Niliugua kifua kikuu(TB)

Habarini za mida wapendwa katika Bwana

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu kuwa mimi niliugua kifua kikuu mwaka 2012

Nilianza kutumia dawa ya kifua kikuu ndani ya mienzi miwili ya awali ambayo kila siku nilikuwa nameza vidonge vinne(4)

Niliendelea na hiyo dozi kwa kuzingatia masharti yake vizuri tu mpaka nikawa nimerudi kwenye khali yangu kama zamani ndani ya hiyo miezi miwili.

Dozi yake niliandikiwa nitumie ndani ya miezi sita na kati ya hiyo miezi sita nilitumiwa dawa miezi mitatu tu nikaacha dawa yaani miezi miwii ya awali na mwezi mmoja tu

Niliacha kutumia hizo dawa kwa sababu nilijiamisha kuwa nimepona japo nilijua kabisa kuwa dozi inatakiwa tumie miezi sita

Kifua kikuu changu hakikuwa kile cha kukohoa kikohozi kikavu hapana nilikuwa nakohoa tu kawaida na makohozi yalikuwa hayatoki kama ilivyo kawaida kwa wagonjwa wengine wa kifua kikuu(TB)

Sasa Basi wapendwa wana Jamiiforums hasa hili jukwaa la Doctor

Nilikuwa nauliza kuwa naweza kuugua/kujirudia tena kuugua kifua kikuu kwa kusitisha/kutokumaliza dozi?

Ikumbukwe kuwa ni miaka minne(4) sasa imepita tangu niugue huo ugonjwa wa kifua kikuu na sijaona dalili zozote zile za kujirudia kuugua tena.

Yaani nipo kama sikuuguaga tu vile

SIYO KILA ANAYEUGUA KIFUA KIKUU(TB) ANA UKIMWI NA SIYO KILA ANAYEUGUA UKIMWI ANA KIFUA KIKUU JAPO HAYA MAGONJWA YANA UKARIBU SANA.

AKHSANTENI

Akhsante sana mkuu mtakavyote

Ki ukweli nakubaliaba na wewe kuwa ukitumia dawa ndani ya hiyo miezi miwili ya awali anasaidia sana

Mimi nilizingatia sana na kufata masharti yote ambayo nilipewa wakati nataka kumeza dawa.

Sasa mkuu mtakavyote nifanye nini ili nisirudie kuugua ugonjwa huu?

Sababu kuu zilizopelekea mimi nikaacha kumaliza dozi ni kuhama sehemu ambayo nilikuwa nachukulia dawa pindi nimeanza dozi.

Ipi ni sababu sahihi?
 
Ipi ni sababu sahihi?
Sababu kuu iliyopelekea nikaacha dawa ni maeneo niliyokuwa nachukulia dawa nikahama mkuu Ze Heby.

Nilijiaminisha kuwa nimepona kwa sababu afya yangu ilirudi kama zamani

Kwa hiyo pindi nimehama sikutaka kuendelea na dawa japo nilijua kabisa kuwa ni kosa ndo maana nimeuliza.
 
Kwa kuongezea swali, uliacha kutumia dawa miaka 4 iliyopita, nn leo kimekufanya uhofie? Kuna dalili zozote za kuugua?
Sijahisi dalili zozote zile kuwa naweza kuugua tena TB mkuu Jozzy

Afya yangu ipo kama zamani tu kabla sijaugua huo ugonjwa.
 
Sijahisi dalili zozote zile kuwa naweza kuugua tena TB mkuu Jozzy

Afya yangu ipo kama zamani tu kabla sijaugua huo ugonjwa.
Basi kuna mawili, la kwanza pengine umepona kabisa, la pili wadudu wa TB (Mycobacterium tuberculosis) wamekuwa weaken na dawa ulinzi wa mwili ukawaweza na hivyo wakawa kwenye latent form, endapo immunity itashuka kwa sababu yoyote ile TB inaweza kuonekana. Ushauri wangu usiwe unakatisha dozi, kwa sababu ugonjwa unaweza kukurudia, pia unasababisha dawa hizi zizoeleke kwa wadudu (drug resistance - wadudu wa TB wana uwezo wa kupasiana genes zinazotoa ulinzi dhidi ya dawa fulani) kiasi kwamba miaka ya baadae hazitafaa kwa matibabu
 
Akhsante sana kwa ushauri wako mzuri mkuu Jozzy.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom