Hussein Mbega
Senior Member
- Jun 7, 2026
- 180
- 411
Mkuu,
Tunasubiri.
Tunasubiri.
Bulooangu aweke wazo aiseehe mimi nifanyie yote hayo ila mapaja utanue tu sitalalamika hata😁😁😁 Blaza blooo!!
Umetisha ChampSa why not 🚫 mjomba 🤔 mbususu haina uhusiano na hali ya mtu uwe nazo au usiwe nazo muhimu mwanamke akuelewe , kama unabisha pata mwanamke awe na hisia na ww akupende ndo utajua kumbe na wao wanahonga...
Formula yangu sihongagi mwanamke ila natongoza anielewe kama ni hela nimpe tu kwa kuamua si kumuhonga au kumnunua, so nilikuwa nachakata tena nilipata mtoto mzuri kbs mjita mmoja mbichiiiii..
Sijui nani aliimbaga haka ka wimbo....Kama una watoto wa kiume,waombee sana...
Muendelezo tafadhariSijui nani aliimbaga haka ka wimbo....
Wanaume tumeumbwa...
Matesoooooo......
Matesoooooo.........
Hallelujah¡¡¡ hallelujah¡¡¡ hallelujah¡¡¡ MUNGU wetu asitaaaaaahiri sifa...Muendelezo tafadhari
Daah stori yako ni ya mateso sana. Aisee wanaume twapitia mengiNAENDELEA PARTY 8
Kwanza nirudi kwa yule dada J nini kilifanyika baada ya kuwa mm nimefukuzwa kazi kwasababu ya roho yake ya kwanini, kwani niliskia kwenye kikao akisema eti imekuaje mi naanza tu kazi nalipwa laki 4 wakatu yeye alianza kwa kujitolea tu kwanini na mimi nisijitolee kwanza.
Kumbuka hapo hata hajui mimi na mzungu tumetoana wapi anasahau pia mimi nilikuwa namzd elimu mbali sana maana yeye alikuwa na certificate tu ndo alikuwa anasaka diploma.
Aisee yule dada J alileta rafiki yake pale ofisini ndiye akawa mtu wa marketing na yeye J akarudi kukaa ofisini.
Ni kweli ambavyo nilinena haikupita hata miezi 2 naye akatimuliwa kwa kutia hasara kampuni yeye pamoja na shoga yake wakapgwa chini.
Haya turudi sasa baada ya kufukuzwa kazi sasa maisha yalikuaje kwa kifupi nilirudi kwenye msoto usio wa kawaida kabisa sikuwa na wa kunitia moyo maisha yangu yote, mama yangu alituacha tukiwa wadogo sana tumelelewa kimafungu mafungu tu yeye mama alirudi kwao huko akaolewa akasahau kabisa kuhusu watoto wake. ( Hii story taileta kivyake kuhusu mama na uhusiano wangu na mzee aisee watu wana roho mbaya sana ).
Ok nikiwa sina kazi rasmi sasa hapo mwanamke hajui kitu na niliapa sitamwambia maana nilijua akijua ataniongezea stress tu.
Kale ka hela nilikobakiza kama laki 2, nako siku 1 mchungaji akaniita kwake akaniomba niwaazime kanisani shs 150,000 baada ya wiki 1 itarudi nikasema hiyo sawa nikampa nikitegemea ni waaminifu itarudi mfukoni nikabaki na elfu 40 tu, wakuu skulipwa pesa yangu yaani skurudishiwa mpaka kesho alooo.
At last nilichafuliwa sana na mchungaji kwa washirika maana niliamua kuachana na mambo ya kanisani kabisa maana niliona kumbe hata hawa wachungaji nao ni walewale nikaamua jifunza kufanya meditation tu siyo mambo ya dini tena.
Msoto ulikuwa heavy skubadili ratiba ya kutoka home nilikuwa natoka kama kawaida alfajiri sn kama naenda kazini kumbe naenda town kutafuta kazi mwanamke ye anajua mi naenda kazni.
Mfumo huo nilienda nao karibu miezi 3 iliisha anaona tu mi natoka kwenda kazini kumbe wapi, akiniuliza salary namwambia kampuni imepigwa faini ya kodi hali si nzuri boss kasema tuvumilie atatulipa malimbukizo yetu.
Ikafikia hatua sasa ya kutembea sina kitu mfukoni naikumbuka na hela yangu niliyoazmwa daaah.
