Nilikaa na jini chumbani masaa sita sitasahau

Nilikaa na jini chumbani masaa sita sitasahau

gen parton

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
642
Reaction score
411
Dunia tunayoishi ina mambo mengi ambayo hatuyajui japo wanadamu huwa tunajifanya wajuvi wa mambo mengi, Hasa kwa sie tunaotumia milango mi 5 ya fahamu yaani kuona, kusikia ,kunusa, kupapasa na kuonja lakina wapo binanadamu ambao ama kwa kudra za MUNGU au kwa utundu wao hawa milango 6 ya fahamu huona ambayo sisi binadamu wakawaida hatuwezi kuona, Tuje kwenye point mimi ni mwenyeji wa mbeya kwa baba na mama na familia yetu ukweli MUNGU katupendelea kuhusu mambo ya kipato tuko vizuri kiasi chake elimu ya msingi tu ndio nilisomea hapa tz secondary O level hadi A level nilisomea zambia kwa wenyeji wa mbeya ni kawaida tu chuo nilienda kusomea kenya nilisomea mambo ya utalii sababu huwa tunaamini hawa wenzetu wapo juu katika hii field baada ya kumaliza tu nilifanikiwa kupata kazi visiwani katika hotel moja katika pwani ya kiwengwa ntahiifadhi jina kwa sababu maalum katika nafasi ya umenager niweke wazi wenzetu wazanzibar hawakufurahihishwa na huwa hawafurahishwi na hii hali, kuna siku jumamosi jioni moja nikiwa nyumbani nilipopanga maeneo ya mwanakwelekwe nje ya nyumba tulikua watatu na rafiki zangu tunabadilishana mawazo alikuja dada moja chotala wa kiarabu kwa zenji wako wengi tu akatuulizia mtu ambae kwakweli hatukumfahamu licha kua tulikua na mwenyeji ambae pale mtaani anamiaka zaidi ya saba hakuweza kumfahamu mtu aliekua anauliziwa basi ikawa imepita kama kawaida yetu vijana baada kuondoka tukaanza kumsifia hapa niweke wazi kweli mdada alikua kaumbika lakini kati yetu hakuna aliyefanya jitihada za kumfuatilia alipotokomea, akipita kama wiki nikiwa kwenye boti see bus 2 naelekea dar mara nikamfananisha yule dada wakati bado najiuliza ni yeye au mwingine mara akanyoosha hadi nilipo na kunisalimia kwa jina langu akili akawa kama imefungwa sikumuuliza nani kamtajia jina langu alikua mcheshi na kunitajia jina lake ni jasmini mpaka tuna fika dar alikua ni story bandika bandua nikamu aproach hakua na hiyana ajabu baada ya kushuka tu kapotezana sikuwahi hata kuchukua contact zake nikajilaumu kwa hilo kwani tulishaadiana baada ya wiki mbili hivi wote tungekua tumesharudi zenji tutafutane nikaona basi hakua ridhiki, Baada ya wiki mbili nikarejea kazini kama kawaida mida ya saa tisa nikaona simu imepigwa kwa namba ngeni ambazo sio mitandao ya tz nikajua maadamu tunadeal na foregners huenda moja wao kapiga baada ya kupokea msemaji akajitambulisha ni Jasmini story zikaanza ajabu sikumuuliza no zangu katoa wapi tukakubaliana tutoke weekend lakini akasisitiza atakuja gheto kwangu nilikua nimepanga chumba kimoja na sebule, jamaa zangu niliwaelezea wakataka wathitishe hivyo siku Jasmini anakuja walikuepo kijiweni, mimi Jasmini tukazama ndani kwangu kudet na hawa coloured si kitu kigeni fry catcher na mahotelia wanajua watoto wa kizungu walivyopinda kwa hiyo haikua bigdeal kwangu kutoka na demu wa kimanga, MASAA SITA MAGUMU KATIKA MAISHA YANGU baada ya mashamu shamu ya mapenzi tukaanza round ya kwanza ile namaliza tu nikachukua simu ili nicheki kun sms ziliingia nikawa nimpa kisogo sikua na wasiwasi niko kwangu ile nageuka nilishangaa kitandani hakua yule Jasmini lilikua ni sketon kwenye mifupa linatoa miale kama cheche hivi na nywele zake zinasimama wima nikimbia hadimlangoni ajabu mlango haukuweza funguka lakini alikua anaongea lugha zingine nizizozifahamu ila kwa kunigombeza pia alikua anabadilika kwa sura tatu moja alikua ananyanyua nywele zake na meno mawili mbele yalikua yanajitokeza kwa nje alitisha sikua na ujasiri wa kumtizama nilipata shida sikua hata na uwezo wa kuomba msaada nje au kupiga kelele sauti haukutoka, baada ya kutoka nilijaribu kuwaelezea wenzangu kilichontokea hawakuamini basi nilikaa miezi kadhaa nilirudi nyumbani kufanyiwa matambiko nikalejea tena mzigoni coz nilikua tayari nimejijenga zenji ule usumbufu wa jasmini nilikua nimeshaanza kuusahau ila mashrti alionipa nioe kwa mda nilipuuzia baada ya kupata ushauri kwa watu wenye utaalamu wa hawa viumbe kua majini yako chini yetu ukijitambua jini si lolote kwako hivyo nilipuuza nikaoa siku ya kwanza baada tu kufika na mke wangu wangu Jasmini akatokea japo nilikua ktk wakati mgumu kumwambia mke wangu abc -xyz za jasmin tulijikuta tumelala katkati ya mji maeneo ya darajani tulienda kijihifadha katika kanisa la anglikana mnazi moja hadi asubuhi nikaona hamna haja ya kuendelea kumficha mke wangu juu ya Jasmini, NINI KILIFUATA STAY TUNED CIAO wandugu wapendwa jana niliishia hapa kuwaletia masahibu yaliyonikumba maisha japo wengi wanona kama comed hanikatishi tamaa kuwasimulia hadi mwisho maisha yakaendelea na nilimweza mke wangu kuanza mwanzo hadi wa kisa chote nashukuru alikua mwelewa na alisimama na mimi kama mke Clinton katika ile kesi yake na Monica lewsky any way alikua mtu wa idada sana aliekua mtu wa maombi hapa kuna ushauri mwingi sana tulipewa wengine walitushauri tumalize kwa njia za waganga wengine walitushauri tuendelee na maombi tukaamua kufuata maombi nakumbuka tukaingia kwenye maombi ya siku saba na kufunga na jamaa zetu pale kanisani mnazi moja anglikana ile tunafika tu siku ya tatu tu vita ikaanza tukiwa tumelala na mke wangu usiku karibu na kupambazuka tulijikuta kitanda kinayumba sana kama kinaelea kwenye maji nilijua labda naskia mimi tu mara mwenzangu akaniamsha tulikua kweli tunaele baharini katika pwani ya bububu tuliondolewa kwa msaada wa wavuvi tukawapelekea wanamaombi wenzetu nakumbuka kuna mama moja alitutia moyo kua sasa kazi imeanza hakuna kurudi nyuma wala kujisalimisha nashukuru kitu kingine mwanamke niliekuanae naweza ni jasiri sana alisaport kwa kila hali niliyokua napitia na kinitia moyo na maisha yakaendelea na vitisho vya Jasmini taratibu vikaanza kupungua mara akawa ananitokea kwenye ndoto tu ashukuriwe MUNGU asieshindwa na chochote katika ile vita nniliibuka mshindi na kutukana na basement ya maombi niliiyoianzisha baada kukumbwa na matatizo leo huwa sitishwi kirahisi na hizi negative force pia nakagundua kitu kimoja wengi wanaojaza makanisa leo sio wote ni wale waliowahi kupingwa kiboko na shetani au kukumbana namasahibu kimbilio la waliokata tamaa ni kwa YESU japo nilifunguliwa vifungo vyote vya ibilisi mwovu shetani nilishauriwa nihame zanzibar kuepuka kutumia nguvu kubwa katika maombi sasa naishi maisha ya raha mustarehe na familia yangu heri wanaoamini kwa kusikia kuliko wanaosubiri kuona,BYE BYE
 
