Kisa: Nilivyowahi maishani

Kisa: Nilivyowahi maishani

Choosen85

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,303
Reaction score
5,554
Wakuu hamjambo nyie madogo na wale wakubwa heshima yenu aisee....

Nikiwa nimemaliza degree yangu na matumaini kibao aisee haya maisha haya yamenifanya kuwa na nidhamu sana.
1. Mtiti ulianza home nilikuwa na chumba changu cha nje sjui kilitokea nn mzee one day ananitumia sms kwamba nikiwa natoka basi nikabidhi key kwa mama ( wa kambo ).
Ukweli nilikuwa natoka asubuhi narudi usku si kwamba nilikuwa naenda kuzurula hapana kutafuta hata kazi tu ya kujitolea .

Nilijibu ile sms kwa kumwambia mzee anipe wiki 1 nihame kabisa mi staki maneno maana maisha yashaanza kunichanganya. Hakujibu ila nilifanya hivyo akakatalia kitanda nikawaachia nikasepa zangu kuanza maisha enzi hizo goba bado sn nalala chini kwenye mkeka, asubuhi naamka natembea kwa mguu mpka posta aloooo.
Nilikuwa na demu wangu 1 akabeba mimba uzuri yeye alikuwa ameajiliwa ni mwalimu but naye alikuwa kichomi sana aisee, sasa kazi ikabaki kwangu nilikuwa natoka asubuhi sana home sjui naenda wapi sjui naenda kutafuta nn mfukoni sina hata 200 ya mihogo.

Natembea kwa mguu goba, mbezi luis, to kkoo to posta kisha narudi sina hali na hakuna wa kunionea huruma.

Sjui kula yangu wala kunywa yangu mwanamke hanielewi na wakati mwngne anasepa kaacha mtoto ndani sina hata 100 niliteseka sn, ajabu wenye maduka walikuwa wananiamini sn sjawahi enda dukani kukopa nikakosa lazma wanipe tu wengne nililipa wengne skulipa aloooo.
Kuna wakati nilitembea kwa mguu nikaenda tulia chini ya daraja fulani nkapitiwa usingzi aisee ile nashtuka nakuta nimezungukwa na ma kenge kama 50 hivi sjui ndo yalikuwa yanajipanga kunivamia nilikimbia hata sjui nilikiwa naelekea wapi 😴.

NILIAMUA KUFUNGUA BIASHARA YA KUCHOMA MAHINDI

Ila nyie mahindi yenyewe sjui kuchoma yakawa yanaungua tu mara mi siuzi wenzangu wanamaliza mi siuzi kbs nikaifunga skuwahi pata faida yoyote ile zaidi ya hasara huku namuwazia mwanangu home maana mwanamke haelewi.

Taendelea....
 
NILIAMUA KUFUNGUA BIASHARA YA KUCHOMA MAHINDI
Msoto mi ulianza nimemaliza tu Six, home hakukaliki, huyooo naenda zangu Uhindini mtaa wa Bhojani kuosha magari au kufuta vioo.

Kuna siku sina hili wala lile akapita mwalimu aliyenifundisha Accountancy Mwl Mwasalanga aisee niliona noma kinomanoma.

Mungu ni mwema sahizi naelewa nini maana ya "soto" na nshakuwa dingi.
 
Hizo kazi kama hutitaki unaziona nyingi, ukianza kuzisaka huzipati. Miaka hiyo hapo Dar nilionaga kaz za usafi kwa makampuni nyepesi, na form six yng ilipigwa interview nikakosa. Watu kibao tulikuwepo hadi la saba failures.

Nikapata nafuu baada ya kumpata Lamomy ndo akawa ananihonga hela za kula
Ulikua unazurula tu au uliomba kibarua hata cha kubeba mizigo kkoo
 
NAENDELEA PARTY 2
USIKU MMOJA NAKAMATWA ETI NIMEIBA MEZA YA WATU YA BIASHARA

Usku mmoja nikiwa narudi home nimechoka nina njaa kiu hopeless nikawaza nyumbani kuna viunga vilibaki nikifka nikoroge uji bila sukari ninywe maana najua mwanamke wng atakuwa kapka na hajanibakizia kitu.
Nikapata wazo nikakope vimchele nusu na mafuta hata ya 200 nikifka nipike, kweli nilipata ila sasa moto wa kupikia natoa wp🤔 wakati nipo njian nawaza hapo ni usku wa saa nne, nikapata wazo nitafute vikuni nifke niwashe nipike.
Wakati natembea njian nikaona limeza bovu bovu la mbao lipo njiani aaah saa ngapi nisilibebe ili nipate Kuni nikiwa natembea mdogo mdogo nmekaribia kbs home nashangaa jamaa mmoja mbavu ananisimamisha na kunihoji meza nimetoa wp hiyo ni meza ya BIASHARA ya ndugu yake.
Nikiwa bado najitetea sn kwa huruma labda jamaa anielewe kwamba mi nina shida tu jamaa akasema turudi nilipoitoa.
Na pana umbali nikaongoza njia mpka nilipoitoa akampgia simu mwenye mali aje haraka mwizi wa meza yake kakamatwa jamaa akasema huyo mwizi mlete nyumbani.
Nikabeba tena mmeza mzito tukapga masafa mpka huko kwa huyo mwenye meza aisee akanihoji hoji pale kisha akanambia beba hiyo meza ipeleke sehemu fulani kisha uende zako.🤲 Nikashukuru nikabeba na kuipeleka alikosema nikasepa..
Zangu mchele wenyewe ulidondoka huko njiani wakati nimekatishwa na yule jamaa na skuupata nilifika home mwanamke kalala na hakuna menu nikacheck nikaona ukoko wa ugari uliomwagiwa maji nikachukua nikala tena upo kwenye maji machafu skuwa na namna nikanywa na maji nikalala.


TAENDELEA...
 
Hizo kazi kama hutitaki unaziona nyingi, ukianza kuzisaka huzipati. Miaka hiyo hapo Dar nilionaga kaz za usafi kwa makampuni nyepesi, na form six yng ilipigwa interview nikakosa. Watu kibao tulikuwepo hadi la saba failures.

Nikapata nafuu baada ya kumpata Lamomy ndo akawa ananihonga hela za kula
Na gari pia ya kutembelea nilikuhonga umesahau? 😹😹
 
Back
Top Bottom