Nikawa natoka alfajiri natembea kwa mguu toka goba napita makongo juu to mlimani city mpaka mbezi stand nakanyaga tena mpk kkoo au naamua kuzuga zuga hapo mbezi stand kama nasubiri usafiri wa kwenda mahali kumbe mi na gain time tu muda usogee sogee naposema mbezi namaanisha stand ya mbezi kabla haijaamishiwa makumbusho enzi hzo.
Nilipgika viatu vikaisha, nguo zkachakaa sina wa kunisaidia wala kunionea huruma njaa yangu, jua langu, kiu yangu, joto langu.
Wakati mwngn naishia pale udsm nazama kwenye miti miti kule natafuta sehemu nakaa peke yangu nalia sana kimoyo moyo nafanya meditation mpk nasinzia huko aloooo alooooo...
Sasa nikaanza kuwa siku zingne nabaki home tu.
Je nn kilijili sasa nilipokuwa nikibaki home pale sku moja moja...
TAENDELEA....
🙆NAENDELEA PARTY 12
Nilipofika hapo kwa ndugu yangu mwanza aliyesema mwanzo kwamba nitafute pa kulala, story story kweli kesho yake yule sister alifika na nilimpokea kule kazini akiwa na matumaini kibao akiamini sasa kazi kapata maana kama ameambiwa aje kazini reporting.
Nilicheka sn kimoyomoyo nikamwambia hapa hamna kitu hapa hawa wanatupotezea muda wetu tu hapa akawa kama anataka kuni mind kwamba yaani mi nipo tu kama yeye anayajuaje mambo ya ndani ya ofisi kwamba kaz ipo au hakuna nikamwambia poa basi haina shida tukae ipo siku utayakumbuka haya niliyosema.
Siku zilianza kusonga sasa huyu sister nikawa nashinda naye kule ofisini na bado home kule kwa ndugu yetu tunaenda wote daaaah issue akaja nauli na menu lazima ni msupport maana yake hata pale kwa ndugu yetu nikawa napambana kwa washikaji ninafahamiana nao hasa yule jamaa yangu niliyefikia kwake wakati natoka dsm alinisaidia sn kiukweli hela ya kununua vimboga na unga nikawa natoa pale ila kwa machungu sana.
Likatokea zali kuna kazi za muda mfupi zilitokea za wizara ya afya za kwenda kufanya research ya chanjo mikoa tofauti tofauti yule bro wa kazi akaniunganisha huko nikapata na nilienda mkoa wa shinyanga nilipiga kazi huko wiki 2 na nilipata kama laki 5 ya faster.
Niiporudi nikawa nishaamua tu kuanza maisha yangu kazi hapa uzushi tu, nilinunua godoro, jiko la gas, vyombo kadhaa na nikabakiza kama laki 1 ya kodi.
Sa wakati natafuta chumba mwanza nikakumbuka kuna ndugu yangu 1 alikuwa mkoa wa kagera huko wilaya fulani na kipindi fulani aliwahi nishawishi sn niende nikampe hi, niliamua mtafuta tukaongea na nikampeleleza khs hali ya huko na gharama za maisha kwa ujumla akanambia we njoo tu gharama za maisha huku ni simple sn vyumba vipo mpaka vya ten na kina umeme, maji yapo ok.
Niliamua kwenda huko haraka sana na wakati huyo yule dada aliyekuja kwaajili ya kazi naye alisharudi huko kwake, nilifungasha vitu vyangu safari ya mkoa wa kagera ikaanza nilifika jioni sn na huyo ndugu yangu alikuwa kazini maana ni askali so akaniunganisha na mkewe akanipokea.
Nilipumzka pale siku kadhaa kwa ndugu yangu ili niendelee kuyasoma mazingira ya mji na tabia za watu wa mji ule na nijue nafanya nn sasa ili kupata kipato.
Alooo nilikuja kugundua shemeji yangu ni noma na ndugu yangu alishamalizwa kbs hana say si mnajua wahaya wakuu ni noma wanawake wa kihaya mnisamehe sana.
Nilianza kutafuta room haraka sn aisee nikishirikiana na huyo ndugu yangu nilipata room nikahama pale maana niligundua yule shemeji yangu tungekosana mapema sn maana bnafsi spendagi mambo ya kijinga jinga kabisa na ukimya wangu si wa kizuzu
Alooo TAENDELEA
Napo majanga yalianza huko kagera kati yangu na ndugu yangu...
Kubwa sana hiiKama una watoto wa kiume,waombee sana...