Nilichojifunza ndani ya mwaka mmoja bila ajira

Wakati huo mwenye kuweza kuweka mazingira mazuri ya ajira ananunua madege kwa fujo ili kuwapatia watoto wa Trump ajira huku wa kwake wakihangaika mitaani.
Cha ajabu zaidi wabunge majuha ya CCM kazi ni kupongeza upuuzi!!!
 
Shida ni pale unapoajiriwa, halafu ukasahau kuwekeza
Ikiwa hauna ajira ni rahisi kufikiri kuwa wenye ajira wana kipato kikubwa kinachowawezesha kuwekeza!! Sehemu kubwa ya waajiriwa kipato chao hakitoshelezi mahitaji yao Hivyo huwa na madeni muda wote! Mshahara ukichelewa siku mbili tu wataanza kulia humu jamvini!
Ni heri anayehangaikia kujiajiri mwisho wa siku ataibuka kidedea!!
 
Vitabu sometimes vinasaidia sana kuvisoma vinapanua knowledge ya mtu na uwezo wa kufanya imagination ya maisha yako ya baadae kabla ya kuiacha iyo kazi,kuna kitabu kinaitwa BEFORE I QUIT MY JOB,Utajifunza mengi sana namna watu wanavyohaso kipindi wameacha kazi au kuachishwa kazi, usiweke miguu miwili kazini maana muda wowote unatolewa.
 
BITTER TRUTH
_If you really love your children, get a business, not a job, because when you die your children cannot inherit your job, but they can definitely inherit your business. In fact, if you die on the job, your boss will replace you before your burial.

If your family live in the company house, they will kick them out before they can say anything. So when you close from work, don’t go and watch television. Go home and think of a business idea._

:Uhuru Kenyatta Quote.
 
Hii ni fact 100 percent
Nashukuru kwa kuianzisha siku yangu vizuri.

Hili la mke kuwa mpambanaji kwa wale walio makazini ni jambo zuri sana japo wengi hawaliwezi, ukiwa kazini mwanaume unapaswa kumtumia mkeo kama tool kwenye kutafuta kipato mbadala..
 
Nina miaka miwili sina kazi, nilifanyiwa figisu kama zako - nimepanga Tabata 250K per month, watoto wa2, mmoja anasoma std 6 Atlas na mwingine std 2 Christ the King. Nitakomaa mpaka tone la mwisho hapa mjini.

NB: Figisu za mjini naziweza vizuri tu-wala sio muoga wa maisha.
Mkuu ungetwambiaje unafanya nini kwa sasa ili utifundishe, hili neno la NITAKOMAA halina definition.
 
Nashukuru mkuu, siwezi kata tamaa.
Hapo ulipo una deni la mil.3. Hii ni Hasara. Faida uliyonayo ni uzoefu was miaka 2 katika kilimo cha matikiti, shamba, pump, kijumba cha kupumzikia shamba, vifaa vya kulimia. Kitu kingine ni connection na wapi pa kupata na jinsi ya madawa (rudi kalime tikiti changanya na mazao mengine yanayoendana) ukipata faida kidogo jaa na juchanganye sehemu zenye mdongamano wa watu wengi kama gongolamboto, mbezi mwisho, mbagara fanya buashara
 
Usikate Tamaa. Jaribu kulima aina Nyingine ya mazao ambayo unaona inalipa.pia fanya Tafiti ( Research ) ni zao gani linastawi vema katika eneo uliokuwa nalo. hii itakupa ufanisi mkumbwa katika kilimo chako na hata utendaji wako wa kazi!
 
Nilichojifunza ni kuwa ajira ni kama mtumwa anayelipwa. Huna haki ya kiomba fidia yako. Na ukojidai kimbelembele unatumbuliwa. Hii ndiyo maana unaona hata viongozi wa serikalini siku hizi wamekuwa kama mbwa koko. Wanabweka mbele ya mwenye mbwa ila kumbe huku nyuma wanakutana na pumbavu za kutosha.
😂😂😂
 
Wewe ulikuwa unapiga mishe gani ya kudhalilisha?
Sio aibu mkuu vitu vingine hua haviko poa maana katika maisha habari mbaya ndo husambaa zaidi kuliko habari nzuri mfano ukifukuzwa kazi watu wengi sana watashangilia tofauti na ukipata shavu i.e World Bank
 
Mkuu mugomangara, nimefurahi kuwa watu wengi wako upande wako. Ila kuna mdau hapa amekupa ushauri ambao nahisi au umeufuata au nyote mlikuwa na mawazo sawa. Swali langu ni je una soko tayari la hizo Karanga? Na kama bado kwanini usijaribu tu kutafuta soko au sehemu yenye soko/ order hata kwa kuanzia hapa JF?

Kuna wataalamu wa kila aina ukimjulisha na Mh.aliyesema hutamsahau. Pia piga mahesabu na ujue kuwa Karanga zako utakuwa na kiasi gani na utaweza kuziuza kwa kiasi gani na ni lini mwisho utangaze hapa. Unaweza kupata mnunuzi hapa hapa.

Na hivi Kilimo cha Ekari 2 utaingiza kiasi gani chaa pesa? Unaweza kupata watu wa kukuchangia/ sio mkopo, hata ukipata watu 20.

Nakutakia kila la kheri.

Ahsante ndugu...ninasubiri mvua nipande karanga hekari 2 kwanza
 
Je,umejiwekea kuangaika kwa muda gani?
1.ikiwa ni miezi tu lima mbogamboga
2.ikiwa ni mwaka mmoja lima miwa maana unalo bwawa la maji
3.ikiwa miaka 4 lima matunda hasa machungwa,malimao,machenza...nk
4.ikiwa ni miaka 10 na zaidi lima miti ya mbao

NILIYOYAPATA KWA POST ZOTE 280
Nyanya eden f1 gm.5 ni sh.50,000 na ina miche 500 to 800 na zinakomaa kwa siku 80 wanashanbuliwa sana na mdudu aitwaye 'Tuta Absoluta' au 'Kanitangaze

NB
kuhusu ufugaji sijagusia kabisa, pomoja na changamoto zako za kazi ya kuajiriwa
Mwisho
Samahani ikiwa nimekukwazeni washiriki
 
Miye hapo kwenye kufukuzwa kazi hakuna mkono mrefu kwa serikali naomba kujua tu ajira yako ilikuwa ya kudumu au mkataba kama mkataba je huo mkataba unao, pili mlikuwa mnalipanaje mshahara kupitia bank au mnapeana mkononi tu kama bank je kuna salary slip?

Kama ni bank na salary slip zipo haki yako ipo bado

Kama ulijaza mkataba na unahisi ukienda kinyume na mjataba ulifukuzwa tu kazi haki yako ipo

MY TAKE

Wale watu wa idara ya kazi ebu jitangazeni watu wa wajue majukumu yenu na mnasaidia vipi wafanyakazi kama hawa watu hawajui kabisa kuwa wakija uko mtawapa wanasheria bure kudai haki zao na hawajui kuwa kampuni nyingi tz ni wajanja wajanja so idara ya kazi ndio mwarobaini wao yani wakija uko boss aruki sababu anajua kampuni yake ina uhuni mwingi so wanaogopa chunguzwa
 
Ng'ombe Wa maziwa ni mradi mzuri sana, ukifakikiwa kuyaongeza thamani maziwa unatija zaidi.
Mfano mikoa mingi bei ya maziwa fresh ni shilingi elfu moja kwa Lita, lakini maziwa hayo ukiyaongeza thamani utauza bei ya jumla shilingi elfu tatu mpaka nne.

Lakini pia kuna baadhi ya miji maziwa fresh huuzwa shilingi elfu mbili kwa lita kabla hayajaongezwa thamani.
Kuongeza thamani maziwa yanatija Kwani hata uhifadhi wake ni Wa muda mrefu na sasa hivi process za kisheria kuhusu value added zimepelekwa mpaka wilayani kupitia sido na TBS.

Bei ya ngo'mbe Wa maziwa kwa mashamba ya serikali ni shilingi milioni moja na laki tano na unapata mtamba ambae akizaa unaweza kamua maziwa zaidi ya Lita kumi kwa siku.

Sioni wadau wakishauri kufuga ng'ombe wa maziwa sijui mradi huu umepoteza umaarufu?
 
Back
Top Bottom