NAENDELEA PARTY 14
Narudi kwa ndugu yangu wa kagera nikiwa pale kwenye pool table yake, nilikuwa na nidhamu sana sana kila kidogo nilichopata nilikuwa nahakikisha nafika nacho home natunza zingne naweka kwenye simu.
Yule ndugu yangu wa pool table yeye alikuwa kaajiliwa ni askari shida yake pombe, mademu ilikuwa ni changamoto sana kwake anapenda mno, mpaka nafika umri huu sinywi pombe hata unipe za bure au unifungie nazo ndani mwaka mzima utazkuta nina nidhamu sn kwenye hilo, siendi bar wala grocery na ukiniona huko bs ujue kuna mtu kaniomba nimpe kampani tu, kuhusu mademu ni kawaida sn ila sina tabia ya kuhonga mwanamke akitaka kunifukuza alete pigo za kupewa hela hela naweza kumpa tu ila si yeye aniletee pigo za kutaka pesa yangu najiondoa.
Haya tuendelee nilisimamia ile pool table ndani ya miezi 4 nikanunua kitanda na godoro 5 kwa 6, nikanunua flat 32 inch smart kbs, then nilikaa tena miezi 2 nikachonga sofa kali ya L shape na kuweka subwoofer la seapiano sp912 nadhan mnalijua hili sub.
Sa pale kijiweni nikajiongeza nikaweka tupombe sungura napima na kuuza full at last nikanunua friji mtumba nikaweka vinywaji full, nikapambana nikaweka mabonanza ya kichina yale na si hilo tu nikaanza na udalali wa simu na tv, subwoofer nilikuwa nafanya research na kujua bei zake kisha natangaza anayetaka alete pesa nimletee mpk mlangoni.
Kimsingi nilipiga hatua sn eeeh watu wakaanza wivu pale kijiweni wakawa wanampanga ndugu yangu kwamba inaonekana kuna hela sn pale hiyo elfu 50 ninayompa ni ndogo mi napata hela sn ndo maana nina vitu sn.
Siku moja ndugu yangu akanambia wkend anataka asimamie mwenyewe pool table lake hapo nikawa nimeshamsoma kwamba anataka afanye uchungu kwa siku anaweza pata shs ngapi, nikamwambia poa kweli akasimamia wkend ikaisha mara akasema anataka awepo wk nzima nikamwambia poa ni yeye tu.
Nilichoamua hiyo wiki yote aliyokuwepo nilifunga biashara zangu bnafs nikawa siendi kabisa pale kijiweni nilitulia tu home kutafakari nawezaje kuachana na pool ya watu na kile kijiwe.
At last wk iliisha akaniambia nimpe elfu 60 wa wiki hapo niligoma niliamua kumwambia mi tampa elfu 40 kuanzia J mpka jmos tampa elfu 40 then jpil yeye aje akusanye pesa yote akasema sawa.
Niliendelea kupga kazi kwa tahadhari sn ulipita kama mwezi huyo ndugu yangu akaja na hoja nyingne kwamba kapata mtu wa kusimamia na wamekubaliana ampe elfu 70 kwa wiki na wameshajaza mkataba mmmh hapo nilimgomea nikamwambia ww ulinipa hii table ndani ya miezi 6 ulikuwa umesharudsha pesa uliyonunulia na ww ndiye uliniomba nije kusimamia leo unataka kuniachisha kienyeji una shida gani ww aisee yule ndugu yangu hakunielewa kabisa.
Basi nikamwambia nipe wk 1 kisha mlete huyo mtu wako umkabiz kiroho safi. Hiyo wiki moja niliitumia kujiandaa kuhamia sehemu nyingne nikapambane kivyangu, kweli wiki iliisha nikamuita nikamwambia mlete huyo mtu pool yako hii hapa hatudaiani kbs nikamshukuru nikamkabizi.
Mimi niliamua kuondoa biashara zangu zote kwenye eneo lile kisha nikasepa zangu skuwahi kanyaga tena pale kwenye kile kijiwe aisee.
Ajabu siku moja huyo ndugu yangu akanipgia simu kwamba kuna jambo anataka nambia anataka tuonane mmmh ilinistua sn kunani tena.
Zilipita siku kadhaa hatuonani niliamua kumpgia simu anieleze kuna nn.
Eeeh nashangaa na kwa maskitiko makubwa sna akadai kwamba mimi kuna watu nimewaambia kwamba yeye atakuja kufa na ukimwi kama mama yake ( RIP AUNT YANGU ) nilistuka sn nikambana aseme nani kasema hayo akagoma anasema tu watu wa kijiweni pale, nikamsihi sn basi naomba umuite mtu huyo aje tuzungumze friendly aseme wp nilitamka maneno mazto kama hayo pia akagoma bt ukweli kbs sjawahi zungumza kitu kama hicho kwa mtu yeyote sjawahi na siwezi ila nilikuja kujua kumbe aliambiwa na mkewe kwamba eti ameskia kwa watu mi nasema hivyo na huyo mkewe akapga mpka simu kwa baadhi ya ndugu zetu akisema mimi nimemwambia hivyo ndugu yangu daaaah 😴😴😴😴😴.
TAENDELEA
Mjue nini kilijiri