Kisa: Nilivyowahi maishani

Kisa: Nilivyowahi maishani

Msoto mi ulianza nimemaliza tu Six, home hakukaliki, huyooo naenda zangu Uhindini mtaa wa Bhojani kuosha magari au kufuta vioo.

Kuna siku sina hili wala lile akapita mwalimu aliyenifundisha Accountancy Mwl Mwasalanga aisee niliona noma kinomanoma.

Mungu ni mwema sahizi naelewa nini maana ya "soto" na nshakuwa dingi.
Hii Mbeya moja
 
NAENDELEA PARTY 16

Turudi sasa kule kwa wazazi
Tulizaliwa watoto watatu mimi nikiwa first born kabisa kisha akafata my young sister kisha dogo wa kiume wa mwisho.
Binafsi nimelelewa na kukulia kwa aunt na moka nahitimu drs la 7 nilikuwa najua ndiye mama yangu na nilimuita hivyo na ilinichukua muda sana mpaka kufuta neno mama kwake na kukubali ni shangazi tu.

Siku moja usku sana alikuja mama yangu mzazi sasa akiwa na huyo mdogo wangu wa mwisho akiwa bado mdogo sana na mimi nilikuwa kama drs la 3 au la 4 hivi mama alikuwa na bibi wametokea dsm wamepita pale kwa aunt skujua kinaendelea nn hapo ila nakumbuka mama alimuacha yule mdogo wangu pale kwa aunt yeye akaondoka kurudi kwao pia bibi alibaki pale maana ndipo alipokuwa akiishi kwa mtoto wake .
Nilikuja kugundua miaka mingi sana imepita kwamba mama sku hiyo ndiyo ilikuwa siku yake ya mwisho kuwa na mumewe yaani baba kwamba walikuwa wameachana na ndiyo alikuwa anarudi kwao sasa rasmi.
Yule mdogo wangu wa kike yeye alikuwa dsm huko kwa mzee. Toka siku hiyo mama skuwahi kumuona tena udogoni sasa, aisee kumbe kuna mambo mazito yaliyokuwa yamejificha kuhusiana na kuachana kwa mzee na mama na waliokuwa nyuma ya hilo jambo ni kina shangazi yaani ndo walipanga mipango mama akiwa kwao kwenda kujifungua huyu mdogo wangu wa mwisho huku nyuma watu wako busy kumtenganisha na mumewe.
Sasa kule dsm mzee alikuwa anaishi pia na mdogo wake ambaye naye ni aunt yangu huyu sasa ndo alikuwa kiungo mshambuliaji kwenye hili sakata akishirikiana na wenzie kuhakikisha mama anaachika.

Moja ya tuhuma nzito ambayo nilikuja kuijua miaka miwili tu imepita toka nimejua hilo inasemekana kwa mujibu wa mama kwamba mzee alikuwa anatembea na huyo mdogo wake ambaye ni aunt na alikuwa analala kwenye chumba cha kaka yake kufua kupika na mambo mengne kama mke kbs lakini lililokuja kunistua yule aunt yangu alitoka dsm akiwa na ujauzito na mpaka tunavyozungumza hapa huyo mtoto wake aisee wanafanana na mzee copyright kbs hata huulizi kitu.
Lakini baba wa mtoto huyo huwa hajulikani specifically ni nani na yuko wp maana hajawahi onekana na huyo ndugu yng mtoto wa aunt ninayemzungumzia hapa anatumia majina ya ukoo huku kwetu.
Sasa ilikuja kupatikana picha halisi baada ya hiyo issue mama kuisanua kwamba mzee anatembea na mdogo wake na kampachika mimba ndipo ma aubt wakaanza harakati za kumtoa kwenye mji wake ili mambo yasiwe mengi sana.
Pale home kulikuwa na binti wa kazi haraka sana akina aunt wakaanza mpigia debe ndiye aolewe na mzee na kweli walipambana yule mdada akaolewa na mzee na mpka leo hii tunavyozungumza hapa ukitaka kosana na ma aunt mguse huyo mke waliyempa mzee nadhan naye anajua nn kilifanyika ndo maana wanamlinda sana uwenda ana siri nyingi kuhusu family.
Mimi niliendelea kuishi kwa aunt mkoani mpaka nilipohitimu drs la 7 kwa mara nyingine tena sasa nipo na aut yangu huyo niliyekuwa namuita mama tulienda kijijini huko msibani na huko kijijini kwetu ndiyo pia kwao na mama.
Tuneshuka kwenye gari kumbe pale tuliposhukia ni jirani na kwao mama, na alikuwa ananipeleka kumsalimia eeeh mi nikiwa nimetangulia aunt akiwa nyuma nikapishaana na mama mmoja hivi mweupe mwembamba alikuwa akija kumpokea aunt akanipta akamfata aunt.
Eeeh kumbe ndiye mama yangu mzazi skumjua wala hakunijua ndiyo kushtuka akarudi kunisalimia na kunipokea alooooo.
Lakini mi wala hata skuwa na issue naye yaani ile Bond haipo kabisa nikasikia wanaongea na aut kwamba baadaye atakuja kunichukua hapo msibani ili nikapaone kwake kimoyo moyo nikasema siendi aisee na kweli alikuja kunichukua na nilikataa.

TAENDELEA
Niwajuze ya mbeleni...ni mazito sana.
 
Wakuu,

Haya maisha acha kabisa sikuwahi fikiri kuna siku nitabeba mzigo kichwani kama kibarua.
Loooh! Nawahurumia sana yatima yaani nilipokosa wazazi nilipata funzo la dunia.

Niliamua kutumia jina halisi JF nakuacha fake ID kwa kukumbuka tu kuwa ni napaswa kufata mambo yangu bila kuudhi mtu.

Nitaleta kisa changu ila big up sana mkuu mimi binafsi nashukuru ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa na mimi kipindi chote. Sina chuki dhidi yao pia walio nikosea nimegundua.

MSAMAHA ni neno dogo ila LINAPONYA
MWENYEZI MUNGU awafanyie wepesi wote mnapitia magumu🙏🏻🙏🏻.
 
Back
Top Bottom