Nilikataa sasa nimekubali! Hata matajiri wameanza kuishi kishetani!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Nilikataa kuwa kamwe matajiri wa Tanzania hawawezi kuishi kishetani ila sasa nimekubali.

Shughuli ninazozifanya zimetokea kuniweka karibu au kunifanya niwakaribie matajiri wa kitanzania ila sasa nimeanza kuwanotice wakibehave tofauti na zamani.

Matajiri wamepunguza wafanyakazi kwa kiasi kikubwa, wakiwaacha hawa watu watopee kwenye ukosefu wa kipato na familia zao kufa njaaa. Japo kuna tajiri mmoja tu ndio nimesikia kagoma kupunguza wafanyakazi.

Ameamua kiwanda chake kizame kikiwa na wafanyakazi wake kwa vile anachelea kuua njaa familia za watu.

-Matajiri wamepunguza matumizi... Hata ukienda supermarkets bidhaa hazitoki kabisa. Magari show room mengine yana miaka kadhaa utadhani yamekuwa majengo.

- Matajiri wamepunguza kufanya shughuli za maendeleo kama vile ujenzi, shughuli ambazo zilikuwa zinachochea maendeleo ya nchi.

Ama kweli matajiri wameanza kuishi kishetani, na aina hii ya maisha itaondoka na watu wengi hasa kwa misongo ya mawazo na BP.
 
Huo ni uongo matajiri walio wengi wana pesa na vitega uchumi ndani na nje ya Tanzania.Mara zote tajiri anakuwa na plan B.Kusubiri eti wataishi kama mashetani ni plan za kitoto.Dua la kuku halimpati mwewe.
 
Huo ni uongo majiri walio wengi wana pesa na vitega uchumi ndani na nje ya Tanzania.Mara zote tajiri anakuwa na plan B.Kusubiri eti wataishi kama mashetani ni plan za kitoto.Dua la kuku halimpati mwewe.
Umesema vema. Wenye busara watahoji je matajiri kuishi kama mashetani kumewasaidia nini maskini?
Matajiri wakipunguza wafanyakazi anayeumia ni nani?
Matajiri wakipunguza wafanyakazi, je ni dalili nzuri kwa nchi yetu?
Ukweli ni kwamba wafanyakazi wakipunguzwa ni ongezeko la maskini(mashetani).
Tuache kushabikia utaratibu unaoua uchumi wa nchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom