Lamomy
JF-Expert Member
- Sep 4, 2023
- 39,429
- 94,851
Acha kunifananisha fananisha hebu 😹😹Kuna bidada umefanan nae sana ni mke wa david sportwear. Duka lake linaitwa Kariakoo bag liko Tandamti pale unamjua?
Acha kunifananisha fananisha hebu 😹😹Kuna bidada umefanan nae sana ni mke wa david sportwear. Duka lake linaitwa Kariakoo bag liko Tandamti pale unamjua?
Inasikitisha... sanaNimesikia maumivu moyoni

daaaaaah uyo mwanamke alikosea sanaNAENDELEA PARTY 3
NATELEKEZEWA MTOTO MCHANGA WA MIEZI 2.
Aisee siku usku nilirudi na unga wa ngano na mafuta na sukari nikiwa na lengo la kutengeneza maandazi ili angalau cha kutafuna kiwepo home hata kama mwanamke ataamua kupka kivyake bs na mimi niwe na cha kujishikiza.
Nilifika home saa 5 usku nikawasha jiko, nikakanda unga bahati nzuri mwanamke naye akaamka akawa ananisemesha hapo namjibu vzuri ukzngatia pia mi ni mkimya sn skuwa na ugonvi naye wala.
Huku nachoma maandaz yangu mdogo mdogo mpka namaliza yeye kalala, kumekucha akajiandaa kwenda kazn kwake na alikuwa anaondoka na mtoto anamuacha kwa mama ake mdogo, nikiwa ndani na mtoto naona kimya mtu harudi ndani.
Kumbe ameshasepa katoroka mtoto ana miezi 2 tu mara mchana huo mtoto analia njaa hatari sn nikapata wazo nimkorogee uji mwepesi sn nimnyweshe yes nikafanya hivyo kwa tahadhari sn kakanywa kakalala mara jioni hii mara usku huu sioni mtu kurudi home.
Nikakapa tena uji kakanywa kakalala kesho asubuhi kimya sioni mtu nikaenda kutoa taarifa polisi na nikamwambia na mama yake kuptia simu, bs sku ya pili tena kimya nipo na kichanga nalala njaa nashinda njaa ndani kuna viunga ndo natumia kudanganyishia mtoto siwezi vitumia mm.
Siku ya 3 mchana napigiwa simu namba mpya na mtu aliyejitambulisha ni polisi kwamba nashitakiwa na mdada mmoja akamtaja majina ni yule demu wangu nashitakiwa eti nimempga wakati skumpga na usku tulilala vema tu tena kwa amani.
Nikamjbu polisi mi kuja huko haina shida ila shida huyo mdada kaniachia mtoto wa miezi 2 natokaje sasa kuja huko, nikasikia wanamfokea kwann kaacha mtoto mchanga simu ikakatwa.
Usku wa siku hiyo alirudi kwa kuletwa na mama mchungaji wake na mama mwngn usku wa saa saba nagongewa mlango hapo mtoto ana sku 3 hanyonyi..
Wakanisihi niwe mpole tu kwani wameshamkea mi nilinyamaza tu akaingia ndani ananuka majasho hatari sjui huko alikuwa haoigi.
Kesho yake namuhoji ulienda wp akadai aliamua kuondoka na kupanga chumba kuanza maisha yake yaani anaongeaongea tu ujinga wakati vitu vyake vyote aliacha home nilipo.
ITAENDELEA...
Alikuwa depressed, kulea halafu mshikaji ramani ngumu sio lele mama.daaaaaah uyo mwanamke alikosea sana
inasikitisha mkuu unakuta mtu anateseka duniani na bado anajiogezea matatizo kwa kuvunja amri za M-nguInasikitisha... sana...
Kuna wanasema ID yangu ni Yako 😅Acha kunifananisha fananisha hebu 😹😹
Eehh..!! 😹😹Kuna wanasema ID yangu ni Yako 😅
Basi na sisi wadogo zako tuko 🔥🔥🔥Eehh..!! 😹😹
Basi nitafananishwa na wengi humu ndani..!!
huu ulikua msoto kwel kwlNAENDELEA 4
NILIAMUA KUFANYA KAZI YA KUSAJIRI LINE NIKAISHIA NDANI..
Wakati naendelea kupambana siijui kesho yangu sina wa kunionea huruma. Nilikutana na dogo mmoja anasajili line nikamuuliza hii kazi unafanyeje , akanipa maelekezo na vigezo uzuri nilikuwa navyo nikaenda aliponielekeza.
Walinipokea wakanisajiri kisha wakanipa smartphone mpya ya kufanyia kazi rasmi nikaanza kutembea mitaani maeneo ya Riverside nasajili line huku nawaza ikitokea nimekutana na wanaonijua tawaambia nn kiukweli yalikuwa mateso tu.
Unazunguka chocho kwa chocho na hupati kitu home nako hamna kitu.
Bado natembea kwa mguu toka goba mpaka ubungo kila sku kuwahi ofisini. Nikapata wazo kwamba liwalo na liwe mi nauza hii smart nitimize mahitaji yangu na family pia hasa mtoto kweli niliuza kisha nikapotea hewani.
Jamaa akaanza kunisaka goba huko anazunguka kuniulizia ila hakufanikiwa kunipata, ulipita kama mwezi 1 nikakutana naye mbezi luis akasema yeye anataka simu au twende polisi nikamwambia simu sina na nikampa hali halisi akalazimisha twende polisi basi tukaanza enda.
Nikapata wazo huyu nimkimbie tu si nikamchomoka akaniitia mwizi mara kuna raia walikuwa wanafyatua matofari wakaibuka na nyundo, mawe, mafimbo nk nikasimama nikawaambia mimi siyo mwizi aisee na nikaelezea situations yote jamaa wakatulia tu wakashauri at last mwenye simu akakomaa polisi kweli kwa mara ya kwanza nazama ndani mahabusu nikakutana na vijana wamepinda mle, harufu kali, ndoo la mavi humohumo mtu anajisaidia hapo pembeni huku watu wanakula kando, funza kama wote, usku mnajazwa kama mizigo plus joto la dsm ooooooh.
Nilikaa kama siku 5 hivi sina matumaini kabisa mwanamke akija ananitolea maneno makali mi kimya tu, siku moja akaja mpelelezi akanitoa akanipiga pingu uelekeo kituo cha polisi shekilango, tulifika kule akanihoji kisha kuna ndugu yangu mmoja akanizamini nikatoka.
Ila kesi iliandikwa nadaiwa hela mi nilikataa sababu nilikuwa nadaiwa simu tu si pesa at last tuliyamaliza mimi na mwenye simu nilimpa property yangu 1 hivi kesi ikaisha.
Siku narudi home mwanamke ananifukuza na ilikuwa usku wa saa sita nikazungumza naye kumtuliza kidogo akawa mpole, kuna ndugu yangu huyo aliyekuja kunidhamini wakati nipo ndani kumbe yeye na mwanamke wangu wananisema mpk mambo yakafika home eti mi ni tapeli mwizi nimefungwa aisee ila binadamu bhana 🥺 ila yalipita na nipo imara sn na mwenye nidhamu kubwa mno.
TAENDELEA..
Hapana maybe hukuona hili lilipo anziaMakasiriko ya nini tena?unapitia nyakati ngumu maishani?