Nilikutana na mwanamke mjane

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
39,981
96,229
"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke
mjane aliyekua na binti mkubwa tu na mimi na
huyo mjane tukaamua kuoana. Baadaye baba
yangu akamuoa binti yangu wa kambo (yaani
binti
wa huyu mke wangu niliyemwoa akiwa mjane),
hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama
yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto
wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu
akawa mama mkwe wa mkwe wake.
Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu
wa
kambo (ambaye kwa sasa ndiye mke wa baba
yangu na hivyo kuwa pia mama yangu wa kambo)
alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume
akawa mdogo wangu kwa sababu tulichangia baba
mmoja. lakini kwa vile pia alikua ni mtoto wa
binti
wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke
wangu na mimi nikawa babu yake huyo mdogo
wangu.
Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na
mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa
msichana (yaani binti ya mke wangu ambaye pia
ni
mke wa baba yangu) ambaye ni ndugu wa mtoto
wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao
mmoja, akawa pia bibi yake na mwanangu
(mwee!!). Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu
kuwa
shemeji wa mtoto wangu (achilia kuwa babu
yake!!) ambaye ndugu yake wa kike kwa upande
wa
mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo
mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo
ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa
binti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni
mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu
yangu mwenyewe... KAMA HAUJAELEWA MUITE
MKALI WA KISWAHILI UNAYEMJUA AJE
AKUDADAVULIE.
 
Back
Top Bottom