Nilikubali kuibiwa ili niweze kumkamata mwizi

Nilikubali kuibiwa ili niweze kumkamata mwizi

The Thugs001

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2018
Posts
471
Reaction score
974
Kwanza mimi sio mwandishi mzuri kwenye mapungufu ya uandishi tuvumiliane.

Mimi ni mfanyabishara wa vitu mbali mbali vya umeme Electronics item nategemea sana wateja wa online yanii kupatana, instgram, Facebook na magroup ya whtsapp.

Kuna wizi unaojulikana wa miamala or muamala zile za kupokea sms kama hii:

Imethibitishwa umepokea Tsh 900,000/= kutoka NBC Bank Ref namba LG14TY. Tembelea tawi lolote la NBC ndani ya siku 7. Neno la siri 3193858. Ahsante kwa kutumia NBC Bank..




hii sms unayotumiwa inakuja katika simu yako ikiwa Sender ni Bank husika kama NMB, CRDB,NBC kama nilivyo ionyesha hapo chini katika picha...inasemekena kuna Application inaitwa Sender wanadownload hawa wezi hio Application ndio inawawezesha kumfanya mpokeaji kupokea sms ikijitambulisha imetoka bank husika

Wizi huu unalenga sana wafanyabiasha wa mitandaoni, mbinu anayoitumia mwizi ni kujifanya mteja wa item iliyopostiwa sehemu nilizotaja hapa juu.

INAKUAJE: Utapokea simu kutoka kwa mwizi mara nyingi ni muda wa mchana. Atajitambulisha kuwa yeye ni mteja wa item uliyoipost sana sana wanalenga Tv, Redio, Camera, laptop.

Hapa atakupigia mtapatana bei mara nyingi hawalalamiki sana katika bei discount kidogo tu ukimpatia anaridhika. Mkishakubalina bei atakwambia yeye yupo safarini or mkoani sana sana Dodoma, then mnunuzi (mwizi) atakujulisha anae kijana wake anayeweza kumsaidia kumsafirishia hio item (bidhaa) ukumbuke amekupigia mchana ila huyo kijana anyezungumziwa kuwa atapokea hio item muda wake wake unakuwa ni jioni kuanzia saa 12 ndio anaweza kuonana na wewe muuzaji.

Hatua ya pili: Muuzaji wa bidhaa kupeleka bidhaa kwa mpokeaji mara nyingi maeneo yao ni Mwenge, Ubungo, Magomeni, Mbezi
Ukishaonana na mpokeaji anaweza kuikagua ila mara chache sana, mara nyingi mkionana wewe muuzaji ndio unampigia simu yule Mwizi kuwa nimeshaonana na kijana atakwambia naomba namba nikurushie pesa namba atakazoitaji ni Zantel , Airtel, Vodacom.
Ukishatuma namba kati ya hizo utapokea SMS ya Bank kama hio ya juu hapa katika kutumiwa pesa kunachukua muda sana dakika 5 mpaka 10 na anaweza kuomba no ya mtandao mwingine kama ulimpa ya Vodacom anaweza kuitaji ya Airtel, ukishapokea pesa ukiridhika na pesa SMS uliyoipokea inakuwa ndio biashara imekwisha kijana unamkabidhi item anaondoka.

Hio style ya SMS wameshaibiwa sana madalali wa Kariakoo wanaochukua item madukani (mali kauli) na kupost katika mitandao wameshapeleka sana item katika hizo sehemu nilizotaja hapo juu then wanarudi madukani na hizo SMS feki TV zimeshaibiwa sana Ubungo mpka inch 65 mtu anapeleka mbili n.k zinaibiwa kwa njia hio.

Tukio: Nilipokea Simu kama ilivyo kawaida yao kwakuwa habari zao ninazo tulijipanga kwenda kukamata. Mnunuzi kama kawaida alitupa location Ubungo pale stendi ya mwendokasi nimekutana na kijana nikamuonyesha item wala hakuikagua, mwizi akanipigia simu nikasubiri pesa kama kawaida nikapokea SMS ya muamala hewa basi tukamkata aliyekuja kupokea tuondoka nae

Utafiti: Mwizi anatumia akili nyingi sana katika kufanikisha wizi wake.. kwanza anakusanya namba za bodaboda na walinzi sehemu za kulaza magari bila ya wao kujua kuwa mtu wanayetengeneza nae urafiki ni mtu wa dizaini gani ila anakuwa na namba zao kwa njia ya urafiki, mazoea.

