Nilichokishuhudia leo...!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,914
Dunia ina mambo........
Na mengine ni yakusikia tu............

Kuna jamaa yangu alikuwa anatafuta nyumba ya kuishi[kupanga],alinijulisha hili jambo na tulisaidiana kutafuta kuepuka usumbufu wa madalali na gharama zao

Hatimae wiki moja iliyopita alifanikiwa kupata nyumba eneo la Nyakato Buzuruga,hapa jijini Mwanza,na alihamia siku hiyo hiyo.Ilikuwa ni nyumba nzuri sana na iko kwenye hali nzuri tu

Siku 4 baada ya kuhamia yeye na mkewe na watoto wao wawili jamaa alinipigia simu akiniomba jioni baada ya mihangaiko yetu niende nyumbani kwake kuna mambo hayaelewi kidogo kuhusiana na nyumba ile

Jioni nilikwenda na aliniambia kuwa mara nyingi nyakati za usiku wakati amelala na mkewe huwa wanarushiwa matonge ya ugali kitandani na wakati mwingine kumwagiwa mchanga,na kila yalipokuwa yanatokea hayoi matukio huwa anawasha taa ili kuona labda ndani kuna mtu lakini huwa kunakuwa hakuna tofauti ya yeye na mkewe,na akirudi tena yanarudia yaleyale,na kali zaidi usiku wa kuamkia siku niliyokwenda mkewe aliingiliwa kingono na mtu ambae alikuwa hamuoni na alipojaribu kupiga kelele ili mumewe aamke alikuwa anashindwa,hivyo alikuwa anaomba nimshauri cha kufanya

Nilikaa kimya kwanza nikitafakari haya aliyoniambia,baada ya kimya cha kama dakika 2 hivi nilimuuliza kuhusu lolote analojua kuhusiana na uchawi akaniambia hana analojua zaidi za kusikia story tu mitaani,pia nilimuuliza kuhusu uhalisi wa hayo na alinihakikishia ni kweli kabisa,kiukweli nilishindwa kukubali au kuataa na nilimuambia anipe muda wa kutafakari kidogo

Ndipo leo nikiwa nipo nyumbani na kwakuwa leo sijaenda kwenye shughuli zangu kwa kuwa sijisikii vyema na wakati huohuo sijui cha kumwambia huyu rafiki yangu kutokana na mambo yake kutokuwa na ushahidi na uhakika alinipigia simu niende kumsaidia kupaki vitu kwenye gari kwani anahama nyumba ile.[alikuwa anajua kuhusu kuwepo kwangu home leo]

Nilistuka kidogo,lakini nikajisemea wacha niende nikamuulize kulikoni hukohuko.

Nilifika na kumkuta mkewe pamoja na wanae wakiwa katika harakati hizo za kuhama,nikaamua nitamuuliza baada ya kumaliza harakati hizo maana inaonekana kama kuna jambo kubwa sana lililomfanya ahame ghafla hivyo

Ndipo wakati wa kuhamisha vitu hivyo ndipo kilipotokea kioja kilichonistua sana.
Tulikuwa chumbani tukifungua kitanda mimi na huyu rafiki yangu ili kipakiwe kwenye gari,mule ndani kulikuwa na sofa la kumtosha mtu mmoja na juu yake lilikuwa limewekwa begi kubwa la nguo na mule ndani hakukuwa na mtu zaidi ya mimi na yule rafiki yangu tuliekuwa tumezama kwenye kukifungua kitanda na huku akiniambia baadhi ya vituko vya pale

Unajua kuna vitu mtu huwezi kumuambia na mtu akakuelewa labda tu awe amevishuhudia,na ndio kama hiki changu,kwani ghafla tulisikia harufu ya kitu kinaungua na wote wawili mimi na na rafiki yangu huyu tulitazamana na kisha tukageukia kule tulokokuwa tunahisi kunaungua na ndipo tulipoona moto ukiwaka pale lilipokuwa limewekwa lile begi,yaani kwenye sofa

Nilipigwa pumbuwazi kwanza kwa sababu sofa lile halikuwa mlangoni tungesema labda kuna mtu aliingia kwa kificho na akawasha moto kisha kutoweka wakati sisi tukiwa tumezama kwenye kufungua kitanda,lakini sivyo,sofa lilikuwa nyuma yetu na mlango ulikuwa mbele yetu yaani mtu ili aingie ni lazima tungemuona tu

Ilibidi tuanzishe harakati za kuuzima ule moto lakini cha kushangaza ilionekana ule moto ulikuwa umewaka muda mrefu sana bila sisi kusikia na ulikuwa umeshaliunguza lile begi robo tatu na moto ulikuwa umeanza kushika kwenye sofa

Kwa taharuki tuliuzima ule moto na kufanikiwa na tulilitoa nje lile sofa huku kila mmoja akiwa na maswali mengi sana kichwani

Tulishindwa hata kuuliza maana mazingira tu ya kuwaka moto ule yalifanya tukose ujasiri wa kuuliza kama kuna mtu aliingia mule ndani na kuuwasha ule moto

Yaani mtu aingie ndani na kuwasha moto mpaka begi liungue uwe hujasikia?Ni ngumu sana kueleweka,mkewe rafiki yangu alipouliza kulikoni begi limeungua na sofa tulimwambia tutamueleza kazi ya kuhama ikiisha!

