Baada ya simu yangu ya tecno kuharibika sikuona haja ya kupoteza hela kuipeleka kwa fundi kwa sababu nilikuwa nimeitumia kwa miaka mitatu hivyo nikaona ni bora tu nikatafute simu nyingine mpya ya kutumia. Tarehe 2/2 nikaamua kwenda town kununua simu ila niliplan safari hii ninunue Samsung maana sikuwahi kuitumia kabla. Nilipofika town nikaenda kwenye duka moja la simu nikaulizia bei ya Samsung nikaambiwa 680,000 ila hela yangu ikawa haitoshi ndipo jamaa ambaye ni muuzaji akanishawishi kama vp kuna Samsung pia za mkopo hivyo kama sitojali naweza tu kuchukua halafu niwe nalipa kidogokidogo. Basi mi sikujali kwa sababu aliniambia kianzio cha mkopo ni 80,000 halafu hiyo iliyobakia nitakuwa nailipa mdogo mdogo hadi mda wa mkopo wangu utakapoisha. Akanipa Samsung Ao5 nikalipa kianzio halafu akanipa namba ya kampuni ambayo nitakuwa nalipia hela iliyobakia, kama ni kwa wiki, siku au mwezi. Kwa siku2260 au kwa wiki 15821. Sasa kitu ambacho mimi sikukigundua wala kuuliza ni kiasi cha riba kwenye hizi simu za mkopo kwa sababu wiki mbili baadae jamaangu mmoja nae alienda kununua simu kama hii ya kwangu lakini yeye haikuwa ya mkopo alilipa cash. Sasa kitu kilichonishtua ni bei jamaangu aliyonunulia, yeye aliuziwa 240’000 na mimi niliambiwa ni 411’000 nilipe kidogokidogo kwa miezi 6. Kilichonishtua ni bei halisi ya simu kwa cash na mkopo. Yaani 240’000 cash na mkopo 411’000 ikiwa ni ongezeko la 170’000 yaani riba ya mkopo ni robo tatu ya bei ya simu. Duh kweli vitu vya mkopo kwangu basi nilinasa kwenye mtego na sitorudia tena hakika huu ni wizi na utapeli wa waziwazi.