Nilichosema bungeni kuhusu mpango wa taifa (2011-2016) na Bajeti (2011/2012)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza kuhusu nishati ya gesi ambayo ingetumika majumbani kama LPG, gesi hii kama watu wangeitumia ingepunguza bei ya nishati nyingine. Tunazungumzia kuhusu gesi kutumika kwenye magari ambayo ingeshusha nusu ya nauli Dar es Salaam au nusu ya gharama. Investment kwenye gesi na miundombinu ya gesi siyo bomba tu lile na mitandao ya gesi, vituo vya kujazia mafuta ya gesi na kadhalika ni kama vile imeachiwa TPDC tu peke yake na hiyo retention ya 50% kama tunataka kupunguza gharama za maisha lazima pamoja na kupunguza kodi kwenye mafuta twende kuwekeza kwa nguvu sana kwenye nishati mbadala.
ccm wanafumbia macho hadi vitu ambavyo ni simple
 
Excellent work sir...but who is going to read all book on the internet....can you make story shot mheshimiwa....?

Make it short yourself....mboana watu manakuwa wavivu wa kusoma......kila kitu mpewe summary...acheni uvivu
 
Jaribu kupunguza uvivu wa kusoma....hii ni kutoka kwenye hansards....hazina kusamaraizi

Mkuu usimlaumu,wengine wavivu wa kusoma kama huyu. Then ndo hawa hawa wanaorukia mijadala bila kujua inatoka wapi.
 
Lakini cha muhimu zaidi kwangu ni pale unapeleza wazi wazi ni kitu gani wananchi wa Ubungo wamekutama ukasimamie Bungeni.

Lazima uelewe kuwa mbunge hawakilishi wapiga kura wake tu....la hasha anawakilisha watanzania wengine pia....ikiwa kila mbunge atajadili yale ya jimboni kwake tu nadhani maana ya bunge itapotea
 
tunazungumza kuhusu nishati ya gesi ambayo ingetumika majumbani kama

hapo tuko pamojo ndg mbunge nchi zote zilizoendela zinatumia gesi majumbani maana umeme hauwezi kukidhimaitaji kama nchi inakua
Hata sisi tunatumia gesi ya kutoka Uarabuni kwa shs 50,000 kwa mtungi licha ya kuwa Mungu ametupa neema ya gesi kibao. Lini nchi hii itapata viongozi wenye upeo wa kuziona rasilimali tulizonazo na kupanga kuzitumia kumaliza shida zetu na sio kumaliza shida za wazungu.
 
Mkuu Mnyika nakuamini mkuu plz tuonee huruma sisi wanyonge tunavyokamuliwa kodi zetu je unaweza kupeleka hoja binafsi ya kuondoa kitu inaitwa viti maalumu bungeni? kwani huu ni mzigo kwa taifa na walipakodi. Asante sana na ni matumaini yangu utalifanyia kazi.
 
John Mnyika,

Hoja zako ni Nzuri sana,haya ndiyo matunda ya kuwa na wabunge vijana bungeni ,tena sio vijana tu...vijana wenye uwezo.Atleast unaziba Ombwe lililoonyeshwa na baadhi ya vijana wenzao waliokuwa wanapwaya katika Hoja.

Suala la viwanda halikwepeki.Tatizo la ajira kwa vijana litapunguzwa kwa kuwekeza zaidi kwenye kilimo sambamba na viwanda.At the same time suala la nishati ni injini katika hilo.Ni lazima tuweke mkakati wa kupunguza import na kuongeza export at the same time unaongeza ajira na living standard.Nitakuja kuchangia vizuri kwa mtiririko baadae.Otherwise,Keep It up Comrade!
 
Mnyika hatuna umeme tangazeni maandamano.tunakufa aiseee
Hivi wandugu ni nani anayepanga vipaumbele katika nchi? Kwa mawazo yangu hakuna cha kupanga kuhusu maandeleo kama nishati muhimu haipo. Hivi ninavyoaandika ni mwendo wa majenereta na maana yake hicho kidogo tunapeleka Uarabuni kwa wenye mafuta. Biashara nyinajgi mfano ya samaki ziko hatarini. Hivi kweli nchi hii tunategemea maendeleo yatoke wapi kwa hali kama hii???Natamani kulia kwani sioni hata uongozi magufuli style wa kututoa hapa tulipo...tatazo lililopo mbona ni kubwa sana na sioni kama wahusika wanaona hivyo??? Nakosa hata cha kusema....Maandamano ya ndio njia tutakayoweza kuitumia kutoa sauti yetu..Senegal wameshaandamano kwenye hili la umeme sisi lini???
 
Barua ndefu kama hii. Ndugu mnyika tuombee fungu la kuchonga barabara za jimbo letu hasa ile ya kibangu-jeshini, ile inayoanzia pale river side. Blah blah nyingine baadae
 
Baadhi yetu hatupendi kusoma na kujitafakarisha, hongera Mnyika pole pole wavivu wa kusoma watapata nafasi ya kuvipa kazi vichwa vyao na kuwajibika ipasavyo
 
Asante Mh John! Food of thought

Lakini mbona hii simu yako huwa haipatikani?

0784222222,
 
Hivi wandugu ni nani anayepanga vipaumbele katika nchi? Kwa mawazo yangu hakuna cha kupanga kuhusu maandeleo kama nishati muhimu haipo. Hivi ninavyoaandika ni mwendo wa majenereta na maana yake hicho kidogo tunapeleka Uarabuni kwa wenye mafuta. Biashara nyinajgi mfano ya samaki ziko hatarini. Hivi kweli nchi hii tunategemea maendeleo yatoke wapi kwa hali kama hii???Natamani kulia kwani sioni hata uongozi magufuli style wa kututoa hapa tulipo...tatazo lililopo mbona ni kubwa sana na sioni kama wahusika wanaona hivyo??? Nakosa hata cha kusema....Maandamano ya ndio njia tutakayoweza kuitumia kutoa sauti yetu..Senegal wameshaandamano kwenye hili la umeme sisi lini???
Kuna member aliweka bandiko akasema ukiwa serious sana na mambo ya nchi hii unaweza ukafa kwa ungonjwa wa moyo...maana hatuelewekie tuna endawapi, tunataka nini, tuanze na nini mara kilimo kwanza, kwenye budget wameyapa kipaumbele mambo mengine...
 
big up Mnyika, kwa kweli tulichoshuhudia ubungo ni mabomba kupitishwa ila maji imebaki historia.
 
Back
Top Bottom