Mwizi anakuwa na access za namba zao anaishi nazo kwa kazi yake asilimia 99% bodaboda na mlinzi wa sehemu ya kulazia magari awajuani na mwizi yanii mwizi atokee mbele ya bodaboda hapo huyo badobado amkumbuki mwizi walionana wapi yeye mwizi anavuna no ya simu tu kwa njia anayoijua yeye anaishi nayo namba

Rejea: Siku unayopeleka item sehemu muda wote anayetaka kujua umefika wapi ni yule mwizi wa mkoani, Huyu mpokeaji mara nyingi unarushiwa no yake tu na mara nyingi huwa inatokea umepewa location kama ubungo pale mwendokasi ndio upeleke item ila gafra anaweza kukwambia dogo ametoka njoo River side, Kibo n.k ina maana anampigia bodaboda mwingne atakayekuwa available sehem zile zile sio location ya mbali. Pia huyu unayemkabidhi mara nyingi sana hakagui mali na smtmz na yeye anakuwa na haraka katika mishe zake za kukimbilia abiria anakwambia mpigie jamaa (huyo mkoani) atume pesa

Huyu bodaboda akishaipokea item kutoka kwako anapigiwa simu na mwizi anaelekezwa apeleke sehem ya kulazia magari

Mlinzi nae anakuwa amjui jamaa ila anavyopigiwa simu na mwizi anatengenezewa mazingira kama vile wanajuana juna anaweza kumwambia mimi huwa nalaza gari hapo scania, kenta n.k nikija kulaza gari hapo baadae nitachukua huo mzigo wangu

Bodaboda anaweza kulipwa na mlinzi wakati huo mlinzi anategemea jamaa akija kulaza gari atarejeshewa na yeye atapewa chake...

Mzigo ukifika kwa mlinzi utafatwa na bodaboda mwingne kabisa na huyu bodaboda anaonana na mwizi wakati anapeleka item kwa mwizi na huyu bodaboda ajui kuwa huyu ni mwizi ila wanaonana ila mda mwingine mzigo unalala mpka asubhui pale kwa mlinzi unafatwa asubhui na bodaboda. Kwa kawaida mwizi huwa aingii front kabisa katika ilo tukio

Mwizi anakuwa na simu zaidi ya 3 mpka 5 anakuwa na line zaidi ya 30 na hizi simu na line zote zinakuwa za magumashi simu za wizi na line za wizi

Siku ya kumkamata: Utafiti ulikamilika baada ya kuwakamata wanaotumwa yanii bodaboda na walinzi mara mbili sehemu mbili tofauti mwaka jana mwezi 12.

Mwaka huu nimepokea simu kutoka kwa mwizi mazungumzo yake ndio yananitambulisha kujua kama ni wale wale kutokana na maelezo niliyoyatoa hapo.

Nikampelekea TV ubungo riverside ile TV ilikuwa na track ( inatumia umeme na betri) inaweza kusoma location kama kawaida kijana amekuja wa bodaboda nikawa nae pale ikaingia sms hewa ya bank nikaipokea nikakubali kuibiwa.

Kijana nikamkabidhi item mwizi aknipigia nikwambia fresh shukran pesa nimeiona biashara imekwisha bodaboda akaondoka zake timu kazi ilijipanga tukaifatilia bodaboda..hii bodaboda ikafatiliwa bila kujijua mpaka kanisa la Kkt riverside kuna sehemu ya kulaza magari kijana wa bodaboda akaondoka baadae ikaja bodaboda nyingine ikabeba nayo tukaifatilia mpka Ubungo kibo, kaka mwizi akajitokeza akabeba TV akaingia nayo tukaenda kumalizana nae anaitwa Makamba, mwenzie mmoja anaitwa Inno ameshafariki Katika tukio la wizi ila mwingine anaitwa Hassan bado yupo.
View attachment 1629150
 
Huyo ilikuwa unampiga picha japk sheria ina yake pia, halafu unatenganisha kiungo kimoja baada ya kingine kwa lengo la kufanya scrape, mfano pua, sikio na kadhalika

Sent from my HD1910 using JamiiForums mobile app
Hao wa mwanzo tulikamata lakini tuligundua hamna kitu wanachokijua na polisi hatukuweza kupata msaada mkubwa tukaamua kudili nao wenyewe kwa njia zetu
 
Hao wa mwanzo tulikamata lakini tuligundua amna kitu wanachokijua na polis atukuweza kupata msaada mkubwa tukaamua kudili nao wenyewe kwa njia zetu
Nishaumizwa na hao kunguru ni sawa wale hiyo pesa tuma huku para "hallo unaongea na ... kutoka vodacom /tigo/ Airtel /Halotel,
Alivyompumbavu anamuuliza tafadhali nataka kujua naongea na nani?

