Nilitamani kulia kisa mchango wa harusi

cold water

Senior Member
Oct 6, 2021
175
618
Mar pap jirani kaja nyumbani, kapiga hodi nilikuwa nimelala nimechoka na kazi. kapiga piga hodi na kelele nyingi za kuniita niamke, nikaamka kumsikiliza alafu nilikuwa nimechoka sana na night, akanambia habari nikamwambia salama shikamoo kaanza kunisema sema kwanza kisa nimemwaga majivu ovyo wakati huo eneo sio lake ni la kwetu, akidai nachafua mazimgira eneno hilo litatumika kwenye sherehe ya mwanae ivyo nizoe majivu yote niliyomwaga mwaga nikatupe shimoni.

Nikamwambia sawa nitafanya ivyo baada ya kunisema akaniambia nakukaribisha badae nyumbani SAA kumi jioni kwenye kikao, mwanangu anafunga ndoa ivyo karibu tujadiliane hautakwepo pekeako watu wengi watafika kumbuka ni siku ile ile alonisema kuhusu majivu.

Nikamwambia sawa ni mama mtu mzima na ni staff mwezangu kazini japo mimi ni mgeni tu ata miezi sita sina nikamwambia sawa, imefika ile SAA kumi nikaenda nisijue kama kikao kinawahusu wana kamati, kumbe kikao chenyewe ni kuwa mwanakamati,kwaiyo ikaonekana nimeudhulia kile kikao na nimekuwa mwanakamati kama kilazima fulani ivi,Though kwa uzoefu wangu najua ivi mtu anakufata anakuomba naomba uwe mwana kamati,mana kama tunavyofahamu ukiwa mwanakamati mchango unakuwa mkubwa kuliko waudhuliaji wengine,mana kamati kazi yake kuiendesha sherehe. Basi jamani kwenye kikao ikapigwa idadi pale pale ya watu tulohudhulia siku ile wakagawanya kwa badgeti ambayo imepigwa , dah kimoyomoyo nikajisonya sana,alafu mambo yenyewe kafanya ghafla tumeambiwa mwezi ulopita july mwishoni mchango mwisho tareh 14 August.

Mimi sina ela imebidi niingie mkopo kwaajili ya kutoa ela ya kamati, kikao cha kwanza tulijadiliana kiwango flani kila mwanakamati atoe iyo,nikajitahidi wiki lile lile nikatoa ile ela. Tumeenda kikao cha pili ela haijatosha ikabidi badgeti ivunjwe ipigwe upya kwasababu ela tulochanga ilionekana ndogo ivyo haiwezi kukidhi mahitaji, kwaiyo kila mwanakamati aongeze tena pesa kwakweli kikao cha pili machozi yalinilenga lenga sana nikicheki sina ndoto za kukaa huku mda mrefu na nina uhakika hii ela ninayoitoa haitarudi na nikicheki mfuko hausomi,yani kama najilazimisha kutoa mchango.
 
Katika maisha hata siku moja usione haya kusema neno SINA au SIWEZI ikiwa jambo lipo nje ya uwezo wako ama halina maslahi yoyote kwako.

HIyo pesa uliyochangia haitorudi wala kukunufaisha chochote zaidi ya kipaja cha kuku utakachokula siku ya shughuli kama utahudhuria.

Ilipaswa siku ile ile ya kwanza ulipohesabiwa ujitoe kwenye kamati. Daima kukaa kimya humaanisha kuridhia.
 
Yaani ningewaambia sina iyo waliopanga ila nitafuta ntayokayo pata na nitawasilisha!!

Me hata WhatsApp group ukiniunga sijui mchango na hujaniambia kabla na left live kabisaaa

Kwa jamii zetu ukishakuwa na ka ajira wanaweza wakakufilisi kwa michango
Kuna mwana alikuwa kila akiniunga kwenye hayo magroup yao naleft mwisho nikasema isiwe tabu nikamblock then nikafuta namba yake nikanyuti kimyaaa. Sasahivi tumekuwa maadui eti
 
Mar pap jirani kaja nyumbani, kapiga hodi nilikuwa nimelala nimechoka na kazi. kapiga piga hodi na kelele nyingi za kuniita niamke, nikaamka kumsikiliza alafu nilikuwa nimechoka sana na night, akanambia habari nikamwambia salama shikamoo kaanza kunisema sema kwanza kisa nimemwaga majivu ovyo wakati huo eneo sio lake ni la kwetu, akidai nachafua mazimgira eneno hilo litatumika kwenye sherehe ya mwanae ivyo nizoe majivu yote niliyomwaga mwaga nikatupe shimoni.

Nikamwambia sawa nitafanya ivyo baada ya kunisema akaniambia nakukaribisha badae nyumbani SAA kumi jioni kwenye kikao, mwanangu anafunga ndoa ivyo karibu tujadiliane hautakwepo pekeako watu wengi watafika kumbuka ni siku ile ile alonisema kuhusu majivu.

Nikamwambia sawa ni mama mtu mzima na ni staff mwezangu kazini japo mimi ni mgeni tu ata miezi sita sina nikamwambia sawa, imefika ile SAA kumi nikaenda nisijue kama kikao kinawahusu wana kamati, kumbe kikao chenyewe ni cha wana kamati kwaiyo ikaonekana nimeudhulia kile kikao na nimekuwa mwanakamati kama kilazima fulani ivi, mana kwenye kikao ikapigwa idadi pale pale ya watu tulohudhulia wakagawanya kwa badgeti ambayo imepigwa pale, dah kimoyomoyo nikajisonya sana,alafu mambo yenyewe kafanya ghafla tumeambiwa mwezi ulopita mwishoni july mchango mwisho tareh 14 August.

Mimi sina ela imebidi niingie mkopo kwaajili ya kutoa ela ya kamati, kikao cha kwanza tulijadiliana kiwango flani kila mwanakamati atoe iyo,nikajitahidi wiki lile lile nikatoa ile ela. Tumeenda kikao cha pili ela haijatosha ikabidi badgeti ivunjwe ipigwe upya kwasababu ela tulochanga ilionekana ndogo ivyo haiwezi kukidhi mahitaji, kwaiyo kila mwanakamati aongeze tena pesa kwakweli kikao cha pili machozi yalinilenga lenga sana nikicheki sina ndoto za kukaa huku mda mrefu na nina uhakika hii ela ninayoitoa haitarudi na nikicheki mfuko hausomi,yani kama najilazimisha kutoa mchango.

Na kingine katuambia July mwishoni, tulikaa kikao iyo siku alotuambia na mwezi huu wa nane weeken ilopita na mchangi mwisho tarehe 14 mwezi wa nane mwishoni ndoa. hii ela unaitoa wapi kwa siku chache ivi mimi najuaga ndoa inatangazwa mapema ili watu wajiandae sijui kakurupuka kumuodhesha mwanae yani dah nikimwangalia ananitia hasira uyu mama jamani!!?
Nakunon'goneza asisikie mtu, kalibu kwenye Uisilamu hatuna michango ya hausi wala ya msiba
 
Back
Top Bottom