Nilivyonusurika kutwangwa risasi na rafiki yangu kisa mchepuko wake

Nilivyonusurika kutwangwa risasi na rafiki yangu kisa mchepuko wake

Wanaume jamani yani mchepuko una nguvu kushinda mke...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nasemaga mm vitu vya bure sio vizuri,ni ushauri tu kijana.
 
Unapopoteza uwezo wa kukitumia kilichomo ndani ya kichwa chako.....ndio mwanzo wa mabalaa maishani mwako......

Mwenyezi Mungu anapokiharamisha kitu si katika kutunyima raha sisi wanadamu la hasha ni kutaka tuishi kwa amani na upendo......

Pombe ni mama wa maasi yote kwa sababu inamfanya mtu apoteze udhibiti wa kichwa chake na kumuondolea aibu....na kujikuta akifanya jambo ambalo baadae analishangaa.....
Hayo uliyoyafanya hapo katika hali ya kawaida yamechangiwa na pombe na pengine umefanya ngono isiyo salama na kujiweka hatarini kupata maradhi.....bila shaka ungekuwa macho makavu na kwa aibu usingefanya jambo hilo......au pengine ungetumia japo kinga kumlinda mkeo....

Vile vile hapo mmewadhalilisha wake zenu na mmedhalilisha ndoa zenu....mmjenga taswira mbaya ya ndoa kwa vijana na mabinti wanaotarajia kuoa au kuolewa.....
Mmefanya ndoa ionekane ni taasisi ya kipumbavu hasa huyo bwege aliyesema kuwa bora ungetembea na mke wake kuliko huyo hawara wake.......
Hii ni ishara kuwa wanaume wenye sifa za kuwa vichwa vya familia wameshaisha au wamebaki wachache sana na ndio maana wanawake wanachukua madaraka yetu......
Ni mwanamke gani atatamani kuwa chini ya mwanamume asiyeweza hata kujiongoza yeye mwenyewe na fikra zake....!!???
Ni mwanamke gani atatamani kuwa chini ya mwanamume asiyetambua majukumu yake kama baba na kichwa cha familia....!!? Muda ambao unatakiwa uwe na familia yako na kushauriana na mkeo kuhusu ustawi wa familia yenu...wewe upo baa na machangudoa unafuja pesa.....!!! Hakika wake zenu wamepata hasara.....
Kama bado unajiona huwezi kuishi na mke na kutunza familia kwanini unaamua kuoa na kumpa jakamoyo mtoto watu mpaka anaonekana mzee kwa mawazo angali kijana....
???...Mnajenga picha gani kwa wanao ikiwa baba ndani ya nyumba unavuma kwa mabaya...!!??...ikiwa baba unaweza ukamaliza miezi watoto hujawatia machoni badala yake unashinda baa na mabaamedi...!!??

Ni vitu vya kipuuzi ambavyo hata wendawazimu muda mwingine huwa wanavishangaa kuwa vinawezaje kufanywa na mtu mwenye akili timamu.....!!!!

Inashangaza na kustaajabisha kuwa ni wapi tunaelekea kama wanajamii ikiwa matukio kama haya baada ya kukemewa badala yake yanaonekana kuwa ni ya kishujaa....!!!??

Ngoja niwakumbushe kuwa daima mchuma janga hula na wa kwao....hayo mnayoyafanya leo na kuyafurahia yakija kuwafika yakuwafika mtawasumbua watu wenu wa karibu...pindi mtakapoanza kutumia malipo ya dhambi zenu.....mtasababisha watu waache kazi zao na kuwavesha nepi na pempasi.....

TIME WILL TELL....
 
Yaani hii story yako inaonyesha jinsi wanaume tusivyojali familia zetu, wote wa3 waliotajwa kwenye hii story wanamiliki michepuko.
 
Rafiki yako anayefanya kazi, anakupigia simu muda wa kazi kwa masuala yasiyohusu kazi; anakuuliza uko wapi, unajibu home, na anauliza kwanini hujaenda kazini..? Anyway...
 
