Daktari wa Meno
JF-Expert Member
- Sep 5, 2019
- 509
- 1,617
Kipindi fulani nikiwa kijijini nilikuwa nimebuni kitoweo ambacho kwa kweli kulikuwa kinanipa sana nyama ila kupatikana kwake haikuwa kazi ndogo.
Nilikuwa nakata ndimi za ng'ombe na kunywa supu bila wenye ng'ombe kujua kama wanyama wao hawana ndimi. Siku moja nikiwa nimekaa wazo likaniijia namna gani naweza kupata vitoweo kwa ajili ya ugali. Niliwaza uvuvi ila kijijini hakukuwa na chanzo chochote cha maji ambacho kinaweza kufanya uvuvi.
Siku moja nikapata wazo na kukata ndimi za ng'ombe na nikafanya majaribio nikaona mafanikio ni makubwa sana. Nilichokuwa nafanya ni kwenda zizini kwa mtu usiku na kumfunga ng'ombe kwa kamba imara ili asinijeruhi (kwa wale ng'ombe wakorofi) nikishamfunga nabana taya zake kwa vidole kisha atatoa ulimi nje, akitoa tu naukata kwa kisu nusu ya ulimi nakuwa nimeikata na kisha nampaka chumvi na dawa moja hivi ya kienyeji ili asioze ulimi.
Basi nilikuwa nafanya hadi kupata ndimi 10 kwa usiku mmoja, ilikuwa ni kazi ya hatari ila nilikuwa napata sana pesa na kitoweo kwa ajili hiyo. Mafanikio yakawa makubwa na sasa nikaamua kuuza supu ya ulimi pale kijijini hakuna mtu alijua kuwa asilimia kadhaa ya ng'ombe wamekatwa ndimi kijijini pale. Basi nikawa napika jioni supu, usiku naenda kutafuta ndimi kwenye mazizi ya ng'ombe.
Ile kazi iliendelea baadae nikaona soko limekuwa baya nikaamua kuacha maana ndimi ziliadimika sana, kuna muda nikawa naenda hadi vijiji jirani kupata hizo ndimi kwa ajili ya biashara na kitoweo.
Vijana ajira ni akili yako sio akili za wanasiasa.