wanaamini tu kikichwa kichwa wanayoambiwa Kanisani na Mapasta ambao wao pia ni wajinga. Si dhamira yangu kukashifu, bali ni dhamira yangu kuwaita kutumia akili. Akili ndiyo Mwenyezi Mungu ametutofautisha na viumbe wengine, na kwa sababu ya akili ndiyo atatuadhibu kwa kukosea. Akili ni kitu cha thamani sana sana sana. Usikubalii yeyote aitawale bila ya wewe kuitumia. Hata CCM!
Wajua katika Uislamu, Mwislamu anayejiita Muislamu kwa sababu tu baba yake au ukoo wake ni Waislamu, bila yeye mwenyewe kufanya utafiti na kuukubali....ana mapungufu makubwa. Mwenyezi Mungu amewakashifu watu hao aya : ' Wanasema, bali tunafuata tu yale tuliyowakuta wazee wetu wakiyafuata!"
 
Arsisi Allah atamdhalilisha kwa kutaka binaadamu wawaendekeze majini baada ya Mungu mmoja
 
Mmmm makubwa haya
 
Usipo taja ukristo unapungukiwa nini kama unaona uislamu unafaa acha kushupaza shingo komaa na dini yako mkuu itakupeleka peponi
 
Mimi ni muumini wa maisha mengine na majini.
Hapa umemaanisha nini kwa kusema wewe ni muumini wao?
Kufika Wajerumani Tanzania kuwa ni 1076. Wakati hu hakukuwa hata na Ujerumani! Wazungu wengi walikuwa wanaishi mapangni! Uliksea kutaipu?
Kwa mujibu wa historia mwaka huo hauko sawa. Lakini miaka hiyo wazungu hawakuwa wakiishi mapangoni.
 
Umefanya utafiti? 😆 Tueleze Hypothesis yako iliitwaje? Methodology ni zipi na sample ni zipi? Wakristo wapi, maana wako matabaka mengi kuna Catholics na Protestants, katika Protestants kuna Adventists, Lutherans, Anglican na mengine mengi sana.
Uli base wapi au uliwapitia wote, marejeleo yako ni yapi? Kama hauna hivyo vichache basi mkuu umetumia hisia na mihemko, na maneno ya kuskia skia.

Kama ulivyosema wakristo wengi ni wajinga hasa linapokuja suala la uislamu, pia na mimi naona waislamu wengi ni wajinga vilevile linapokuja suala la ukristo.
Mkuu mimi case yangu na wewe ni pamoja na matumizi ya neno utafiti, wewe hauna resource za kufanya jambo hilo.
Nipe hata list ya vitabu vya kufafanua uislamu na vinavyounga mkono uislamu ambavyo umesoma ukiondoa kitabu kikuu Koran takatifu.

Pia nipe chapisho au kitabu ulichosoma kinachoupinga uislamu, haya mambo yangekuwa mepesi kama unavyoamini watu wasingekuwa katika mkanganyiko wa kiimani unaouona.

Kwa hiyo mkuu na wewe kuhusu ukristo bado hauujui,na pengine haupaswi kuusoma ukifatilia dini yako vizuri usije ukachanganya mambo. Ndio maana mataifa yanayoendeshwa kiislamu hayaruhusu pengine kirahisi shughuli za dini tofauti na yao.

Kuna waarabu wakristo pale Lebanon zama na zama na wao pia unafikiri kwa miaka yote ya mwamko wa uislamu mbona wanabaki katika ukristo wao? Unataka kusema kule pia wanafundishwa na wajinga
 
Neno utafiti lisikufanye ukakosa hekima na kulifasiri tu kwamba ni lazima liwe na zana 1234. Utafiti unawezekana kuwa ni kufuatilia kauli za viongozi, wahusika na maamuma wa madhehebu kwa muda fulani na kutokana natija inayofanana.
Unazungumzia Wakristo Waarabu na mimi niliweka wazi kwa kusema 'Waafrika'. Hakuna Mkristo Mwarabu anayefunzwa Kanisani kuwa Uislamu ni dini ya Mapepo! Au Qur'an ina uhusiano wowote na Mapepo. Haya ni ya Wakristo wa Kiafrika tu. Hata Wazungu hawaamini hivyo.
 
