Niliyoyaona kule Ruvuma kupitia Luninga

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Jana kwenye taarifa ya habari ya ITV nilisikitika sana kuona darasa zima la watoto wakiandika wakiwa wamelala sakafuni kwa ukosefu wa madawati.

Mimi binafsi nawalaumu viongozi wakuu wa Mkoa ni aibu kuwa na viongozi katika Mkoa halafu watoto wanaandika wakiwa wamelala sakafuni.

Ushauri kwa Mhe.Magufuli. Usimteue Mkuu wa Mkoa, wa Wilaya na Mkurugenzi ambaye Mkoa,Wilaya yake ina upungufu wa madawati au atakapoteuliwa umpe muda ili kukamilisha madawati kwenye Mkoa, Wilaya yake vinginevyo utengue uteuzi wake.

Nawasilisha.
 
Kulikuwa na madawati mkuu, lakini hayakutosheleza idadi ya wanafunzi darasani. Ukisema darasa zima watoto walikuwa wanaandika wamelala chini sidhani Kama utakuwa sahihi. Tukileta taarifa hapa JF tujaribu kuepuka kupotosha jamii. Kwa sababu kuna watu hapa JF ndio platform yao ya kupata taarifa na mambo mengineyo.
 
Back
Top Bottom