Tulimaliza na tumeahidiana na rafiki yangu kuwa tutakutana kesho jioni ili tuongee zaidi kwani nyumba aliyokuwa anahamia ilitakiwa aifanyie marekebisho kidogo hivyo alihitaji muda kwaajili ya hilo

Nilirudi nyumbani majira ya saa 6 hivi huku nikiwa na maswali mengi sana kuhusiana na ule moto,hadi sasa sijui ni nani aliuwasha na uliwakaje na kwanini

Matukio haya nilikuwa nasimuliwa tu na nilikuwa nahisi labda mengine ni story tu ila leo nimeshuhudia live mimi mwenyewe,sina majibu hadi sasa!

Sina ham kwakweli!

Kuna haja ya kuwa makini na hizi nyumba tunazoishi
Unaweza kwenda kuishi mahali pa ajabu sana!
 
Mmh!! Poleni!! Kuna vitu huwa ni vigumu kuamini kwakweli!! Lakn 2naambiwa vipo !! Dunia ina mengi ati.
 
Kaka Eiyer kuna watu wanaitwa wenye nyumba simply kwa kuwa walitangulia kufika mjini ila bila hata kugoogle ni wazi kabisa kuna namna zao wanajua ambazo wametumia kujipatia fedha/mali zilizopelekea kujenga nyumba zinzzowafanya wawe tittled wenye nyuma!

Makafara yametembea sana na manuizo ya ajabu ajabu kwenye nyumba tunazoishi mjini! Just imagine mtu anaishi kwenye banda lisilopigwa walau plaster nje ya mji ilihali mjini ana flats alizojaza wapangaji,kwa nini usitazame mafanikio yake kwa jicho la tatu!

Binafsi nimejiwekea dhamiri juu ya hizi nyumba za kununua ambazo hujui waliojenga waliweka maagano gani na mizimu(naexclude wanaojenga kwa minajili ya real estate) Ni mara mia kujitafutia kajisehemu kako ukajenga kwa kuunga unga huku ukiomba yasikufike makuu kuliko kuingia kwenye haya majanga!
 
Last edited by a moderator:
mwanza noma bugando getini wanauza maji waliyooshea maiti,tena ya mtoto mchanga bei juuu poleni jamani mmepata fundisho kabla kuhamia nyumba za kupanga muwe mnaulizia majirani kama nyumba ipo poa ama haya yanawakuta wengi sana nyumba analala siku moja mwenyewe anahama bila kudai kodi yake
 
Mhh hiyo kali aisee..............sasa vitu vilivyokuwa katika begi havijaungua!!!!!!!!!!!!!
 
Mie kuna rafiki yangu hapa hapa daslama mtoto maeneo Tangi bovu

nae amewahi kunihadithia stori kama hizi hizi.....mtoto wake alifariki

baada ya tukio ndio akaambiwa hiyo nyumba mbona Vifo vya watoto

wachanga tena vyenye utata ni kawaida na wote ndio kinachowahamisha!!!!!!!!!

na hata namna mtoto wake alivyofariki tumebakia tunasema tumwachie tu Mungu maana NI UTATA mtupu...
 
Last edited by a moderator:

Yaani siku hizi kuna umuhimu sana wa kuwa na wakili na mganga wakati unanunua nyuma ........lol!!!!!!!!!!
 

Hata huyu jamaa yangu hakudai kodi
Unadhani ujasiri wa kudai kodi utautoa wapi?


Halafu unadhani ni Bugando tu?
Hii makitu ya kuuza maji ya maiti niliwahi kukutana nayo mahili kwingi sana na mikoa tofauti tofauti!
 

Yaani hivi vituko ni vingi sana
Unaweza kuhamia kisha ukaambiwa wanaume humo huliwa kibog sijui inakuwaje aisee!!!!!!
 
huu tuendelee kuuita UPOLE wa Watanzania, tukiuita UJUHA hapatakalika.
Nchi nyingine ujinga namna hii ulikwisha miaka ya 1800 baada ya kuhakikisha kwamba kila anayeleta janga anapata STAHILI yake.
 
huu tuendelee kuuita UPOLE wa Watanzania, tukiuita UJUHA hapatakalika.
Nchi nyingine ujinga namna hii ulikwisha miaka ya 1800 baada ya kuhakikisha kwamba kila anayeleta janga anapata STAHILI yake.

Mkuu ni wapi huko ambako hii kitu waliimaliza kwa style hiyo?
 
sijamaliza kusoma... Ila nahisi huyo jamaa yako na mkewe...,mmoja kati yao atakua mwanga.
 
Duuh,..Mwenyezimungu atuepushie mbali hayo mambo,...hizo ishu zipo,wengi zimewakuta. Watu wanasamehe hadi fenicha ili mradi asirudi tu kwenye nyumba.
 
Yaani siku hizi kuna umuhimu sana wa kuwa na wakili na mganga wakati unanunua nyuma ........lol!!!!!!!!!!

Na zile za kupanga kiwepo kipengele cha kuallow wapangaji wawe wanafanya mambo yao kabla ya kuhamia. Kwa Wakristu watakase kwa damu ya Yesu,Muslims wasome dua na wale wenzangu na mimi tuende na kina 'Babu Nyuki' tukate vichwa kuku weusi basi manuizo ya wenye nyumba yawe neutralized till mkataba utakapoisha ayaaamshe kama ataona inafaa
 

Kabisa mkuu!
Hii mambo ya kuhamia halafu unakutana na stiki kama mtoto hayafai!

Maana kuna jamaa aliwahi kuniambia kuwa alipohamia kwenye nyumba moja hivi alikuwa anatandikwa fimbo sana hasa zile siku alizokuwa anamgegeda mkewe

Sikumwamini ila leo nimejua alichokuwa ananiambia....lol!

CC Mtambuzi !!!!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…