Huyo James sio mzima kichwani yaani anathamini mchepuko kuliko wife? MIMI nikikukuta na mkewangu.................................(R.I.P).
 
Mlimalizanaje Na mkeoo..Maana inawezekana kabisa nacho kikawa kisanga kingine..Na Je Huyo Joy wako alikusimulia kisa cha yeye kumfukuza joy usiku Na kukuita wewe
BAK my Bro .. Upo
 
Huyo James sio mzima kichwani yaani anathamini mchepuko kuliko wife? MIMI nikikukuta na mkewangu.................................(R.I.P).
Ndo maana jamaa akala mchepuko...akijua angekula wife ingekua nongwa...sasa imekua kinyume.
 
Pole sana, nusra jamaako akupasue kichwa kisa mchepuko! So sad
Asingekipasua angekitoboa tuu
Mwanzo niliamua kisa hiki kibakie kuwa siri maishani wangu, lakini kwa sababu jamaa amegoma kunisamehe hadi leo, ngoja tu niwashirikishe.

Jumatatu ya Juni 22,2015.

Niliamka sijisii poa, nikaamua kupiga simu job na kuwaambia niko hovyo sana leo naenda hospital, bosi wa idara yangu akaniruhusu, hata hivyo nikalala hadi saa tano nikaona kama niko fiti hivi. Mara simu yangu ikaita kucheki nikaona James (Sio jina lake halisi) akaniuliza uko wapi, nikamjibu home. Akauliza tena job hujaenda, nikamwambia sijisikii poa. Akasema njoo basi Kimanga mwisho Sunset bar (Tabata) naishi maeneo ya kwa Swai kwa wanaoijua Tabata wanaelewa.

Nikajivuta hadi Sunset Bar, nikamkuta anakula supu ya mbuzi na chapati, mimi supu huwa haipandi hata nikinywa, nikaagiza mtori na ndizi mbili.

Mazungumzo yakaanza:
Yeye (James), "Unajua nini John (sio jina langu) shemeji yako (mke wake) kanikera sana leo tumegombana na nimeshindwa kwenda kazini nimeomba udhuru, hivyo nimekuita ili leo tunywe tu maana nina Kilo tano hapa( Laki tano).

Mimi, "Dah shida ni nini?"
Yeye, "Limimba lake linamsumbua (mke wake alikuwa na mimba kama ya miezi saba hivi), kanitukana usiku kucha kwamba mimi malaya sababu kafuma sms ya mademu zangu wanne, mmoja yule wa Kahama(Namfahamu kitambo tu), nusu nimtie vitasa, sema kwa kuwa na hali yake nimeamua kuondoka na leo sirudi home, tutafute kijiwe tule monde mwanzo mwisho."

Baada ya kumaliza supu akanipa funguo akaniambia endesha wewe gari, tukatoka hadi Buguruni tukaenda Hoteli ya Popex ipo pale jirani na mataa na karibu na Kimboka, tukapiga monde hadi saa moja usiku tukaamua kuhamia Micasa Ubungo.

Tukiwa Micasa akampigia mchepuko wake mmoja anaitwa Joyce (sio jina lake) akasema yupo Ukonga Banana, akamwambia achukue pikipiki hadi Ubungo na kweli baada ya kama dakika 50 hivi Joyce awasili Micasa.

Tukanywa pale hadi saa tano usiku, ghafla James akaanza kutupiana maneno makali na Joyce mimi ikanibidi niwe msuruhishi wao, wakatulia na tukaamua kuhamia Kinyaia bar pale Landmark hotel (siku hizi hostel).

Kwa mujibu wa makubaliano yao ni kwamba, yeye James na Joyce walale lodge ipo jirani na bar ya Kinyaiya na wakalipa kabisa tulikubaliana mimi niondoke na gari wao niwaache pale yeye asubuhi atachukua boda.

