Nilitegemea kuona kampeni ya wachezaji wa Simba sc kuwaomba msamaha mashabiki wao, baada ya kudondosha point mbili muhimu dhidi ya KMC.

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,305
12,802
Ndiyoo!! Msemaji wa Simba sc (Ahmedy Ally) alianzisha Jambo la kiungwana la kuombana msamaha haswa mnapokoseana.

Hii kampeni ilianza baada ya Simba sc kuchukua point tatu muhimu Mbele ya Wydad Casablanca huku mfungaji akiwa Onana, na kipa Ayub alionekana kufanya vizuri tokea wakiwa kwenye uwanja wa Wydad Casablanca.

Kampeni iliendeshwa na Ahmedy Ally akiwataka mashabiki wa Simba sc wawaombe msamaha wachezaji haswa Onana na Ayub maana wao ndiyo walikua wakishambuliwa sana na mashabiki kuwa hawana kiwango.

NALIA NGWENA nilitegemea kuona hii kampeni itaendelea hata kwa mashabiki kuombwa msamaha endapo timu itapoteza mchezo Kama ilivyotokea kwa kudroo na KMC na kusababisha Simba sc kudondosha point mbili muhimu lakini imekua tofauti kabisa nilichokuwa nakiwaza kichwani mwangu.

Maoni Yangu : msemaji wa Simba sc Ahmedy Ally aendelee na Kampeni yake Tena Safari hii wachezaji wawaombe msamaha mashabiki kwa kucheza chini ya kiwango na kuwapotezea matumaini mashabiki Nia ya kuinua kwapa (kuchukua kombe) la NBCPL.

Nawasilisha hoja.
 
Back
Top Bottom