NAENDELEA PARTY 2
USIKU MMOJA NAKAMATWA ETI NIMEIBA MEZA YA WATU YA BIASHARA
Usku mmoja nikiwa narudi home nimechoka nina njaa kiu hopeless nikawaza nyumbani kuna viunga vilibaki nikifka nikoroge uji bila sukari ninywe maana najua mwanamke wng atakuwa kapka na hajanibakizia kitu.
Nikapata wazo nikakope vimchele nusu na mafuta hata ya 200 nikifka nipike, kweli nilipata ila sasa moto wa kupikia natoa wp🤔 wakati nipo njian nawaza hapo ni usku wa saa nne, nikapata wazo nitafute vikuni nifke niwashe nipike.
Wakati natembea njian nikaona limeza bovu bovu la mbao lipo njiani aaah saa ngapi nisilibebe ili nipate Kuni nikiwa natembea mdogo mdogo nmekaribia kbs home nashangaa jamaa mmoja mbavu ananisimamisha na kunihoji meza nimetoa wp hiyo ni meza ya BIASHARA ya ndugu yake.
Nikiwa bado najitetea sn kwa huruma labda jamaa anielewe kwamba mi nina shida tu jamaa akasema turudi nilipoitoa.
Na pana umbali nikaongoza njia mpka nilipoitoa akampgia simu mwenye mali aje haraka mwizi wa meza yake kakamatwa jamaa akasema huyo mwizi mlete nyumbani.
Nikabeba tena mmeza mzito tukapga masafa mpka huko kwa huyo mwenye meza aisee akanihoji hoji pale kisha akanambia beba hiyo meza ipeleke sehemu fulani kisha uende zako.🤲 Nikashukuru nikabeba na kuipeleka alikosema nikasepa..
Zangu mchele wenyewe ulidondoka huko njiani wakati nimekatishwa na yule jamaa na skuupata nilifika home mwanamke kalala na hakuna menu nikacheck nikaona ukoko wa ugari uliomwagiwa maji nikachukua nikala tena upo kwenye maji machafu skuwa na namna nikanywa na maji nikalala.
TAENDELEA...