Niliiba mume wa rafiki yangu, alichonifanya siwezi sahau

Feb 9, 2016
74
153
Tulipotoka chuo mwanzoni mwa miaka ya 2000 mimi na rafiki yangu kipenzi tulipata kazi nzuri na yenye kulipa vizuri sana, kazi hiyo tulitafutiwa na Mchumba wa huyo shosti wangu, tulipomaliza probation tu, rafiki yangu na Mchumba wake wakafunga ndoa rasmi.

Baada ya kama miaka 3 hivi, mimi na yule shemeji yangu tukaanzisha uhusiano usiofaa kwa siri bila mwenye mali kujua, baadae yule bwana akaanzisha fujo nyumbani kwake ili waachane, rafiki yangu akaja kugundua kuwa mimi ndiye mbaya wake, urafiki ukaishia hapo na akalipeleka suala hilo hadi kazini lakini akajibiwa wao hawahusiki na masuala hayo,tukawa hatusalimiani tunapishana tu hapo kazini.

Yule bwana akahamia kwangu kabisa kupika na kupakua wakati akishughulikia talaka, mkewe aliniambia wazi kuwa atachonifanya sitasahau na nitarudi kwake kupiga magoti, sikumjali sana.

Baada ya muda flani nikaanza kuhisi kama vile nina kipele kwenye ulimi chenye maumivu makali, siku zilivyozidi ulimi wote ukaanza kuvimba na kujaa mdomoni, hospital walinipa antibiotics na sindano bila mafanikio, after 3 weeks nilikua nimelazwa maana ulimi umevimba na umekua mwekundu, unauma hakuna mfano na siwezi kuongea, maana umejaa mdomo mzima kama mtu anae puliza moto, nikapelekwa Ocean road lakini haikua kansa, nikalazwa Muhimbili miezi 2 bila nafuu, nikawa mtu wa nyumbani na hospital, nilikua nakula kwa mipira, mdomo haufunguki wala kuongea siwezi achilia mbali kula.

Tulienda kwa waganga mbali mbali bila mafanikio ila wote walisema ni rafiki yangu ndie mhusika isipokua uwezo wa kutegua ndio hawakua nao, wazazi wangu walienda kumuomba msamaha lakini alidai sio yeye na hajui chochote na alipoona usumbufu umezidi akaacha kazi na ndugu zangu hawakujua tena pa kumpata, miezi sita ilipokatika kazini wakaniletea barua ya termination due to sickness yule bwana akanikimbia pia nikabaki na wazazi na ndugu wakiniuguza nyumbani, wakisubiri siku yangu ifike, maana nilikua na homa kali wakati wote isiyoshuka hata kwa dawa.

Siku moja nikawa nimelala kwenye godoro chini ya mti wa kimvuli, walipenda kuniwekea godoro chini ya huo mti nashinda hapo kutwa nzima, nikawa nimepitiwa na usingizi nikasikia kama sauti inaniambia inua ulimi wako kuna kitu kiko chini ya ulimi ukikitoa unapona, nilipoamka nikaanza kuwaza sana kuhusu sauti ile, ndoto si ndoto, sauti si sauti, wazo si wazo, lakini baadae ngoja nilifanyie kazi jambo hilo.

Sijui ni kwa ujinga wangu au nini sielewi, nikainuka na kwenda kuchukua mswaki, watu walishangaa huo mswaki nitapigaje maana nina karibu miezi nane bila kupiga mswaki ulimi umejaa mdomo mzima na unauma vibaya, nikajikaza na kuingiza vidole mdomoni na kuinua ulimi juu kwa nguvu huku nikilia kwa maumivu makali, wakaja kunizuia wakifikiri nimechanganyikiwa, tukawa tunashindana, haraka nikaupachika mswaki chini ya ulimi, nikagusa kitu kigumu, hicho hicho nikaanza kukivuta nje huku nalia kwa maumivu na damu na usaha vinatoka kama maji, maana ule uvimbe ulipasuka, sikuacha nikaendelea kuvuta hicho kitu Chini ya ulimi kwa kutumia mswaki hadi kukitoa nje, watu wote walipigwa na butwaa kuona kile kitu ni hirizi nyeusi imeanguka mbele yangu, na maumivu yote yakaisha hapo hapo, ulimi ukanyauka wote na kurudi kawaida, homa ikakata, nikaanza kuongea hapo hapo, mama yangu alilia kama mtoto mdogo, tulilia wote huku tukiwa tumekumbatiana.

Wakazoa ile hirizi na kwenda kuichoma, baada ya siku tano hivi vidonda vya kwenye ulimi vyote vilipona, nikawa mzima kabisa, nikawa nakula kama vile nafukukuzwa, nikaanza upya kutafuta kazi na nikafanikiwa, ni miaka mingi imepita tangu tukio hili, sijawahi kuonana na huyo rafiki yangu tena, nimemtafuta sana ili nimwombe msamaha bila mafanikio.

Nimeolewa na nina familia yangu, nilimvunjia rafiki yangu ndoa yake akiwa na mtoto mchanga wa miezi saba, ndo maana aliumia sana, namshukuru sana Mungu kwa ukuu wake, najua sio ujanja wangu kwamba nilipona, huenda Mungu alimtumia huyu rafiki yangu kunisamehe hivyo akaenda kutengua huko alikonifunga.

Popote ulipo na kama umesoma maelezo haya najua utafahamu kuwa ni mimi nisamehe kwa yote yaliyotokea kati yetu, ni shetani alinitumia kufanya yale yote, nimekutafuta kwa miaka mingi bila mafanikio, kama upo JF na umepita hapa Pleas find a place in your heart to forgive me.
 
Pole sana japo ulivuna ulichopanda kabisa na shukuru Mungu sana na endelea kumtafuta rafiki ako kwani yawezekana umemwaribia maisha yake completely... Na iwe funzo kwa wasichana wengine wakora wenye urafiki wa kinafki na kutamani waume wa marafiki zao..How comes unamvulia mume wa rafiki yako kabisa pichu banaa..Hata kama yeye ndo amekuanza sasa kisa mimi natabia za kijinga na wewe rafiki wa wife wangu unikubalie tu nitimize malengo yangu...Hapana ukinikatalia sintoweza kukubaki na utakuwa umenipona mimi na ndoa yangu..
 
Kama umekiri ulifanya kosa na kutubu,, jua hata mungu amepokea tubu yako na ndio maana ulipona na kuwa mzima wa afya, zidi kuomba mungu kuna siku utakutana na rafiki yako na kuomba msamaha mbele yake pia atakuelewa na kukusamehe.. ama hakika mungu ni mwema mbele yako
 
Mh...haya maisha haya, kama ni kweli,Pole yake kwa hayo yote uliyomfanyia.
 
Ubinadamu kazi. Natumai umejifunza. mke/Mme wa mtu anauma sana sikia tu kwa wengine.

Hilo ni funzo lako.
 
Mshana Jr njoo si huwa wanasema ety zile thread zako huwa ni za kufikirikaaa
 
Duuuh

Touching..Pole sana....

Ni funzo kubwa...Kweli ulimuumiza sana mwenzako....hakustahili

ila sisi wanaume sometimes ni wapumbavu sana
 
Back
Top Bottom