Eeeh, hulka yangu kila nionapo kosa katika lugha ya Kiswahili ni kusahihisha. Nina maana, na hadithi ndefu juu ya hilo. Kifupi, kosa lolote katika lugha huenda likaharibu fahiwa au maana iliyokusudiwa na wazungumzaji aslia wa lugha hiyo.
Faiza: Ni kosa kusema 'dhehebu' hakuna 'singular form' ya madhehebu. Sababu: neno hili limeazimwa kutoka lugha ya Kiarabu namna hiyo hiyo- madhehebu. Hivyo: Madhehebu ya Sunni, Shia, Katoliki....nk. Kamwe hakuna dhehebu, kama ambavyo hakuna 'dini' kuwa ni singular ya 'madini' au 'ji' kuwa singular ya maji.
Najua matatizo yako na ya wengi ni kwamba aghalabu Kiswahili kinaunda 'plural' (wingi) kwa kuongeza 'ma'
Ila hapa si mahali pake.
 
Kuna tofauti kati ya 'demons' (mashetani, mapepo) na Majini (Jinns). Kwa ufupi, demons ni Majini waliomwasi Mwenyezi Mungu wakafuatana na Iblis (Mkuu wa Demons). Ama Majini ni wale walioendelea na hulka yao. Wao ni kama watu, kuna wema na wabaya.
Waislamu wanapozungumzia Majini ni tofauti kabisa na Wakristo wanapozungumzia Mapepo.
 
Sijui Wakristo wanajua hakuna 'Gospel' (Injili) ya aslia popote pale, zilizopo ni tafsiri tu. Na hao waliofasiri hawakuwa na 'Gospel' ya asli kabisa.
Gospel ni utunzi wa Mark, Luke, Matthew na John. Ukifungua Gospel Utasoma This is Gospel according to (kwa mujibu wa) St. Mark, au, according to St. Luke au according to St Matthew, au according to St. John.
Nataka Mkristo aniambie kwa nini ikaandikwa 'kwa mujibu wa'
 
So bloody.........(ongeza adjective)
 
Mkuu
Mkuu wakristo waafrika wa dhehebu gani?
Ndiyo maana nikasema huo uliouita ujinga, upo kila upande juu ya dini ya mwenzake. Isingekuwa hivyo probably watu wangefuata imani moja.

Mfano unaanzaje kuufanya uislamu thabiti ukiri dhana ya utatu mtakatifu na haipo katika kitabu chao, na unaanzaje kuufanya ukatoliki ukiri Mtume Mohammed (S.A.W) ni mtume wa mwenyezi Mungu na hayupo katika biblia, na kama yupo hawaoni jina?
Au Wayahudi na dini yao wakubali Yesu ni kristo, na hawakubali habari zake?

Jambo kama hili utaweza kulifanya kirahisi kwa muislamu mmoja mmoja na mkristo mmoja mmoja.

Biblia ina mistari mingi inazuia ushirikiana na viumbe wengine wa kiroho bila kujali ni wazuri au wabaya, sasa utawezaje kumfanya mtu alieshika biblia akubali kuwa ni sawa.

Hata humu unaona kuna baadhi ya waislamu nimeona kama wanasita pia kukubaliana na hii issue ya Arsis.

Lakini ukija kwa mtu mmoja mmoja kama mimi, napenda kujifunza maarifa naweza kusoma na kusikiliza nikiwa katika neutral ground
 
Ndio najua. Simba alishauliza zamani ataleta kisa chake hapahapa.

Simba anajua mambo mengi sana.
Nikusaidie, tena kwa elimu ya kusoma, si ya mazingaombwe! Kasha la Agano (Ark of Covenant) ambalo katika Qur'an limeitwa 'Tabuut' liko katika Kanisa moja la zamani sana kule Ethiopia. Kanisa hilo limechimbiwa chini ardhini. Au lilijengwa kutokana na kupasuliwa kwa mwamba. Hakuna ruhusa ya yeyote kulifungua kasha hilo isipokuwa makuhani watatu tu, hivi kwamba Condoleeza Rice, Waziri wa Marekani wa zamani wa Usalama, aliwahi kulifungia safari kutaka afunguliwe aone mabaki ya waliyaacha watu wa Musa (Moses), kama ilivyosema Qur'an.....lakini hata yeye alikataliwa!
 
Ayatul Kursi (Aya ya Ufalme wa enzi, kiti) Siyo Mursi! Huyu alikuwa rais wa Misi, akauawa na rais wa sasa Al-Sisi, ambaye mama ana urafiki naye, hata ameleta Wamisri wengi kuwekeza. Ni dikteta mkubwa, lakini: 'birds of same feather flock together'!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…