Mheshimiwa Waziri mkuu wa Tanzania Bw Mizingo Pinda alitamka hayo alipokua akijibu maswali ya viongozi wa jumuia mbalimbali za Watanzania waishio Uingereza. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania jijini London pia ulihudhuriwa na Mh Balozi mama Mwanaidi Maajar na Maafisa wa ubalozi.baada ya viongozi wa jumuia hizo kujitamulisha wakiongozwa na mwenyekiti wa Tanzania association,Waziri mkuu alitoa fursa ya kujibu maswali badala ya kutoa hutuba,akichelea kuwbowesha wasikilizaji wake.Maswali yaliyojitokeza yalihusu 1,uraia wa nchi mbili 2,hali ya ufisadi nchini TZ 3,mizigo bandarini 4,hospitali mkoa wa mara 5,rushwa(bandari,TRA,(EPA)).6,hospitali ya muhimbili na 7,kitabu ;bunge lenye meno.Katika kujibu maswali hayo waziri mkuu alielezea hali ya bandari ya dar kama ni ya kusikitsha mno na ana hakika ubovu mkubwa uliopo na uzorotaji unasababishwa na MKATABA MBOVU ambao umemkabidhi Mkandarasi mmoja kumiliki shughuli zote. kutokana na kukosa mshindani imemfanya aendeshe kama apendavyo alisema waziri Pinda.Hiyo ni tofauti kabisa na hali niliyoikuta Dublin,Bandari ya Dublin kuna Wakandarasi Tisa wanaoopareti hivyoni wazi kutakua na ushindani wa kutrak Meli in. Hivyo nimeondoka na funzo kuwa mkataba tulionao Dar hautufai na hauwafai Wananchi na sidhani kama itakuwa kazi kuwashawish wenzangu kuvunja mkataba huo na tuige mfano wa Dublin.I think we can alisisitiza Pinda na Wasikilizaji walijibu YES WE CAN huku wakipiga makofi.Chanzo changu kiliniarifu kuwa kikao hicho kilichelewa kuanza lakini kwa mtazamo wake kilikua cha mafanikio kwa pande zote. kikao kilifanyika jana 02 03 2009.
Takriban mwaka na miezi miwili sasa toka waziri mkuu Mh. Mizingo Pinda atoe ahadi ya kurekebisha matatizo yaliopo katika bandari ya DAR ifanane na aliyoyaona katika bandari ya Dublin. Kesho 26/05/2010 anakutana na Wadau wale wa mwaka jana jijini London, mh Waziri mkuu, swali la nyongeaza: Ni mabadiliko gani yamefikiwa katika Bandari ya Dar es salaam toka ulipotupa ahadi ya kupeleka mfano wa Bandari ya Dublin zaidi ya mwaka mmoja uliopita?