Wakazama room mi nikawaacha, hiyo ni saa sita usiku mimi nikaamua nirudi Micasa nichukue kiepe maana wife aliniagiza nimbebee kwakuwa tuko wawili watoto walikuwa na bibi yao hatapika.

Nafika maeneo ya taa za External, James ananipigia simu, anataka nirudi pale lodge ya Kinyaia nifanye haraka, nikarudi namkuta kasimama nje na Joyce huku kila mmoja kakasirika. Nikawauliza kulikoni, akaniambia nirudishe home na huyu malaya (Joyce) mpeleke kwake Kurasini. Nimwambia kaka siwezi usiku huu mimi narudi zangu home.

Wakaiingia kwenye gari tukapita njia ya jeshini kwenda Tabata nikamfikisha home kwake akasema wewe kapaki na gari na mtafutie logde huyo malaya (joyce) alale, funguo niache kwa mlinzi tunapolaza magari( tunalaza sehemu moja magari yetu).

Mi nikamwambia si pale Kinyaia mmeshalipa kwanini tulipe nyingine? Akanijibu fanya unavyojua (James ni mkubwa kwangu kiumri kwa miaka mitano, so huwa ananifanya kama mdogo wake), akatoa buku 30 akampa Joyce.

Mi nikawasha gari hadi Ngujini iko jirani na Mazda kwa wanaoijua Tabata, nikamwambia kacheki room hapo ulale, Joyce akasema twende tukaangalie wote, mi nikashuka tukakuta kipo cha 25, akalipa, lakini akakataa kulala peke yake.

Mimi wala sikujivunga, nikaingiza gari getini nikazima simu tukalala (nilimtafuna usiku kucha)

Sasa kumbe kuna rafiki yetu mmoja nae alilala pale Ngujini na mcheuko na akaliona gari ya James pale asubuhi, akampigia simu kumjuliza kama amelala pale, James akajibu hapana na wakati huo kumbe James amekwenda tunapolaza magari kuchukua funguo akakuta hola. Akalikuta gari langu tu.

Jamaa alivyo na sifa akasubiri kuona nani ataondoka na gari, akalipaki kwa chini kidogo kuna sehemu ya kuchota maji akawa kama analiosha, na mimi na Joyce tukatoka ni (saa mbili hiyo), akajificha akampigia simu James mimi bila kujua, (kumbuka huyu jamaa yeye huyu mchepuko naoanaujua kama ni wa James).

Dakika 10 naona James kaja na boda boda kafura vibaya, kufika tu akaniambia nipe funguo, nikampa, akamgeukia Joyce na kumwabia wewe malaya nini umekosa kwangu? Joyce hakujibu kitu, mara yule jamaa akatukaribia.

Bila kutarajia James akachomoa bastola yake, akaniambia hivi: "John ni afadhali ungemtomba mke wangu kulikoa huyo Joyce, kwa kweli siwezi kukusamehe, nakutia risasi ya kichwa mimi naenda segerea. Yule jama akamuwahia James na kushika mkono wenye bastola, huku watu wameanza kujaa.

Nilisikia kizunguzungu baada ya kumuona wife naye huyu, nikajua jamaa yule kashamwaga mboga na ugali.

Mimi na wife tuliyamaliza.

Lakini hadi ninavyoandika hapa, James amekataa katakata kunisamehe, anasisitiza afadhai ningelaa na wife wake angenisamehe, lakini sio Joyce na bado kwa sasa wapo pamoja tena.

Kifupi ushikaji wetu wa miaka zaidi ya 17 umekufa rasmi na mimi naendelea na maisha yangu kama kawaida.

Juzi nimemkuta sehemu tunapolaza magari aliponiona tu aligeuka haraka na kuondoka hata hakuandika kwenye daftari. Nikasema Poa tu na yule jamaa mnoko tulipaki wote gari pale The Great bar mpya jirani na Baracuda, akaenda kulitoa na kwenda kupaki sehemu nyingine.