Mbona hujamalizia alipokutawadha kwa kutumia jiti, nyie watu wa bara mna matatizo sana/
 
Wataalamu wanasema jini akijibadili kuwa mwanadamu hudumu kwa masaa yasiyozidi mawili tuu katika hali ile ya ubinadamu, baada ya masaa mawili hubadilika na kurudi hali yake ya kijini. so hapo anakuwa hawezi tena kukaa na mwanadamu.
Mnapotunga hadithi ni vizuri mkawa mnafahamu facts kama hizi.
 
jamani mnatutisha na story za majini usiku usiku. dah!!!
 
Da hadithi hizo za kizenji za kawaida ..tukisha kula orojo .
Tunajifurahisha..tu...but mambo hayo zenji saivi hamna yamepotea kabisa..








..
 
we nawe eliminate mchanganyiko inachanga hadi akili si kosa lako ni walokulea
 
Nenda kafanyiwe maombi hayo ni maagano tayari,Nenda kwenye makanisa ya kiroho ukafanyiwe deliverance haraka.Tayari umekuwa na connection na milango ya giza katika maisha yako.Wewe ndio unayeelewa ulichokiona na usifikiri kila mtu atakuelewa nenda kafanyiwe maombi.
 
pole sana kuna watu umu kazi yao kukandia tu mara tamthilia hiyo.aya mambo yanatokea kila mtu ana matatizo yake tukishindwa kutoa ushauri tukae kimya sio kukandia uyu jamaa anaitaj ushauri na maombi pia
 
hebu ipange vema kwa paragraph isomeke
hapa tunaumizana tu macho.
 
Back
Top Bottom