Kumbuka alishakuambia umeshinda kiasi au ...

Sasa wa hivyo si unatamani umpate live na njia nzuri ni wewe mwenyewe kushughulika naye na si hao usalama/polisi

Usalama mzuri wa kumsaidia ni wewe ndio amekuchagua umpe

Sent from my HD1910 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza mimi sio mwandishi mzuri kwenye mapungufu ya uandishi tuvumiliana.

Mimi ni mfanyabishara wa vitu mbali mbali vya umeme Electronics item nategemea sana wateja wa online yanii kupatana, instgram, Facebook na magroup ya whtsapp.

Kuna wizi unaojulikana wa miamala or muamala zile za kupokea sms kama hii:

Imethibitishwa umepokea Tsh 900,000/= kutoka NBC Bank Ref namba LG14TY. Tembelea tawi lolote la NBC ndani ya siku 7. Neno la siri 3193858. Ahsante kwa kutumia NBC Bank

Wizi huu unalenga sana wafanyabiasha wa mitandaoni, mbinu anayoitumia mwizi ni kujifanya mteja wa item iliyopostiwa sehemu nilizotaja hapa juu.

INAKUAJE: Utapokea simu kutoka kwa mwizi mara nyingi ni muda wa mchana. Atajitambulisha kuwa yeye ni mteja wa item uliyoipost sana sana wanalenga Tv, Redio, Camera, laptop.

Hapa atakupigia mtapatana bei mara nyingi hawalalamiki sana katika bei discount kidogo tu ukimpatia anaridhika. Mkishakubalina bei atakwambia yeye yupo safarini or mkoani sana sana Dodoma, then mnunuzi (mwizi) atakujulisha anae kijana wake anayeweza kumsaidia kumsafirishia hio item (bidhaa) ukumbuke amekupigia mchana ila huyo kijana anyezungumziwa kuwa atapokea hio item muda wake wake unakuwa ni jioni kuanzia saa 12 ndio anaweza kuonana na wewe muuzaji.

Hatua ya pili: Muuzaji wa bidhaa kupeleka bidhaa kwa mpokeaji mara nyingi maeneo yao ni Mwenge, Ubungo, Magomeni, Mbezi
Ukishaonana na mpokeaji anaweza kuikagua ila mara chache sana, mara nyingi mkionana wewe muuzaji ndio unampigia simu yule Mwizi kuwa nimeshaonana na kijana atakwambia naomba namba nikurushie pesa namba atakazoitaji ni Zantel , Airtel, Vodacom.
Ukishatuma namba katika ya hizo utapokea SMS ya Bank kama hio ya juu hapa katika kutumiwa pesa kunachukua muda sana dakika 5 mpaka 10 na anaweza kuomba no ya mtandao mwingine kama ulimpa ya Vodacom anaweza kuitaji ya Airtel, ukishapokea pesa ukiridhika na pesa SMS uliyoipokea inakuwa ndio biashara imekwisha kijana unamkabidhi item anaondoka.

Hio style ya SMS wameshaibiwa sana madalali wa Kariakoo wanaochukua item madukani (mali kauli) na kupost katika mitandao wameshapeleka sana item katika hizo sehemu nilizotaja hapo juu then wanarudi madukani na hizo SMS feki TV zimeshaibiwa sana Ubungo mpka inch 65 mtu anapeleka mbili n.k zinaibiwa kwa njia hio.

Tukio: Nilipokea Simu kama ilivyo kawaida yao kwakuwa habari zao ninazo tulijipanga kwenda kukamata. Mnunuzi kama kawaida alitupa location Ubungo pale stendi ya mwendokasi nimekutana na kijana nikamuonyesha item wala hakuikagua, mwizi akanipigia simu nikasubiri pesa kama kawaida nikapokea SMS ya muamala hewa basi tukamkata aliyekuja kupokea tuondoka nae

Utafiti: Mwizi anatumia akili nyingi sana katika kufanikisha wizi wake.. kwanza anakusanya namba za bodaboda na walinzi sehemu za kulaza magari bila ya wao kujua kuwa mtu wanayetengeneza nae urafiki ni mtu wa dizaini gani ila anakuwa na namba zao kwa njia ya urafiki, mazoea.

Mwizi anakuwa na access za namba zao anaishi nazo kwa kazi yake asilimia 99% bodaboda na mlinzi wa sehemu ya kulazia magari awajuani na mwizi yanii mwizi atoke hapo bodaboda amkumbuki mwizi walionana wapi yeye mwizi anavuna no ya simu tu kwa njia anayoijua yeye anaishi nayo namba

Rejea: Siku unayopeleka item sehemu muda wote anayetaka kujua umefika wapi ni yule mwizi wa mkoani, Huyu mpokeaji mara nyingi unarushiwa no yake tu na mara nyingi huwa inatokea umepewa location kama ubungo pale mwendokasi ndio upeleke item ila ghafla anaweza kukwambia dogo ametoka njoo River side, Kibo n.k ina maana anampigia bodaboda mwingne atakayekuwa available sehem zile zile sio location ya mbali. Pia huyu unayemkabidhi mara nyingi sana hakagui mali na smtmz na yeye anakuwa na haraka ya kuwahi abiria anakwambia mpigie jamaa (huyo mkoani) atume pesa

Huyu bodaboda akishaipokea item kutoka kwako anapigiwa simu na mwizi anaelekezwa apeleke sehem ya kulazia magari

Mlinzi nae anakuwa amjui jamaa ila anavyopigiwa simu na mwizi anatengenezewa mazingira kama vile wanajuana juna anaweza kumwambia mimi huwa nalaza gari hapo scania, kenta n.k nikija kulaza gari hapo baadae nitachukua huo mzigo wangu

Bodaboda anaweza kulipwa na mlinzi wakati huo mlinzi anategemea jamaa akija kulaza gari atarejeshewa na yeye atapewa chake...

Mzigo ukifika kwa mlinzi utafatwa na bodaboda mwingne kabisa na huyu bodaboda anaonana na mwizi wakati anapeleka item kwa mwizi na huyu bodaboda ajui kuwa huyu ni mwizi ila wanaonana ila mda mwingine mzigo unalala mpka asubhui pale kwa mlinzi unafatwa asubhui na bodaboda. Kwa kawaida mwizi huwa aingii front kabisa katika ilo tukio

Mwizi anakuwa na simu zaidi ya 3 mpka 5 anakuwa na line zaidi ya 30 na hizi simu na line zote zinakuwa za magumashu simu za wizi na line za wizi

Siku ya kumkamata: Utafiti ulikamilika baada ya kuakamata wanaotumwa na walinzi mara mbili sehemu mbili tofauti mwaka jana mwezi 12.

Mwaka huu nimepokea simu kutoka kwa mwizi mazungumzo yake ndio yananitambulisha kujua kama ni wale wale kutokana na maelezo niliyoyatoa hapo.

Nikampelekea TV ubungo riverside ile TV ilikuwa na track ( inatumia umeme na betri) inaweza kusoma location kama kawaida kijana amekuja wa bodaboda nikawa nae pale ikaingia sms hewa ya bank nikaipokea nikakubali kuibiwa.

Kijana nikamkabidhi item mwizi aknipigia nikwambia fresh shukran pesa nimeiona biashara imekwisha bodaboda akaondoka zake timu kazi ilijipanga tukaifatilia bodaboda..hii bodaboda ikafatiliwa bila kujijua mpaka kanisa la ktk riverside kuna sehemu ya kulaza magari kijana wa bodaboda akaondoka baadae ikaja bodaboda nyingine ikabeba nayo tukaifatilia mpka Ubungo kibo, kaka mwizi akajitokeza akabeba TV akaingia nayo tukaenda kumalizana nae anaitwa Makamba, mwenzie mmoja anaitwa Inno ameshafariki. Katika tukio la wizi ila mwingine anaitwa Hassan bado yupo.
Wewe ndo mwenye ile clip inayozunguka WhatsApp ikielezea hili tukio?
 
Back
Top Bottom