bolivia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2021
- 3,142
- 5,298
Kwanza poleni na harakati za hapa na pale kwenye kutafuta riziki.
Kwa kawaida huwa nawahi sana kuamka asubuhi sana na mapema kwa ajili ya kwenda kuweka mwili sawa kwa kufanya mazoezi ya hapa na pale. Huwa nakimbia half marathon eneo ninaloishi sio mbali na uwanja wa taifa. Nakimbia na kurudi nyumbani baada ya hapo ratiba zingine zinaendelea kwa kuwa naishi peke angu kama bachela nina uhuru na muda mwingi wa kufanya vitu kwa wakati.
Ubachela una raha yake kwa mbaliii japokuwa naona umri unaelekea kuwa kwenye mahusiano ya kudumu yani kutafutaa mke sasa tuweze kuwa wawili maana bado sijaona faida ya kubadili wasichana mara kwa mara magonjwa yamekuwa mengi sana.
Leo wakati wa asubuhi niliamua kwenda mimi mwenyewe sokoni (Tandika-stereo) kununua vifaa na mahitaji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani (chakula) huwa nikipata vijihela kidogo nanunua kwa jumla. Mabachela wenzangu wananielewa vzuri hapa. Sasa wakati nipo pale sokoni niliona vitu ambavyo dah nilipata surprise kidogo. Nilikutana na vijana wenye umri kama wangu kwa makadirio yetu wengi wetu ambao tumehitimu elimu ngazi ya degree 1(bachelor) lkn cha ajabu mle ndani wale vijana ambao ni tough guy na very handsome miongoni mwao sio mbaya kumsifia mwanaume mwenzio kama ni mzuri.
Wale vijana baada ya kuniona tu wakaanza kunifuata kutaka kunisaidia ile mizigo ya vyakula niliyobeba wafikishe nje ya soko angalau niwalipe ujira kidogo wa pesa kati ya elfu 1 hadi elfu 1500 inategemea na ukubwa wa mzigo
Wengine kazi yao ni kubeba magunia na kuyapakia kwenye magari, mwisho wa siku nikagundua nchi yetu bado ipo kwenye changamoto kubwa sana kwenye suala la ajira.
Mimi tu kijana mdogo nina gari ya kutembelea nimeingia sokoni naonekana tajiri.
NAIPENDA TANZANIA.