Nchi yetu, vituko haviishi. Kila sehem kuna mambo yake. Na watu wake huamini kuwa ni mambo ya kawaida na ndio nchi inatakiwa iende hivyo. Licha ya kwamba mengi katika yanayotokea tuhuma huelekezwa kwa serikali lakini sisi wananchi tunanafasi kubwa ya ukombozi wa nchi yetu.
Pale uwanjani wakati wa kucheck in, wakaniambia mzigo wangu umezidi kama kilo 8. Nilishtuka kwa sababu huwa ninakawaida ya kucheck uzito wa mzigo kabla ya kusafari. Mara hii nikapatwa na hofu maana ni jambo ambalo huwa sipendi kamwe linitokee. Wale wahudumu wa pale, (hasa dada mmoja mjamzito), akawa wa kwanza kunirukia kila kilo dollar 30 kwahiyo inabidi ulipe dollar 240. Akaitwa mtu kwa haraka wewe toa beki lake weka pale. Aliyetoa begi akaniambia wewe ongea nao uwape chochote. Bahati mbaya hili la chochote huwa si katika mfumo wangu wa maisha niliojiwekea. Nikaanza kutoa baadhi ya vitu lengo hasa likiwa vibaki. Wale wahudumu pale wakaendelea kuninasihi niongee na wale watu pale watakubali. Wakati ninafanya hayo, akapita mzungu mwingine naye nikaangalia mzani wake ukawa umezidi wakamuacha aende. Sikujali lile kwa kuwa sikuwa muhusika wa ule mzigo, mara ghafla dada yule akarudi alivyoona kuwa kweli natoa mizigo akasema nakupa allowance ya 5kg, nikabaki ninaduwaa, kumbe anauwezo huu. Nikapack tena vitu vyangu, kupima mzigo haujazidi. Sikuelewa hasa tatizo lipo wapi. Lakini pia kauli za pale zilikuwa ni zenye kukera mno na zimejaa dharau ya hali ya juu. Kuna haja ya sisi Watanzania kujifunza kufanya kazi. Ubabaishaji hautatufaa kamwe. Naamini hii inaweza kuwasaidia watoa huduma wengine lakini pia nitawaandikia na wenye ndege maana wanahangaika na competition lakini kuna watu wanawaangusha.
Mkuu I can bet hiyo ni SWISSAIR. Nilisafiri na hiyo ndege kama wiki kama tatu zilizopita na mimi nilikutana na hivyo vituko vya huyo dada mjamzito!!! Aliniambia mzigo wangu umezidi kilo 3 na hivyo inabidi nilipe dola 90, kwa maana ya dola 30 kwa kilo. Ukweli ni kwamba zilikuwa zimezidi kilo mbili tu wala sio tatu. Nilimweleza kwamba sina tatizo na kulipia hizo kilo tatu ila ningependa nilipe kwa kutumia credit card kwa kuwa sikuwa na cash. Aliniangalia mara mbili mbili na kuamua kuniachia.
Ukweli huyu dada atawaharibia biashara SWISSAIR kama hatajirekebisha!!!!
Tiba
Pole sana !
Mara nyingi kama unaondoka watakufanyia hayo. Kama haitoshi watakuomba chenji. Ninachokifanya huwa ninakuwa na USD 1 moja moja nyingi. Kupunguza shuruba zao huwa nawapa USD 3 - 5 maana huwa hawahebabu na mimi naishia zangu. Kuna siku ofisa wa uhamiaji aliniuliza kijana mbona unasafiri sana kazi yako ni nini? Nikamjibu pamoja na kusafiri afande ni sehemu ya kazi yangu. Akaniangalia na kuniambia sasa utaniachaje? hahahahahah nikamlambisha dolla 2 nikaendelea zangu.
Wakati wa Kurudi baada ya kumalizana na Immigration, unasubiri mizigo ambayo mara nyingi hubebwa kwa mikono maana ile mashine ya kuzungusha mizigo huwa ni Mbovu, ukitoka kuna wale jamaa wa TRA wanafungua mizigo kukagua....Mara nyingi mimi huweka chupi juu wakifungua wanaboreka na kuniambia Mchungaji endelea nitoe basi nisikague mizigo yote najua umechoka....nao huwapa USD moja moja.
Hii ni Made in Tanzania
Nimejifunza mbinu mbili vyupi na credit card watanikoma
sasa kama unajiamini na unajua uzito haukuzidi kwanini uliupunguza? by the way hiyo hiyo CCM unayoilamba miguu ndio imekuletea hizo kero. au akili zako hazijangamua?Nchi yetu, vituko haviishi. Kila sehem kuna mambo yake. Na watu wake huamini kuwa ni mambo ya kawaida na ndio nchi inatakiwa iende hivyo. Licha ya kwamba mengi katika yanayotokea tuhuma huelekezwa kwa serikali lakini sisi wananchi tunanafasi kubwa ya ukombozi wa nchi yetu.
Pale uwanjani wakati wa kucheck in, wakaniambia mzigo wangu umezidi kama kilo 8. Nilishtuka kwa sababu huwa ninakawaida ya kucheck uzito wa mzigo kabla ya kusafari. Mara hii nikapatwa na hofu maana ni jambo ambalo huwa sipendi kamwe linitokee. Wale wahudumu wa pale, (hasa dada mmoja mjamzito), akawa wa kwanza kunirukia kila kilo dollar 30 kwahiyo inabidi ulipe dollar 240. Akaitwa mtu kwa haraka wewe toa beki lake weka pale. Aliyetoa begi akaniambia wewe ongea nao uwape chochote. Bahati mbaya hili la chochote huwa si katika mfumo wangu wa maisha niliojiwekea. Nikaanza kutoa baadhi ya vitu lengo hasa likiwa vibaki. Wale wahudumu pale wakaendelea kuninasihi niongee na wale watu pale watakubali. Wakati ninafanya hayo, akapita mzungu mwingine naye nikaangalia mzani wake ukawa umezidi wakamuacha aende. Sikujali lile kwa kuwa sikuwa muhusika wa ule mzigo, mara ghafla dada yule akarudi alivyoona kuwa kweli natoa mizigo akasema nakupa allowance ya 5kg, nikabaki ninaduwaa, kumbe anauwezo huu. Nikapack tena vitu vyangu, kupima mzigo haujazidi. Sikuelewa hasa tatizo lipo wapi. Lakini pia kauli za pale zilikuwa ni zenye kukera mno na zimejaa dharau ya hali ya juu. Kuna haja ya sisi Watanzania kujifunza kufanya kazi. Ubabaishaji hautatufaa kamwe. Naamini hii inaweza kuwasaidia watoa huduma wengine lakini pia nitawaandikia na wenye ndege maana wanahangaika na competition lakini kuna watu wanawaangusha.
Mkuu si uwalipue tu kama wakikuletea upuuzi :A S 13: !!!
uwalipue kwa nani, system imeoza toka chini mpaka juu.