Niliiba gari nyumbani nikiwa form 2 nikala mzinga

Bora yako wewe mimi nilivamia karandinga la askari magereza wakajua ni ambush nataka kuwatorosha wafungwa nilizungukwa na askari zaidi ya 30 wakaniweka mtu kati nilipigwa mabanzi na mateke mpaka kituoni niliia siku nzima non stop mpaka sauti ikakauka sitokuja sahau.
 
IMG_9049.jpg
 
Binti yako ana passion na magari mfundishe kuendesha kidogo kidogo..na kama alisemaa atachomoka na hilo ndinga basi ipo siku mkijisahau atabeba funguo ajaribu na kama hajui anaweza kula mzinga ikawa majanga

Ukimfundisha mapema kuna faida nyingi tu na akianza kujua saiv,mpaka anafika form four atakua dereva mzuri tu


Nakumbuka kuna wenzangu watatu nilikua nao shule kwao kila mmoja gari lipo ila wanakaziwa kuendesha kisa bado wanafunzi halafu kila siku mimi nawapa story ninavyopiga misele na ndinga la nyumbani wakawa wanatamani kweli kuendesha

Wawili kati yao walijaribu kuiba gari nyumbani kwao lakini wakala mzinga kwa sababu hawajui kuendesha

Mmoja aliwasha gari akaweka reverse akakanyaga wese nyingi moja kwa moja mpaka getini akazoa geti la nyumbani kwao

Huyu mwingine nae siku kavizia kwao wazazi wake wamesafiri kabaki yeye na house girl tu.. kwao kuna gari mbili sasa hiyo siku zilikua zimepaki kwa kufuatana moja mbele moja nyuma lakini kulikua na nafasi ya kama mita tano kati ya gari ya mbele na ya nyuma yeye akaingia gari iliyokua nyuma akawasha chuma na kwenye kutoka ilibidi arudi reverse...sasa yeye akaweka d badala ya reverse akakanyaga mafuta anashtuka gari inaenda mbele badala ya nyuma na alivoona anakaribia kugonga gari iliyokua mbele akapata wenge badala ya kukanyaga breki akakanyaga wese akapasua gari zote mbili
Nilishamuahidi kumpeleka veta kujifunza akimaliza f4,Ili awe na cheti kabisa.
 
Back
Top Bottom