Nilichokiona Muleba nikitokea Uganda na Bukoba

Nilichokiona Muleba nikitokea Uganda na Bukoba

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
9,116
Reaction score
8,658
Majuzi kati nilienda kumsalimia rafiki yangu Bukoba baada ya nyumba yake kupitiwa na tetemeko la ardhi pia nikavuka border kufuata vitu fulani vya biashara. Wakati naenda nilitoka Katoro saa 10:30 jioni na kutokana na tochi za trafiki hivyo basi lilikimbia chini ya spidi 80Kmph na kusababisha kupita maeneo ya wilaya ya Muleba ngiza likiwa tayari limeshaingia. Kutokana na hali hiyo sikuona madhari ya nje lkn siku narudi basi lilisimama kupisha lori lililokuwa na kokoto na ndani ya basi kila mtu alikomaa kupiga picha nje kwani kulikuwa na mti umefungwa chupa za maji hadi matawi ambayo si rahisi kuyafunga. Swali kuu na lililokosa jibu ni kwa nini chupa hizo zimefungwa kwa wingi katika mti huo!!?? Wenyeji wa Muleba tunaomba elimu kidogo hapa
1475235444470.jpg
1475235454527.jpg
 
Ni kweli mkuu hata Mimi niliwahi kupita hapo,niliwauliza wenyeji wa hapo wanasema kuna bwana mmoja akili yake siyo nzuri anaishi hapo ndiye hufanya kazi hiyo kwa mda mrefu sasa na imegeuka Kuwa kivutio
Inawezekana ikawa kweli ndugu!!
 
Labda zimewekwa kama vimizinga vidogo vya asali hahahahaha
 
Ni kweli mkuu hata Mimi niliwahi kupita hapo,niliwauliza wenyeji wa hapo wanasema kuna bwana mmoja akili yake siyo nzuri anaishi hapo ndiye hufanya kazi hiyo kwa mda mrefu sasa na imegeuka Kuwa kivutio
Mbunifu...
 
Nilishawahi kuiona kwenye chombo cha habari kimoja nafkri ni TBC1 mwandishi akimsifia eti kijana ametunza mazingira
 
NO NI IMANI YENU TU...CHUPA KUNINGINIZWA KWENYE MATAWI MAANA YAKE NI KUYAFANYA MATAWI YAANYOOKE...NI KAMA WANAYA FANTA MATAWI KUWA IMARA...

OVA
 
eneo hili linaitwa MAGHARINI. liko jimbo la muleba kusini kwa bi. anna tibaijuka. mwaka jana nilikuwa eneo hili kikazi. nikavutiwa sana. hadi nikafanya mahojiano na mdau mwenye kibanda cha soda juu tukio hili la kustajabisha. akaeleza kuwa alikuwepo mdau kijana mwenye magonjwa ya akili aliyeishi hapo muda mrefu, akawa anakusanya chupa za plastiki, ndoo, magalon na kuyafunga kwa ustadi kwa kutumia kamba kisha kuyaning'iniza (pichani). mwaka juzi walikuja wazungu wakastaajabu kazi ile na walipododosa wakahitaji kukutana na huyo kijana. wwnyeji wanasema waliondoka naye hadi sasa haijulikani yuko wapi, alipona, aliongezewa maarifa (utundu). *chanzo: simulizi fupi kwa wenyeji.
 
Mbona maelezo yako yana utata unatokea Uganda unaenda Muleba kumuona rafiki yako, kwa hiyo ulipanda gari ya kwenda Mwanza ukashuka Muleba halafu ukaelekeawawapo baadae
 
Ni kweli mkuu hata Mimi niliwahi kupita hapo,niliwauliza wenyeji wa hapo wanasema kuna bwana mmoja akili yake siyo nzuri anaishi hapo ndiye hufanya kazi hiyo kwa mda mrefu sasa na imegeuka Kuwa kivutio

Sasa si mara 100 angechukua zile m200 akamtibu huyo jamaa
 
Ikumbukwe pia kwa mkoa wa Kagera kuwa wilaya ya Muleba inasifikana kwa ushirikina wa nguvu, yaani hawa magovi wanatisha ile mbaya.
 
Mbona maelezo yako yana utata unatokea Uganda unaenda Muleba kumuona rafiki yako, kwa hiyo ulipanda gari ya kwenda Mwanza ukashuka Muleba halafu ukaelekeawawapo baadae
Nilienda Bukoba kumuona rafiki yangu pia nikavuka border hadi Kampala baada ya kumsalimia (wakati naenda sikuona hicho kituko sababu nilipita kigiza kimeshaanza, mbona hadi niliposti uzi kuonyesha madhara ya tetemeko hadi guest niliyolala) . Hivyo wakati narudi nilipita maeneo hayo mchana muda wa saa 10 jioni na kuona hicho kituko
 
Hata pale FIRE Karibu na kariakoo kuna jamaa mmoja kichaa kichaa hivi anaandikaga falsafa zake na kuning'iniza makopo kwenye nguzo za Umeme
 
Juma lililopita nimepita hapo nikasimama kushangaa, kwa mujibu wa wenyeji wanasema kuna bwana mmoja (bubu) na ni mgonjwa wa akili hufanya kazi ya kukusanya hayo nakopo na kuyaning'iniza kwa kamba kwa ustadi wa aina yake pale~amazing!
 
Back
Top Bottom