Nilichukua kadi ya CCM kwa Hofu na hali ilivyokuwa awamu ya 5

Pearce

JF-Expert Member
Dec 15, 2018
577
1,381
Moja za awamu iliyokuwa ya kibabe, ilikuwa fashion Viongozi kutisha wananchi wao.

Ajira kwa vijana ilikua changamoto sana.

Labda kwa mazingira ya kutiwa hofu na unawezwa fanywa lolote na magenge ya wasiojulikana na style za Viongozi kama kina Sabaya.

Ajabu wengi nilosoma nao ambao walikuwa wakikesha kusifia mitandaoni walitoboa.

Si kweli CCM ilipata mafanikio ya kuvuna watu awamu iliopita sababu walipenda wengi sababu ya hofu na chuki zilizoshamiri na siasa za kukomesha wenye mawazo tofauti na sera za kiongozi wa awamu iliopita.

Hivyo ni bomu ambalo CCM walibeba kuwa na wanachama wasiona Mapenzi ya kweli wenye uchungu na hasira na chama lakini wamijificha humo.

NB:- baada tulioyaona awamu iliopita hivi Nani atakuwa tayari kuwapigia Kura majimboni aina ya Viongozi PolePole, Ndugai na walionesha kiburi na dharau kwa wananchi sababu walitumania siasa za kibabe za awamu iliopita.

Watavuka kweli hata ndani tu kwa Kura za maoni ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom