Nilitaka nijiunge na JWTZ.

Mfarisayomtata

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
474
188
Mwaka huu nilitaka nijiunge na JWTZ lakini nimeahirisha nasubiri mpaka sakata la kugombea ziwa Nyasa liishe ndo ntajiunga. Isije kuwa unaingia tu unapitiliza.
 
kuwa mzalendo wewe, unadhani kazi ya jeshi ni kuvaa suti kombati baba halafu mstari wa mbele, kama sio kupelekwa huko nyasa utapelekwa somalia au komoro!
 
kiapo cha kazi hiyo ni kuwa tayari kuua au kufa ......
watu kama wewe ni sawa na wale polisi wenye vitambi vikubwa na kunenepa kama mameneja fulani hivi...
kazi ni kazi ... ila inabidi uwe na moyo wa kufanya kazi husika.
wapo watz wapo Sudani, Somalia na wengine sehemu ambazo wanasema wapo coz kumbe ni kazini.
 
Tatizo ni pale unapojikuta unakufa kwa ajili ya mafisadi,
yaani kuifia nchi kwa ajili ya wachache pengine hiki ni
kitu kinachoufanya uzalendo utoweke, yaani we umekufa
halafu kile ulichokipigania kinawanufaisha wachache ambao
wameifanya nchi kama yao huku ndugu zako uliowaacha
wakiteseka.
 
mwaka huu nilitaka nijiunge na jwtz lakini nimeahirisha nasubiri mpaka sakata la kugombea ziwa nyasa liishe ndo ntajiunga. Isije kuwa unaingia tu unapitiliza.
jwtz haihitaji fisi nakuomba wala usisumbuke kuomba kazi huko. Pengine unafaa benki na vitu kama hivyo
 
Back
Top Bottom