kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,068
- 18,075
Nimeona kwenye hii habari kuwa Tz ina makombora ya masafa marefu na masafa ya kati
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali John Mkunda amefunga mazoezi ya kijeshi Brigedi ya Faru, yaliyohusisha makombora ya masafa ya kati na masafa marefu, yakitambulika kwa jina la ‘Kaa tayari,’ ambayo yalikuwa na askari zaidi ya elfu moja.
Kwa majuma mawili, askari wa miguu wa JWTZ wamekuwa katika Pori la Hifadhi ya Msitu Nyahua wilayani Sikonge - Tabora wakifanya mazoezi ya matumizi ya silaha za moto, ambazo ni makombora ya masafa ya kati na yale masafa marefu, huku wakitembea kwa miguu umbali wa zaidi ya kilometa 100 usiku na mchana bila kujali mvua wala jua, wakivuka mito, milima na mabonde kuonesha ukakamavu.
Jenerali Mkunda amesema Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litaendelea kuboresha vikosi vyake kwa mazoezi pamoja na kuvipatia vifaa vya kisasa zaidi…mkakati unaolenga kukabiliana na vitisho vinavyondelea kujitokeza kwa nchi mbalimbali duniani.
#AzamTVUpdates