fabianmalaba
JF-Expert Member
- Feb 21, 2017
- 280
- 183
Nilipata binti mmoja, nikaanza mahusiano nae kimapenzi, baada ya miezi miwili akasema kapoteza simu, nikampa nyingine, siku tatu zilizofuata nikapigiwa na mwanaume kwa namba ileile aliyosema imepotea akinisihi niachane na mke wake.
Niliamua kuongea na huyo mwanaume na nikabaini ni mume halali wa huyo binti japo kuna muda walitengana na kurudiana hivyo hawana maelewano vizuri ndani ya ndoa yao, kwa bahati nzuri au mbaya huyu binti tayari ana ujauzito wangu, mumewe hajui na alinisihi niachane na mke wake.
Kweli niliamua kuachana na huyo binti lakini kila kukicha naamka nikifungua simu nakuta meseji za huyo binti zaidi ya 10 anataka nimrudie maana ananipenda sana na anahitaji tuendelee kimahusiano,juzi kaniomba nimsindikize kliniki nikakataa,
SASA NIPO NJIAPANDA SIJUI CHA KUFANYA, NIMKATALIE NA KIUMBE KILICHO TUMBONI MWAKE AU NIKUBALI LAKINI NIINGIE KWENYE BALAA NA HUYO JAMAA.