Nilishindwa kuuingilia huu ugomvi

Nilishindwa kuuingilia huu ugomvi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,406
Ni kisa cha kweli, tulikutana ukubwani marafiki watatu tulisoma pamoja shule ya msingi.

1. Ni nesi mkunga, ameajiriwa hospitali ya serikali.

2. Police traffic ni mja mzito na amelazwa kwenye wodi ambayo huyu nesi ndiye nesi msimamizi

3. Mimi mpika chapati maarufu wa Kwamtogole.

Traffic Police ana bwana ambae ana mabasi hiaice sijui, unaweza kuona urafiki ulitokea wapi, na ndiye mwenye ujauzito wake. Kila siku anakwenda hospitali na asipoweza anatuma mmoja wa madereva kupeleka mahitaji.

Nesi alipata day off, akasema anakwenda mjini, shost polisi alimuomba apitie kwa bwana wake akamchukulie khanga na night dress kabatini kwani yule mwanaume anasahau kuvileta hospitali.

Nesi alichelewa sana kurudi, aliporudi amekwenda kumuona mgonjwa lakini hana khana wala night dress, anasema yule mwanaume hakumkuta lakini inabidi arudi kesho yake kwani amesahau handbag yake.

Ilipofika hapo niliaga na kuondoka kwani nilimpelekea mgonjwa chapati.
 
Manesi wako vizuri sana katika kupetipeti....inawezekana alimpunguzia uchovu huyo bwana mkubwa wa mabasi
 
huyo alienda kweli akamkosa mhusika.. sasa wakati wa kurudi akasahau.. inatokea lkn with conditions mf. hakuwa ameweka kitu cha muhimu kwa begi kama nauli. au alikuwa na vibegi viwili kidogo kabeba.. au kuna mazingira ambayo mpk muhusika akuhadithie.. lakini hutokea hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom