Nilitamani kuyajua haya - Ajira Mradi wa Bwawa la Umeme la Nyerere (Part - III)

jouneGwalu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,687
1,780
Siku ya Jumapili, ofisi ya Kisaki (Kwa Dada Kulwa) huwa inafunguliwa jioni na hasa ni kwaajili ya kutoa vibali vya wanaoingia jumatatu. Hivyo ilipofika mida ya saa kumi na mbili kasoro ya jioni nilifika pale na bahati nzuri sana Dada Kulwa hakuwepo.
Alikuwepo msaidizi wake kijana mmoja, nilimkabidhi makabrasha yangu na baada ya ukaguzi wake aliandika jina langu kwenye orodha yake, tukaagana kwa kuniagiza kesho mapema sana mida ya saa tisa usiku ndio usafiri unatoka Kisaki.

Mapema sana usiku wa saa 9 kasoro nilikuwa stand Bar ya ghorofa nikisubiri kuingia kwenye gari,
Siku hii nilibahatisha Coaster bana.
Yeah ni Coaster za mradi zinachukua na kurudisha watu. Zina ratiba ya kuja Kisaki na kurudi kwenye mradi. Kuingia kwenye gari ni lazima dereva na msaidizi wake wajiridhishe vitambulisho kwa wafanyakazi au vibali kwa watu wa test. Nilipata siti,
Safari ikaanza.
Hizi Coaster unalipia 5,000 kama wewe sio mtu wa testi.
Kwamba kwenye abiria tunaokuwemo humo kuna wale wanaoenda kuripoti kazini kama mimi, Kuna wafanyakazi wa mradi waliotoka kwa mtindo wa "iende irudi" (tutaelewa mbele kidogo) na kuna watu wa testi.
Hayo makundi yote yanalipa 5,000 isipokuwa watu wa testi tu. Mimi kwenye kuingia dereva na konda wake walinitambua kama mtu wa testi, so 5,000 yangu ilipona.
Tulifika Belmont mida ya saa 11 kasoro hivi,
Kama kawaida tulikuwa wengi kiasi na tulikaa hapo mpaka mida ya saa 5 asubuhi ndio tuliitwa majina.
Mpaka sasa sijaweza kuelewa mantiki ya kuondoka Kisaki saa 9 usiku na kufika hapa saa 11 alfajiri na kuachwa hapo getini mpakaa 5 asubuhi.
Sijui lakini ila sio utaratibu wa kistaarabu kabisa.
Na kama kawaida kuna watu hawakupita kwa Dada Kulwa tuliwaacha pale

Mida ya saa 5 asubuhi Coaster nyingine ilikuja kutuchukua pale Belmont na kuanza kutusambaza kwa kadiri ya maeneo tunayoenda. Sisi tunaoenda kuripoti tukaachwa Kariakoo kwa HR,
Baada ya HR kuchukua makabrasha ya kila mmoja wetu pale, tulitakiwa kukaa nje mpaka atakapoitwa mmoja mmoja.
Tokea hatua hiyo kuna wenzetu makabrasha yao yalionekana hayajakamilika hivyo walitakiwa kurudi walipotoka kwenda kukamilisha.
Hili ndio tatizo nililisema kule juu kuwa HR ya hawa jamaa ni makatili na hawana kabisa ile hali ya kujali na kuheshimu utu.
Tuliokuwa tumekamilisha tulielekezwa kwenda ofisi moja ya "Adminis", hapo tulikaa kusubiri mikataba! Ni utaratibu wa tofauti sana.
Jina langu liliitwa nikapewa mkataba wangu, hapo ndio hali yangu ilibadilika. Nilijisikia tumbo la kukata, koo lilikauka ghafla, hasira na kutetemeka hata kusaini nikawa siwezi. Kiasi kilichoandikwa kama malipo yangu halisi baada ya makato yote niliyaona ni madogo sana, kiasi nikajiuliza kuwa labda sikulielewa tangazo.
Nikamfuata yule Admin na kumuuliza hivi hii post mlikuwa mnataka mtu wa namna gani? Yule binti alinitazama akasema, kama hujaridhika na mshahara basi acha tu.
Sio kwamba labda dharau,
Ila nilitafakari mlolongo wote, pamoja na kuainisha uzoefu wangu na barua za mapendekezo toka kwa waajiri wangu wa awali na viwango vya mshahara, hawa jamaa walinipa offer ya 450,000. Hiyo hela hata ajira yangu ya kwanza zaidi ya miaka 10 iliyopita sikuwahi kulipwa. Baadae nikajirudi sawa na nilikuwa nishafanya maamuzi yangu. Nilisaini yale makaratasi yao na nikasema sitauliza swali lolote hawa watu!
Tulielekezwa ofisi ya HSE kwaajili ya induction.
Pamoja na maelezo mengi juu ya mradi ila msisitizo ni kwenye mambo ya usalama,
Ambapo nilielewa kuwa unapokuwa humo kwenye mradi, mawazo yako yawe kazini tu.
︎Hairuhusiwi kunywa bia siku za kawaida (jtatu hadi jumamosi)
︎Hairuhusiwi kuwa na mahusiano ya kingono na mwanamke

