Nilichojifunza kutoka kwa Khadija

Nilichojifunza kutoka kwa Khadija

Kuna demu nilimfahamu kupitia job, alikuwa ni client, nikamuelewa nikafanya mishe nikapata namba.
Nikawa nawasiliana nae. Namuulizia hali yake, ananiomba ushauri kuhusu hali yake.
Hadi nilienda kumsalimia kwao.
Tukawa tunapiga stori (kwenye simu) yaani naona huyu anakuja kabisa, kilichobaki ni kurusha ndoano

Nikaona hana dalili ya kuwa na mtu, nikarusha ndoano. Akaruka, eti kwa sasa hataki mahusiano.yamemtesa hapo nyuma.

Nikaforce, akasema labda usubiri. Nikasema sawa ngoja tuone.

Mdogomdgo nikaona mimi ndio nahangaika kumtafuta, au kuanzisha mawasiliano.

Mwaka 2024 nikaanza kuwa namkaushia, hata wiki mbili hadi tatu.
Naona na yeye hata hanitafuti.

Nikaconclude kisicho riziki hakiliki.


Ila demu ni mkali jamani.
Kwahiyo fupa lilikushinda mkuu
 
Hapo sina ujanja.

Demu nikikaa wiki bila kunitafuta na yeye hanitafuti.
Nikisema nimtafute inakuwa unidirectional conversation.


Sasa hapo unafnya nini?
Haina namna kwakweli, mi kwa adija pamoja na mda wote huo ila nilitoka empty
 
wanawake huwa hawakatai ukiona anakukataa ujue haujaongea naye kwa njia sahihi
 
Class ulikua unawaza mapenzi tu na bado hata kwenye mtihani ungewekewa swali la kuandika jina la demu unaempenda bado ungelikosa ungeandika hivyo hivyo adija
 
Class ulikua unawaza mapenzi tu na bado hata kwenye mtihani ungewekewa swali la kuandika jina la demu unaempenda bado ungelikosa ungeandika hivyo hivyo adija
We ulitaka naindike Khadija?? Yeye mwenyewe alikua ameandika kwenye counter book zake adija mkuu
 
Hope mko poa kabisa wakubwa.

Nina kisa changu kinachohusu mapenzi, na kuyasotea.

Kati ya waliowahi kusotea pis basi namm nipo,, ila nilitoka kapa tena kapa ya gamba.

Kipindi tupo sec kuna demu tulikua tunasoma nae anaitwa adija. kiukweli nilitokea kumpenda vibaya mno.
nilisotea kidogo niwe mwehu

ila mpaka tunamaliza shule sikuwahi hata kumshika mkono wake tu,, niliongea mpaka maneno yakaisha ila sikulamba unga.

Story ni ndefu ila ngoja kawe kafupi tu,, mpaka nikiwa kitaa bado sikuacha kumuwaza kabisa, ila yule mtu misimamo wake ulikua uleule, kwamba hanitaki hata iweje.

Baadae sana nikaamua kumove on ili maisha mengine yaendelee. Mbaya zaidi kuna watu walikua wanapita nae kama upepo vile,, tena anawafuata yeye mwenyewe .

nikabaki na somo kwamba anayekupenda hawezi kukusotesha miaka yote hiyo,, na tena kilikua king'ang'anizi changu tu pengine ningeamua kumtema mapema yote hayo yasingekuepo.

Kuna muda nilifikiria nimchukie ila nikaona hana kosa, nilimpenda mimi hakuniita so bado ningeuka fala kama ningemchukia.

Tangu hapo sisoteagi mademu tena,, natongoza siku tatu za nguvu asipoeleweka namtema mapema kabisa,,.

Mtu akikuelewa atakujibu mapema tu.. ila wale ambao bado mnatongozaga mwaka mzima hongera kwenu.

Ukiforce demu akuelewe maybe kwa kumpa pesa kibao na mengineyo hapo elewa kabisa mud wowote ule utapigwa na kitu kizito.

Mademu wengine anaweza kuact amekupenda baada ya kuhangaika muda mrefu, inabidi akupe penzi la uongo na kweli ili afidie alizokula kwako, siku akiona malipo yamekamilika anasepa zake. ukiwa mwehu utaanza kuhaha ulipe kisasi,, bro endelea na mambo mengine visasi ni majuto na ni ujinga, kwani alikuita ukampende??? Jibu ni hapana, kwann sasa uingie kwenye ugomvi wa kijinga..

Ukiona haeleweki tafta chuma kingine.

Penzi la kweli halitafutwi kwa miaka mingi.
Khadija/Hadija ila kama uliandika jina lake ulivyoandika - Adija akaliona inawezekana alikumind
 
We ulitaka naindike Khadija?? Yeye mwenyewe alikua ameandika kwenye counter book zake adija mkuu
Moderator kakubadilishia heading kakuandikia Khadija badala ya Adija kwahiyo jina la mpenzi wako linatakiwa kuandikwa hivyo sawa bro?
 
Khadija/Hadija ila kama uliandika jina lake ulivyoandika - Adija akaliona inawezekana alikumind
Mi nimeandika kama yeye alivyokua akiliandika
 
Moderator kakubadilishia heading kakuandikia Khadija badala ya Adija kwahiyo jina la mpenzi wako linatakiwa kuandikwa hivyo sawa bro?
Basi poa mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom