Kisa: Nilivyowahi maishani

Kisa: Nilivyowahi maishani

Hii story kama vile niliwahi kuisoma sehemu fulani kwenye forum. Inaonekana kama ni ile ile au imefanana sana na niliyowahi kuona!
Uliisoma humu na mwandishi ni mimi sema nilikuwa naandika katikati ya visa vya watu saivi ndo nimeamua kuandika kbs nina matukio mazito mpk ya huyu mwanamke ninayemsema humu.

NB: kama na ww unadhan nimecopy pambana utafute hicho kisa halafu uangalie mwandishi ni nani uzuri wapo raia humu wanafahamu visa vyangu watasema kama si mimi.
 
NAENDELEA 4
NILIAMUA KUFANYA KAZI YA KUSAJIRI LINE NIKAISHIA NDANI..

Wakati naendelea kupambana siijui kesho yangu sina wa kunionea huruma. Nilikutana na dogo mmoja anasajili line nikamuuliza hii kazi unafanyeje , akanipa maelekezo na vigezo uzuri nilikuwa navyo nikaenda aliponielekeza.
Walinipokea wakanisajiri kisha wakanipa smartphone mpya ya kufanyia kazi rasmi nikaanza kutembea mitaani maeneo ya Riverside nasajili line huku nawaza ikitokea nimekutana na wanaonijua tawaambia nn kiukweli yalikuwa mateso tu.
Unazunguka chocho kwa chocho na hupati kitu home nako hamna kitu.
Bado natembea kwa mguu toka goba mpaka ubungo kila sku kuwahi ofisini. Nikapata wazo kwamba liwalo na liwe mi nauza hii smart nitimize mahitaji yangu na family pia hasa mtoto kweli niliuza kisha nikapotea hewani.
Jamaa akaanza kunisaka goba huko anazunguka kuniulizia ila hakufanikiwa kunipata, ulipita kama mwezi 1 nikakutana naye mbezi luis akasema yeye anataka simu au twende polisi nikamwambia simu sina na nikampa hali halisi akalazimisha twende polisi basi tukaanza enda.
Nikapata wazo huyu nimkimbie tu si nikamchomoka akaniitia mwizi mara kuna raia walikuwa wanafyatua matofari wakaibuka na nyundo, mawe, mafimbo nk nikasimama nikawaambia mimi siyo mwizi aisee na nikaelezea situations yote jamaa wakatulia tu wakashauri at last mwenye simu akakomaa polisi kweli kwa mara ya kwanza nazama ndani mahabusu nikakutana na vijana wamepinda mle, harufu kali, ndoo la mavi humohumo mtu anajisaidia hapo pembeni huku watu wanakula kando, funza kama wote, usku mnajazwa kama mizigo plus joto la dsm ooooooh.

Nilikaa kama siku 5 hivi sina matumaini kabisa mwanamke akija ananitolea maneno makali mi kimya tu, siku moja akaja mpelelezi akanitoa akanipiga pingu uelekeo kituo cha polisi shekilango, tulifika kule akanihoji kisha kuna ndugu yangu mmoja akanizamini nikatoka.
Ila kesi iliandikwa nadaiwa hela mi nilikataa sababu nilikuwa nadaiwa simu tu si pesa at last tuliyamaliza mimi na mwenye simu nilimpa property yangu 1 hivi kesi ikaisha.
Siku narudi home mwanamke ananifukuza na ilikuwa usku wa saa sita nikazungumza naye kumtuliza kidogo akawa mpole, kuna ndugu yangu huyo aliyekuja kunidhamini wakati nipo ndani kumbe yeye na mwanamke wangu wananisema mpk mambo yakafika home eti mi ni tapeli mwizi nimefungwa aisee ila binadamu bhana 🥺 ila yalipita na nipo imara sn na mwenye nidhamu kubwa mno.

TAENDELEA..
Pole sana mwamba!
 
Uliisoma humu na mwandishi ni mimi sema nilikuwa naandika katikati ya visa vya watu saivi ndo nimeamua kuandika kbs nina matukio mazito mpk ya huyu mwanamke ninayemsema humu.

NB: kama na ww unadhan nimecopy pambana utafute hicho kisa halafu uangalie mwandishi ni nani uzuri wapo raia humu wanafahamu visa vyangu watasema kama si mimi.
mkuu wangu lete story achana na hao

yaan ni episode chche umeleta lakini zina funzo kubwa napendekeza ungekuwa unaelza kwa kirefu zaidi na ufafanuzi

hao waduanzi wapo tangu miaka na miaka humu
ambao wanagezana yaan wakiona mtu kaongea kitu furani basi nao hufuata mkumbo kuongea

so shusha story mkuu wangu
 
NAENDELEA PARTY 7
YALIYONIKUTA PALE OFISINI KWA MZUNGU BAADA YA MIEZI MIWILI TU YA KUANZA KAZI

Ilikuwa ni ofisi ya kukodisha magari na ilimilikiwa na huyo mzungu mwanamke, pale ofisini nilikutana na madereva ambao ilibidi wawe marafiki zangu sana maana mi ndo nilikuwa naamua mtu uweke mafuta kiasi gani au ufanye uhuni upate chochote kupitia mafuta yaani ile naandika full tank lakini siyo full ni nusu tu. Michezo hii niliiepuka sana.
Pia nilimkuta dada mmoja wa kiarusha kama mmsai fulani hivi ila hakuwa mmasai jina linaanza na J, alinipokea pale akapewa jukumu la kunielekeza baadhi ya mambo ya pale ofisini ukizingatia pia ndiye aliyekuwa kwenye kitengo nachoenda fanya kazi, yeye alihamishiwa kitengo kingine cha masoko.

Nilikuta pia anasoma CBE kuongeza elimu yake na kidogo nilikuwa nampa kampani kwenye hayo mambo yake ya shule naye kwa kiasi fulani alinielewa ila bnafsi sikuwa na mpango wowote na yeye.
Baada ya siku kadhaa za kunielekeza mambo kadhaa ya kiofisi yeye akahamishiwa kitengo cha marketing huko alipewa gari na dereva kila sku kumzungusha kwenye maofisi huko town kisha jioni kurudi na kujaza tu kwenye fomu maalum ya ofisi kwamba kapita wapi na wapi na kajibiwa nn, nadhan mnaweza ona hapo jinsi kazi ilivyokuwa rahisi kwake.
Kumbe yule dada J hakufurahushwa na hicho kitengo yeye alitaka kubaki ofisini pale na yule mzungu hakumtaka pale ofisini maana pia alikuwa mvivu sana na majungu mengi sn so kelele zlikuwa haziishi ofisini na madereva.
Sasa kuna matukio yalianza kuwa yanajitokeza kwenye utendaji wangu wa kazi mojawapo nilikuwa nikifanya kazi zangu kwenye pc kesho yake nakuta zimefutwa zote na mzungu akawa ananilalamikia mbona naonekana nafanya kazi lakini kaz hazioni nikamwambia hata mimi sjui labda kuna mtu anafuta maana kiukweli mi kazi nafanya sana tu na hata yeye alikuwa shahidi.
Nikaja kubaini aliyekuwa anafuta ni huyu mdada J lengo nionekane sifanyi kazi kabisa nifukuzwe yeye arudi pale ofisini. Tulipokuwa tunaondoka yeye anabaki ofisini ndo mambo aliyokuwa anafanya pale ofisini.
Kingine nikaambiwa na mlinzi huyu dada huwa anabaki hapa ofisini mpka usku sana na huwa anamwaga madawa hapa ofisini mmmmh.

Alikuwa anaaga hata wiki nzima hayupo na haijulikani alikuwa anaenda wapi na anapokuwa hayupo ofisini kunakuwa na amani sana na hata boss anakuwa si mkali kabisa. Ila akirudi tu panachafuka sana ofisini kelele nyingi sana na uwezo wake wa kazi mdogo mno.
Kwa hisia zangu alikuwa mtu wa waganga sana ni kama alikuwa ameshamteka mzungu kila anachoambiwa na yule dada J ni yes.
Kazi kwangu ikawa kama mzigo sasa maana boss akawa mkali sana visa vingi sana yule mdada akawa anampanga kuhusu mimi kwamba nifukuzwe kazi tu ili yeye mdada J alete mtu mzuri wa kufanya kazi ya masoko na yeye arudi ofisini.

Mambo haya nilikuja kuyagundua nimechelewa sana maana nilimskia kwa masikio yangu akimwambia yule mzungu kwamba tayari kapata mtu wa marketing kwaiyo anaweza tu kuniondoa.

Nilipoyaskia hayo skuwa na papala sana ukzngatia mimi ni mtulivu sana, nikaanza kujipanga kwamba nikitoka hapa hata sjui naanzia wapi, sku moja mzungu alinikabiz milion 24 za kulipia gari kuna mtu angekuja kuzichukua kwangu pale ofisini na ofisn nilikuwa nabaki peke yangu tu.
Kuna wazo liliniijia kabisa kwamba kwanini nistoroke na hzi hela tu maana najua hapa siku si nyingi takuwa sina kazi nikawaza kabisa nitoroke na pesa hata nizamie mikoani huko nikapambane.
Ila sababu haikuwa tabia yangu niliondoa maamuzi hayo.

Hatimaye mwisho wa mwezi ulifika mzungu akaitisha kikao cha wafanyakazi wote tukazungumza meengi ila hoja ilikuwa ni mawili tu kuachishwa kazi au kuwa chini ya yule dada J aisee niliskia uchungu sana sku hiyo na tayari nilishakata tamaa kabisa ya kuendelea kufanya kazi nilimwambia mzungu nilipw mashahara wangu niache kazi leo hii.
Na nikasema hadharani namjua anayefanya haya ni J ila namuhakikishia kama Mungu aishivyo mwezi haiutaisha naye atafukuzwa hapa hawez kudumua hapa.
Nililipwa pesa zangu za mshahara nikaondoka zangu nikaenda kukaa mahali nililia sn kwa uchungu kimoyomoyo mpaka usku ndo nilirudi home nikiwa na uchungu sana skumwambia mwanamke nilinuunua mahitaji ya home kama ya laki 2 hivi kisha nusu ya pesa hiyo niliifanya kama akiba ya kuwa nazungukw town kutafuta kazi tena...

TAENDELEA NINI KILIFATA SASA BAADA YA KUPOTEZA KAZI..
 
Back
Top Bottom