Leo nimeamua tu kushare nanyi jinsi penzi linavyweza kumaliza kabisa urafiki wenu.

Ukimwi wanaume ndio tunaoupeleka nyumbani.
 
Angekuua tu mijitu tamaa na hicho kiepe ulipeleka kwa mkeo?
 
Unapopoteza uwezo wa kukitumia kilichomo ndani ya kichwa chako.....ndio mwanzo wa mabalaa maishani mwako......

Mwenyezi Mungu anapokiharamisha kitu si katika kutunyima raha sisi wanadamu la hasha ni kutaka tuishi kwa amani na upendo......

Pombe ni mama wa maasi yote kwa sababu inamfanya mtu apoteze udhibiti wa kichwa chake na kumuondolea aibu....na kujikuta akifanya jambo ambalo baadae analishangaa.....
Hayo uliyoyafanya hapo katika hali ya kawaida yamechangiwa na pombe na pengine umefanya ngono isiyo salama na kujiweka hatarini kupata maradhi.....bila shaka ungekuwa macho makavu na kwa aibu usingefanya jambo hilo......au pengine ungetumia japo kinga kumlinda mkeo....

Vile vile hapo mmewadhalilisha wake zenu na mmedhalilisha ndoa zenu....mmjenga taswira mbaya ya ndoa kwa vijana na mabinti wanaotarajia kuoa au kuolewa.....
Mmefanya ndoa ionekane ni taasisi ya kipumbavu hasa huyo bwege aliyesema kuwa bora ungetembea na mke wake kuliko huyo hawara wake.......
Hii ni ishara kuwa wanaume wenye sifa za kuwa vichwa vya familia wameshaisha au wamebaki wachache sana na ndio maana wanawake wanachukua madaraka yetu......
Ni mwanamke gani atatamani kuwa chini ya mwanamume asiyeweza hata kujiongoza yeye mwenyewe na fikra zake....!!???
Ni mwanamke gani atatamani kuwa chini ya mwanamume asiyetambua majukumu yake kama baba na kichwa cha familia....!!? Muda ambao unatakiwa uwe na familia yako na kushauriana na mkeo kuhusu ustawi wa familia yenu...wewe upo baa na machangudoa unafuja pesa.....!!! Hakika wake zenu wamepata hasara.....
Kama bado unajiona huwezi kuishi na mke na kutunza familia kwanini unaamua kuoa na kumpa jakamoyo mtoto watu mpaka anaonekana mzee kwa mawazo angali kijana....
???...Mnajenga picha gani kwa wanao ikiwa baba ndani ya nyumba unavuma kwa mabaya...!!??...ikiwa baba unaweza ukamaliza miezi watoto hujawatia machoni badala yake unashinda baa na mabaamedi...!!??

Ni vitu vya kipuuzi ambavyo hata wendawazimu muda mwingine huwa wanavishangaa kuwa vinawezaje kufanywa na mtu mwenye akili timamu.....!!!!

Inashangaza na kustaajabisha kuwa ni wapi tunaelekea kama wanajamii ikiwa matukio kama haya baada ya kukemewa badala yake yanaonekana kuwa ni ya kishujaa....!!!??

Ngoja niwakumbushe kuwa daima mchuma janga hula na wa kwao....hayo mnayoyafanya leo na kuyafurahia yakija kuwafika yakuwafika mtawasumbua watu wenu wa karibu...pindi mtakapoanza kutumia malipo ya dhambi zenu.....mtasababisha watu waache kazi zao na kuwavesha nepi na pempasi.....

TIME WILL TELL....
Madini haya! Shukrani mkuu!
 
🙂 kweli mwizi akiibiwa analia machozi halisi siyo bandia. na shukuru aliwakuta nje, ungekuwa ndani eeeeh asingetoa bastola ya mzungu angetoa ya mniggah unepoteza utu wako.
 
Blaza ulisalit masela ila James ana roho ngumu dadek et bora ungelala na mkewe kuliko mchepuko
 
Back
Top Bottom