Nilichoshuhudia ndani ya treni ya Ubungo

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,900
2,394
Kwanza napenda kutoa pongezi za dhati kwa menejimenti nzima inayoratibu safari ya treni hii ya kutoka Stesheni na kuelekea Ubungo.

Tren hii ni mkombozi kwa wananchi wengi wa mkoa wa Dar es Salaam.Hii ndio ilikuwa suluhu kwa usafiri wa ndani ya jiji la Dar es Salaam kwani haina longolongo la foleni na kupotezeana muda.

Kuna siku nilipanda hii treni kutokea Mabibo relini na kuelekea Stesheni.Nilichogundua kwa siku hiyo, kuna baadhi ya wakatisha tiketi sio waaminifu kwani walikuwa wanachukua pesa za abiria bila kuwapa tiketi haswa wale wanaoshuka njiani. Pia mkatisha tiketi hachukui nauli mpaka treni ikikaribia kufika kisha anachukua nauli na tiketi hakupi, hapo treni inakuwa ishaingia eneo la Stesheni.

Kwa hesabu zangu za haraka haraka zile hela zinakuwa zao haziingii kwenye akaunti ya shirika kwani pale kila mkatisha tiket ana kitabu chake cha tiketi na wanapeleka hesabu kulingana na jinsi walivyouza tiketi. Kwa maana hiyo kama hakutoa tiketi hiyo hesabu imeingia mfukoni mwake.

Hii ni kuleta hasara kwa Shirika kwani litaonekana libajiendesha kihasara na hivyo kusitishwa kwa hiyo ruti na kuleta usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.

Rai yangu kwa wanaotumia huo usafiri, hata kama unapanda Ubungo na kushukia Mabibo relini dai tiketi ili kuliwezesha Shirika kupata mapato yatakayosaidia kuwepo kwa hiyo treni inayofanya safari hiyo na ikibidi iongezwe ruti mpaka Mbezi na sehem mbalimbali za jiji hili la Dar es Salaam.

Nawasilisha.
 
Usimamizi mbovu,ndio maana wanaona inaenda kwa hasara wakati kuna wapiga deal kibaoo
Acha tusubiri mabasi ya mwendo kasi nayo,maana wameishaanza kuyavunjavunja
 
Kwanza napenda kutoa pongezi za dhati kwa menejimenti nzima inayoratibu safari ya treni hii ya kutoka Stesheni na kuelekea Ubungo.

Tren hii ni mkombozi kwa wananchi wengi wa mkoa wa Dar es Salaam.Hii ndio ilikuwa suluhu kwa usafiri wa ndani ya jiji la Dar es Salaam kwani haina longolongo la foleni na kupotezeana muda.

Kuna siku nilipanda hii treni kutokea Mabibo relini na kuelekea Stesheni.Nilichogundua kwa siku hiyo, kuna baadhi ya wakatisha tiketi sio waaminifu kwani walikuwa wanachukua pesa za abiria bila kuwapa tiketi haswa wale wanaoshuka njiani. Pia mkatisha tiketi hachukui nauli mpaka treni ikikaribia kufika kisha anachukua nauli na tiketi hakupi, hapo treni inakuwa ishaingia eneo la Stesheni.

Kwa hesabu zangu za haraka haraka zile hela zinakuwa zao haziingii kwenye akaunti ya shirika kwani pale kila mkatisha tiket ana kitabu chake cha tiketi na wanapeleka hesabu kulingana na jinsi walivyouza tiketi. Kwa maana hiyo kama hakutoa tiketi hiyo hesabu imeingia mfukoni mwake.

Hii ni kuleta hasara kwa Shirika kwani litaonekana libajiendesha kihasara na hivyo kusitishwa kwa hiyo ruti na kuleta usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.

Rai yangu kwa wanaotumia huo usafiri, hata kama unapanda Ubungo na kushukia Mabibo relini dai tiketi ili kuliwezesha Shirika kupata mapato yatakayosaidia kuwepo kwa hiyo treni inayofanya safari hiyo na ikibidi iongezwe ruti mpaka Mbezi na sehem mbalimbali za jiji hili la Dar es Salaam.

Nawasilisha.
Sasa utarogwa fisuri...
 
Hapo wanaopaswa kuwajibishwa ni management kwanini hawaweki mitego ya kuwakamata hao wezi....implication ya hilo ni kuwa they eat together na hao wakatisha ticket
 
Walifanyie kazi hili! Tena haraka iwezekanavyo, simply wafunge camera na kuzireviw kila Sikh!

Camera hata 20 hazifiki na gharama yake plus database nzima haizidi hata 5M na itaondoa ujinga wa namna hiyo moja kwa moja
 
Kwa nini wasitumie na wao mashine za EFD . Kwa wale wa zamani kama mie, mtakumbuka ule ukatishaji wa tiketi za kwenye mabasi ya UDA. Hakuna longolongo na hesabu lazima ijulikane!
 
Back
Top Bottom