Nilijiita waziri mkuu kidogo waniue | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nilijiita waziri mkuu kidogo waniue

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Nov 26, 2009.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  NILIJIITA WAZIRI MKUU KIDOGO WANIUE
  Mkuu wa nchi moja alikwenda kutembelea hospitali ya wagonjwa wa akili ili kujua maendeleo na huduma wazipatazo, siku hiyo wendawazimu wenye kichaa kikali walifungiwa na kuachwa wenye nafuu. Basi Mkuu wa nchi alipofika hospitalini hapo alipokelewa na mganga Mkuu kisha alizungushwa katika wodi za wagonjwa wa akili.

  Wodi ya kwanza ilikuwa ya igonjwa wenye afadhari ambao waliachwa ili kumpokea muheshimiwa hata kuzungumza nae mawili matatu.
  Mgonjwa wa kwanza aliyekutana naye alimuuliza mheshimiwa...

  Mw: Ndugu yangu mbona umeongozana na watu wengi inaonekana wewe ni kichaa mkubwa wamesahau kukufunga kamba, mimi nilipoletwa hapa nililetwa na mtu mmoja lakini wewe umeletwa na watu wengi na polisi wenye siraha kichaa chako ni kikubwa.”
  Rais: Mimi ni Rais wa nchi hii, alimnongÕoneza sikioni.

  Mw: Tena usirudie kujiita Rais mimi nilipokuja hapa nilijiita Waziri Mkuu walinipiga nusra ya kuniua, wewe kujiita Rais watakuua kabisa.” Kichaa naye alimnongÕoneza Rais.
  Mheshimiwa Rais ilibidi amalize ziara yake pale pale kwa kufikiria mwenye afadhali yuko hivyo, je kichaa kabisa atakuwaje.
   
Loading...