Hii ni kwa kuzingatia kuwa nature ya mradi ulipo.
Walipomaliza watu wa HSE walikuja watu wa sheria toka ofisi ya HR,
Kikubwa walisisitiza kuhusu utaratibu wa likizo. Utaratibu wa likizo kule ni kuwa kwenye miezi 6 unaenda likizo ya wiki 2.
Hilo ndio eneo nilipata vichomi tena sasa.
Yaani nakaa miezi 6 bila kuonana na wife na bia kunywa kwa masharti halafu likizo ni wiki 2 tu.
Kingine ambacho jamaa wa HR alitumia mda mwingi kukielezea ilikuwa eneo la "overtime"
Kwamba kwa maelezo yake ni kuwa hata wao wanafahamu kuwa mishahara wanayotoa ni kiduchu,
Hivyo wameweka aina ya mfumo ambapo mtu atatumia mda mwingi kazini na hatimaye kutengeneza masaa mengi ya ziada ili mwisho wa mwezi iingie hela inayoeleweka. Hivyo hesabu ya overtime ni miongoni mwa hesabu ya msingi sana kwa wafanyakazi wa kwenye mradi huu. Japo kuwa masaa ya kawaida ya kazi yanaanza saa 2 asubuhi mpaka saa 11 jioni,
Ila utaratibu umewekwa pale kazi mnaingia saa 1 asubuhi mpaka saa 1 usiku kwa siku za jumatatu mpaka jumapili.
Na jumapili na siku za sikukuu ndio siku zenye rate ya juu zaidi.
Baada ya hizo presentations mida ilikuwa imeenda karibia mida ya lunch,
Tulielekezwa njia ya kupita kwenda kula.
Mimi wakati huu wote nilikuwa nishavurugwa kabisa, sikuwa na furaha kabisa. Na kiasi fulani niliona ile hofu iliyokuwa inanizunguka toka mwanzo kuwa ilikuwa sahihi.

Eneo la Canteen kwa hapa Kariakoo ya huku kwa jamaa zetu lipo karibu na ofisi za HR,
Unapita msikiti (wa kariakoo) kwa mbele kidogo.
Kampuni inayotoa huduma za chakula humu kwenye mradi ni "AKO Catering".
Foleni ya kuchukua msosi ilikuwa ndefu sana, jamaa wenyeji wakasema hii ndio Canteen yenye kutoa msosi mzuri kidogo ukilinganisha na zingine.
Kweli tulikuta menu ya kuvutia japo kwa mtu mwenye uzoefu na huyu Caterer hatukua na cha kushtuka sana.
Siku hii kulikuwa na pilau/wali mweupe, nyama yenye mchuzi mzito na unanukia vizuri sana, kulikuwa na kachumbali, kipande cha tikiti maji na juice fulani yenye asili ya zile juice za ku dilute na maji (cola) ila ilikuwa tamu.

Mpaka hapo utaratibu wa makazi tulikuwa bado hatujapewa, na ilielezwa huo utaratibu huwa ni wa mwisho kabisa mpaka mkipewa vitambulisho.
Hivyo baada ya zoezi la kula tulielekea ofisi ya "Security" hapo ndio wanatoa vitambulisho vya getini. Utaratibu pale, kila mtu unatakiwa kuwa na vitambulisho 2.
Kimoja ni kitambulisho cha HR, hichi ni kwaajilli ya "ku-punch" kwenye POS za maeneo ya kazi ili kuonyesha kuwa umeingia kazini na au umetoka.
Hivyo masaa yako ya kazi HR wanapima kwa kuangalia kwenye system zao kama zinavyokuwa picked toka kwenye POS zao.
Kitambulisho cha pili ni cha "security", hichi ni kwaajili ya watu wa usalama. Tofauti yake na kile cha HR, hichi kina picha yako!
Zoezi la kupata hivi vitambulisho lilichukua mda mrefu sana.
Hadi mida ya saa 11 jioni havikuwa tayari.
Wakati tunashangaa pale jamaa tu mwenyeji pale akasema hapa kama hammjapata vitambulisho basi mtalala "Radwa".
Kama kawaida hamna mtu yeyote aliyejitokeza kutoa muongozo kuwa mtafikia wapi kwa leo na vitu kama hivyo!!

Basi jioni hiyo tukaelekea huko Radwa,
Uzuri wake hapo Radwa ni hapohapo Kariakoo, ni mwendo wa kutembea tu.
Inaelezwa hiyo Radwa ni kambi ya awali kabisa ilijengwa na wakandarasi waliokuwa wanajenga majengo ya hapo Kariakoo. Hivyo ilikuwa kabisa kwaajili ya mafundi na madereva na wahudumu wengine waliotumika kwa mda huo.
Mabweni yake yamejengwa kwa mabati tupu yaani kuta zake ni bati na kuezeka juu ni bati ile tunaita "full suti"
Na sifa kubwa ya pale Radwa ni chawa
Kwa masimulizi tulisikia kuwa "Kuna chawa balaa"
 
Apo kwenye chawa ......!
 
Mchina unampelekea vyet hahahahha acha upumbavu Sasa na tuvyet vyako ole wako ukose ujuz nakuapia utaenda kupamba kwenye kabati la nguo kwenu!
 
Wanaajiri wabongo tu japo mradi ni watu wa china
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom