Niliwahi kuchoma moto nyumba yetu ikateketea nikiwa mdogo

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Nitaeleza kwa kifupi sana!!

Nakumbuka nikiwa shule darasa la tano, dada yangu mkubwa alipoolewa wazazi wangu walipewa mahari ya ng'ombe 22, na mbuzi 5!

Baba yangu alikuwa mwalimu mkuu wa shule katika kijiji hiko, shule ambayo ilikuwa na walimu wawili tu yaani baba na mwalimu mwingine mmoja,

mama yangu alikuwa anatengeneza na kuuza pombe aina ya "kawanzuki" siku za gulio.
kutokana na mazingira hayo mimi nililazimika kutoka shule mapema kuwahi kwenda kupeleka ng'ombe na mbuzi malishoni (kuchunga).

Kwasababu hiyo nililazimika kubeba vitabu ili nikajisomee huko huko malishoni nikiwa nachunga.

Ikawa siku moja nikiwa malishoni nimekaa chini nasoma nikajisahau mifugo yangu ikaingia kwenye shamba la mtu, lilikuwa la baba mmoja mtata akanikamata akaniambia ile mifugo yangu ipo kwenye shamba lake la mahindi, alinicharaza bakora za kutosha! tangu siku hiyo nikachukia zoezi la kuchunga!

Nikamwambia mama hawa ng'ombe bora tuwauze tu mi sitaki kuchunga, mama nae akanicharaza! akaniambia hadi dada ako akizaa huko ukweni ndipo tunaruhusiwa kuuza au kuchinja!

ndipo nikazidi kuchukia kabisa!

Tukiwa machungani kulikuwaga na watu wakipita na noti za Tsh. mia mbili wsnanunua mifugo, nikapanga cku wakinipitia mimi
ningewauzia harafu nyumbani ningerudi na kuwaambia nimepoteza!

bahati mbaya wale watu hawakuja!
nikafikilia tena nifanyeje ili wajue sitaki kuchunga hii mifugo hususani mbuzi walinikera sana kwa mbio zao!

Ndipo likaja wazo la bora kuchoma ile nyumba ili baba auze mifugo ajenge ya bati!

Nikasubili cku ya gulio mama alikua kaenda kuuza kawanzuki, baba alisafiri kwenda mkoani kuangalia mshahara wake kama umetoka.

nikaamua kuchoma nyumba ikateketea yote, na vitabu baadhi vya shule vilihifadhiwa nyumbani vikawa vimeteketea!
Bahati mbaya wakati nikichoma nilisahau kuondoa uniform zangu,chachacha na madaftali yangu Viliniuma sana,Nililia sana;

Nilipiga kelele Wanakijiji walifurika kuzima nyumba yetu! hawakufanikiwa kuzima!
Hakukuwa na simu, Baba siku iliyofuata aliporudi akatukuta tumechuliwa na majilani!

Akasema mshahara haujatoka na nyumba nayo imeungua; Baba aliumia sana,!
Baba angu alisikitika sana akaamua kuwauza hao ng'ombe wote na mbuzi! akanipa adhabu ya kuhakikisha nakata nyasi ya kuezekea nyumba, mizigo 30 nilijitahidi nikakata nyasi mizigo 10 na bahati mbaya nikagongwa na nyoka nikiwa nakata, baba akaitwa akaja kunichukua wakanitibu kienyeji nikapona! Akanisamehe!

Niliendelea na shule,Darasa la saba nikafaulu peke angu kijiji kizima kwenda Technical school!......n.k

Hadi hivi leo wazee wangu wanakula matunda yangu na nimewajengea nyumba nzuri, pia nalisaidia taifa!

Najaribu kuwaza wangelinipa adhabu kubwa ya kukatisha masomo enzi hizo leo mm ningekuwa wapi?

Ndiyo maana huwa napinga adhabu kubwa kwa matukio kama haya ikiwemo ile azabu ya mimba mashuleni kufunga watu miaka 30!

Sheria zisigeuke mzigo! Kuna haja ya sheria kuangaliwa upya! makosa mengine yalipishwe faini ili ndugu na jamaa wajichange wakishindwa ndipo mtuhumiwa afungwe miaka michache!!
Kifungo cha maisha au miaka 30 tuwaachie magaidi!!

Note; Najutia kosa, Nilichoma nyumba ili kushinikiza swala langu lishughulikiwe, lakini zote zilikuwa ni hasira tu! binadam hukosea! Msamaha Wa mzee ulifanyika baraka kubwa sana kwangu!
 
pumbavu zangu, nngekuwa mzazi wako aise ungepaona nyumbani kwenu pachungu
 
Mkuu Mzee wako alikuwa na busara sana maana hayo mambo liofanya kitambo hicho yalikuwa hayavumiliki kwa akili ya kawaida.
 
Bora adhabu uliyoipata kwa kuchoma moto kuliko ungepigwa mimba mkuu...ktk swala la kuwasaidia wazazi ni jambo jema sana ndugu
 
Kwa hiyo tukupe hongera au? wewe mwenyewe haupo guilty kabisa sina shaka na wahalifu wengine hua kama wewe.

Pongezi kwa wazazi wako tho.
 
Duuuh aiseee, kwaiyo unajisifu kuchoma moto nyumba? Maaajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimependa sana hadithi yako. Nafikiri baba yako ana busara sana. Kama wewe ni Msukuma pia una bahati kwa wazazi wasukuma wana adhabu kali sana kwa watoto.

Ungaliweza ukavundikwa darini kama ndizi.

Pia kama umewajengea wazazi nyumba ya kisasa hongera sana. Natumaini utakuwa mtu mzuri na mzazi mwenye busara.

Ukishakuwa mtu mzima zaidi siku moja wape hii stori pia.
 
Back
Top Bottom