Niliyoyagundua baada ya kuwatembelea wagonjwa Muhimbili

Bora hapo wanakutibu kwanza ndo wanaanza kukudai, hospital ya rufaa Mbeya wanakuandikia bill ulipe ndo utibiwe, majuzi nimempeleka dogo kapata ajali kapasuka kichwa, dakotari akiitaji panadol anakuandikia mkeka ulipie kwanza ndo upewe dawa
Very sad
 
Tatizo lenu mnakimbilia kuzaa pasipo kujipanga kiuchumi matokeo yake mnakuja kulalamika hapa jukwaani .
Ndo mjifunze.
 
Nimefanyiwa operation wiki tàtu zilizopita. Ganzi ilikua kuanzia makalioni Hadi miguuni kwa hivyoniliona kila kitu. Pale kwenye chumba Cha operation walikuwapo watu saba. Wengine walikua bizi na majukumu Yao lkn Kuna wadada walikua muda wote wanaperuzi simu zao.
 
Nimefanyiwa operation wiki tàtu zilizopita. Ganzi ilikua kuanzia makalioni Hadi miguuni kwa hivyoniliona kila kitu. Pale kwenye chumba Cha operation walikuwapo watu saba. Wengine walikua bizi na majukumu Yao lkn Kuna wadada walikua muda wote wanaperuzi simu zao.
Pole
 
1. Kwa wagonjwa wasio na rufaa ni ghali zaidi ya mara 3 ya private hospital
2. Sio hospitali ya wanyonge tena bali ya wenye fedha
3. Wagonjwa huzuiwa kutoka hospitalini hapo kama wanadaiwa na kushikiliwa hata kwa zaidi ya miezi.
4. Bima za NHIF husaidia dawa na vipimo vidogo tu vikubwa havipo
5. Huduma za uzazi (mama na mtoto) ni ghali mno

Habari kamili
1. Kama utapata ajali ya ghafla au tatizo lolote la haraka eti hupaswi kwenda direct muhimbili unapaswa uanzie Temeke, Mwananyamala na Amana ili upewe rufaa!.

Swali ni je mmeziwezesha hizo hospitali kuwaokoa wagonjwa walio ktk hatari kubwa za kupoteza maisha?

Eti kwakuwa tu huna rufaa ulipie gharama za matibabu mara kumi ya mwenye rufaa?

Is this fair

2. Sio hospitali ya wanyonge tena bali matajiri!
Nimemkuta dada mmoja kajifungua pre mature (7month) gharama alizoletewa(bill) ni zaidi ya milioni 8 na wamezuia asitoke hadi alipe na hana uwezo huu ni mwezi wa pili wakemshikilia.

Sio mmoja tu wapo wengi mno juzi kuna mmoja kataka kujirusha ghorofani kwakuwa kashikiliwa na hospitali kwa kyshindwa kulipa milioni tano huku hana mume kazaa na mume wa tu tu ambaye naye hana uwezo
Kuna marehemu kibao maiti zao zimezuiwa kupewa wasizikwe kwakuwa zinadaiwa gharama za matibabu.

3. Bima za Afya esp NHIF haina msaada wowote kwa mtanzania wa hali ya chini kwakuwa kifurushi chao hain vipimo vikubwa wala dawa za gharama.

Kuna kijana kaenda kupima ulcers kwa kushushwa mpira tumboni pale OGD_Ostra Genology Department, kile kipimo gharama yake ni sh 150,000/= pekee but hakipo kwenye bima.

Wanapatiwa dawa na vipimo ambavyo wanaweza kuvimudu wasivyoweza hawapatiwi na bima sasa umuhimu wake uko wapi

4. Ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020/2025 inaeleza wazi kuwa huduma za mama mjamzito na mtoto bi bure kabisa but ukienda pale martenity block utawakuta zaidi ya wanawake zaidi ya 50 ambao wamezuiwa kutoka hospitalini kwakuwa hawajalipa bill za huduma hiyo ambayo utashangaa kusikia mtu kajifungua anadaiwa zaidi ya milioni kumi jamani tanzania hii hii ya watanzania wengi wanaoishi chini ya dola moja?

Mwisho kabisa kama una sadaka yako unatamani iwafikie walengwa nenda hospitali watu wana shida aisee

Wagonjwa wameshikiliwa zaidi ya miezi miwili kisa wanadaiwa

Serikali itoe tamko wagonjwa wote walioshikiliwa Muhimbili kisa wanadaiwa waachiwe huru mana wanavyozidi kukaa pale gharama zinaongezeka na serikali inazidi kuwahudumia na kuzidi kuzidi kuongeza gharama ambao hawawezi kulipa sasa mtu kakaa mwezi kisa anadaiwa bado mnamwandika accomadation fee kila siku mna akili kweli?

Hayo ni baadhi ya mengi niliyoyashuhudia Muhimbili sio siri yamenitoa machozi but wote hao hawana sauti wala connection nani awasemee kama sio mtetezi wao?
Shukurani nyingi sana ndugu ulie leta andiko hili, ubarikiwe sana.

Natamani kungekuwa na oganaizesheni ambayo ingekuwa inakusanya majitoleo ya watu 5000 2000 ikifika kiasi fulani ikamtoe mgonjwa mmoja.

Kwa mfano mimi ni a 20,000 kulingana na uwezo wangi, ningetamani kuitoa hapo kusaidia chochote, lakini huo elfu 20 hafaidii kitu ikiwa single wako wakijitokeza kumi au ishirini wenye kiasi kama hicho walao itafaa kitu.
 
serikali iliyofeli inaongeza pesa kwa wanasiasa na kuacha kujali ustawi wa wananchi wao. Angalia wabunge (kikao cha wanaccm) kinavyotafuna pesa za walipa kodi.

ishu ya afya ni nyeti sana
Serikali ya ajabu sana.....hovyo sana. Inaongeza mzigo wa kulipa pension, gari kwa wenza wa waziri mkuu, makamu wa Rais watakapofariki. Huku wamama wanalala muhimbili kwa bill ya milion 1.
Saa100 na chama chake ni tatizo.
 
mimi nina bima nimekata bima timiza sh 987000/ tangu mwezi wa 4 mpaka sasa mwezi 11 haijafanya kazi nimeenda hospitali ya ccbrt kutibiwa magoti wanasema mpaka rufaa, nimeenda saifee hospital hawataki hata kuona, kwa sasa natumia pesa cash hospital ya saifee, ila sh 987000/ zimepotea sikati tena ng'oooooo
 
Na sio muhimbili tu Mimi nilishuhudia hospitali ya wilaya Misungwi mjamzito kagomewa kusafishwa baada ya kupoteza watoto wake mapacha ambao naweza kusema ni kwa uzembe wa wahudumu Mwisho wa siku wanadai elfu hamzioni bahati mbaya yule dada hakua nayo nakumbuka nilimuacha wodini sijui hatma yake ilikuwaje na hyo siku nilitafuta sana ule Uzi waziri Gwajima alijitokeza kuhusu ishu ya mtoto kulazimishwa kuolewa
 
Back
Top Bottom