Trinity
JF-Expert Member
- Jul 20, 2017
- 1,867
- 3,618
Kwanza kabisa niwape pole kwa msiba mzito wa rais wetu Jpm.
Binafsi nimehuzunika sana kumpoteza mtetezi wa wanyonge, mzalendo, mkweli, mchapa Kazi, mbunifu, mcha Mungu,
na jasiri.
Niende direct kwenye Mada,
Aisee nimekua nashangaa watu nikiwaomba chenji wanapata wasiwasi na kuniuliza, pesa yako haina miguu??
Wengine wamekua wakinyima chenji kabisa mpaka unakasirika na kuwaona wana roho mbaya.!
Ipo hivii, kuna eneo la stend nikiwa nimetulia nasubiri wateja waje, akaja dogo amempakia abiria kwenye boda.
Walisimama Karibu yangu na kuomba chenji ya elfu 10 nikasema ninayo ila ni elfu tano tano, dereva boda akasema hiyo hiyo.
Nikazama mfukoni nikatoa kitita cha elfu 60. Elfu 10, kumi zilikua 3 nyingine zilikua elfu tano tano tu.
Nikatoa elfu tano mbili nikampa ile elfu 10 yake nikaikunja na zile nyingine, kwa hiyo elfu kumi kumi nikawa nazo 4.
Hee, baada ya muda kidogo kupita nikaenda mpesa nimtumie mtu elfu 20.
Kuchomoa kitita changu nakuta elfu kumi aliyonipa siioni, niliikariri maana zangu zilikua mpya nahisi second au first hand kabisa kutoka zitengenezwe ila ile ten yake ilionesha imetumika zaidi.
Nilijisachi mpaka kwenye soksi nikavua viatu lkn wapi.
Nilishangaa sana, ile narudi nikamcheki aliposhuka yule jamaa, akawa hayupo na wakati hakuna bus limepita na abiria wengine walikuwa wamekaa kwenye banda la kungojea usafiri.
Nikaja kuconnect na jinsi walivyofika pale nikaamini walikuwa kitu kimoja maana walipofika walikuwa wanaongea kwa sauti ya chini kabla ya kunifuata, sikuwafikiria sana mi nikawa busy tu na smart yangu nafuatilia matukio ya msiba wa taifa.
Wanaonyima chenji nimeamini hawajipendei, imewapasa kufanya hivyo kutokana na mambo ya kihuni kama hivi.
Kama una kisa cha kuibiwa pesa kimazingara kama hivi, tunaomba ushuhuda na jinsi ya kuzuia hawa chuma ulete.!