Nilitamani kuyajua haya - Ajira kwenye Mradi wa Bwawa la Umeme ( Part Two)

jouneGwalu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,687
1,780
Baada ya HR kusema hayo alitutoa nje ya ofisi yake,

Hapo nikajiuliza kitu.

Hivi yule "Dada Kulwa" alivyokuwa ananiambia kuwa amefunga kutoa vibali siku ile nilipofika na mimi kumkubalia hiyo kesho yake ningewezaje kuwahi hii interview?

Pia nilichokiona mpaka hapo ni kuwa HR wa hii kampuni ya waarabu sio watu wenye weledi sana sababu jinsi wanavyopeleka zoezi zima la ajira ni kama mzaha na hawapo serious kabisa na ajira wanazotoa. Ni kama vile wanafanya "unataka njoo hutaki acha"

Kuna kingine kuhusu mazingira ya ndani ya mradi humo,
Kama nilivyoeleza awali huu mradi unatekelezwa katikati ya pori la Selous,
Hii inafanya mazingira mengi ya mradi huu kuwa tofauti kidogo mfano ndani ya mradi sio ruhusa kutembea kwa miguu kutoka umbali fulani.
Ndio maana kama mmeona hapo awali nilisema kutoka pale kwenye geti kuu tulifuatwa na Pick Up
Na umbali kutoka geti kuu mpaka ofisi za HR inaweza kuwa kama KM 3 na nusu au chini ya hapo kidogo
Na hilo eneo la geti kuu limezoeleka kwa jina la "Belmontè". Na hilo eneo la ofisi za HR (of course na ofisi zingine zipo hapo) linafahamika kama Kariakoo.

Haya sasa tuendelee na mkasa wetu;

Baada ya HR kutupa referral tena kwa "Dada Kulwa" yeye alirudi zake ofisini, tukatoka mpaka eneo la kusubiri usafiri.
Awamu hii ikawa tofauti sasa, awali wakati tunakuja tulifuatwa na gari kutoka kule geti kuu (Belmontè) ila muda huu hamna wa kukutafutia gari na vilevile hurusiwi kutembea kwa umbali huo. Sasa gari utapata wapi? Hiyo ni juu yako!!

Muda ukiwa umesogea sana ikielekea saa kumi na mbili kuna Lorry Truck ilikuwa inaelekea pale Belmont, ikatuchukua. Tulikuwa wengi mda huo zaidi ya 15 kwa makadirio.
Tukafika tena getini pale Belmont, ukaguzi ukafanyika tena.
Ukaguzi wao jamaa wanatoa kila kitu kwenye begi lako, wanachambua halafu utapanga tena.
Walipomalizana na mimi nilienda upande wa pili kusubiri gari la kunirudisha Kisaki.
Kumbuka hapo gari ni za kubahatisha sasa yaani ni kuvizia gari inayorudi Kisaki uombe lift.
Ilikuja pick up, na jamaa akaeleza msimamo malipo ni Elfu 5. Mpaka hapo nilikuwa nimechoka sana wazo lilikuwa nifike Kisaki kwa gharama yoyote nitafute chakula nilale. Hata majibu sikuwa na hamu nayo. Tuligombania ile nafasi ya kwenye gari japo nipate kupanda ndani kwenye viti ili nisipate yale mateso ya kuwa nyuma ya pick up,
Kulikuwa kuna watu wana mbavu nene sana nikakosa nafasi ya mbele, nikaona isiwe tabu bana kikubwa kufika Kisaki.

Safari ikaanza,
Tofauti na asubuhi wakati wa kuja, mda huu kulikuwa na vumbi kali sana na tulikuwa tunapishana na trucks nyingi zinazoleta materials mbalimbali kwenye mradi. Tuliokuwa huku nyuma ya pick up tulikoga vumbi bana ... asikwambie mtu!

Kwenye mida ya saa mbili hivi, nilikuwa nipo mbele ya Dada Kulwa nikijieleza tena.
Akaniangaliaaaa,
Akatafuta jina langu kwenye vibali vyake hakuliona, akaniambia "aah nyie ndio wa kishua mnajifanya hampiti hapa eeh"
Kwakweli sikuwa na nguvu ya kujibishana naye kwa chochote, nikamwambia nipatie majibu yangu niondoke hapa Kisaki.
"Unakata tamaa mapema hivyo, haya umepata kazi nenda stationary kachukue form za kujiunga" maelezo ya Dada Kulwa hayo,

Ilikuwa kama kishayaona machungu na hasira za mzunguko wote wa siku hiyo,
Taarifa yake hiyo wala sikuifurahia kivile ila nilijikuta tu natamka maneno ya kumshukuru Mungu,
Pia nilimshukuru kwa kunipa majibu. Akaniambia nikijaza hizo form baada ya siku 2 nirudi pale ili azikague na kunipatia kibali, tena alisisitiza mda huu nisijifanye mjanja

Form zao za kujiunga zinataka vitu vingi mnooo.
︎Passport size zaidi ya 14,
︎Wadhamini 3
︎Barua za serikali ya mtaa
︎Report ya alama za vidole
︎Form ya uthibitisho wa afya toka hospital ya wilaya, mkoa au rufaa
︎Barua za utambulisho toka kwa mwajiri wako au certificate of service

Na vikolombwezo vingine chungumzima!

Basi sababu Moro nina wadau wengi, ikabidi asubuhi ya siku iliyofuata niamshe Moro kukamilisha yote hayo!

Mpaka hapo sijui mshahara watanipa kiasi gani na hilo kwakweli ndio lilikuwa linanipa mawazo. Maana baada ya kuangalia mazingira yale nilisema kitu pekee cha kunikalisha huku ni mshahara wa kueleweka. Na bahati mbaya kabisa mpaka kufikia hapo wala sikuwa na mtu japo wa kuuliza. Kwenye interview walisema masuala ya mshahara utamalizana na HR.

Nilikamilisha documents zao kama wanavyotaka na nilipoona wamesisitiza documents toka mwajiri wako wa awali ilinipa matumaini.
Pia kwenye form zao kuna sehemu walitaka kuainisha mishahara uliyolipwa kwenye kila experience uliyopitia. Hili nalo lilinitia moyo mnooo

Japo bado niliendelea kuwa na moyo mzito ila nilikuwa najilazimisha sana kuwa itakuwa sawa tu.

Awamu hii nilivyorudi sasa Kisaki kidogo wenge lilikuwa limepoa,
Macho yangu yalikuwa yametulia kiasi nikaanza kuiangalia vizuri Kisaki.
Ni eneo ambalo kwa kiasi kikubwa limechangamshwa na mradi huu,

Ndio, japo Kisaki ni kituo kikongwe cha Train ya TAZARA ila effect ya TAZARA sio kubwa kama ya mradi wa Bwawa la Umeme. Usiku wa siku hii ndio nilijua kuwa kuna namba kubwa ya vijana wapo pale Kisaki kwaajili ya "Kusotea" vibarua vya kwenye mradi.

Kusotea ndio msamiati maarufu pale kisaki,
Kiasi kuna vijana wapo pale Kisaki zaidi ya mwezi,
Wanalala nje au kujibanza kwenye kuta za nyumba au maduka ya watu ili tu kupitisha usiku, na asubuhi anaamkia kwa "Dada Kulwa" kuangalia limebandikwa tangazo la nafasi gani ili aombe.

Hivyo ofisi ya "Dada Kulwa" pale ni kwaajili ya kuratibu zile nafasi ambazo ni kwaajili ya wakaazi wa eneo husika ili kukidhi ile tunasema "CSR" ya mradi kwamba "jamii iliyozunguka mradi inanufaika"

Ila bahati mbaya utekelezaji wake umekuwa tofauti sababu sasa imekuwa "ajira zote" za mradi lazima upitie hapo Kisaki na wakati mwingine inaongeza usumbufu sana.

Na hii tutaona huko mbele madhara yake kwa watu wanaomba kazi bila kuzingatia utaratibu huu wa "Kusotea"

Hivyo "Dada Kulwa" anaona wote wanaoenda kwake pale ni wasoteaji tu
Ndio maana yupo kama alivyo!
 
Ccm mbere kwa mbere
 
Back
Top Bottom