Mwanabalagha
Senior Member
- Nov 11, 2015
- 196
- 235
Habari za saa hii wadau,
Hope mko poa na mishe zinasonga hata kama ni kiubishi...
Ni hivi;
Moja kati ya siku chache zilizopita niliamua kumpeleka mchumba wangu kwetu.Mimi najitegemea na ninaishi mbali kidogo na familia yetu kutokana na kazi.Baada ya kufika nae tulikaa pale tukapiga stori mbili tatu mpaka mida ya usiku then tukaenda kulala,kifupi tulikaa pale kwa muda wa siku kama tatu then tukarudi kwenye makazi yetu mi na mwenzangu.
Huyu binti (naomba nimtaje kabila kwa maana ndo msingi wa thread hii) kachanganya kabila, baba ni mtu wa Singida (Mnyiramba) na mama ni wa kusini (Mmakonde).Sasa kilichotokea baada ya kurudi huku nakoishi kesho yake nilipigiwa simu na shangazi yangu nakuniambia haya yafuatayo:-
Binti ni mzuri tumempenda ni mpole na ana sifa nyingi nzuri, ila tatizo kabila lake. Wao (wamakonde) udamaduni wao ni kwamba watoto wote ni wa upande wa mama, hivyo mkipata mtoto tu akishaanza kutembea anakuja kuchukuliwa na bibi yake (mzaa mama) anaenda kulelewa huko we mume huna chako tena.
Vilevile mjomba mtu (kaka wa mwanake utakayemuoa) ndo anakuwa na amri juu ya huyo mtoto kuliko wewe baba yake.
Nikamuuliza shangazi kwanini inakuwa hivyo?
Akanijibu hivi:-
Kwasababu wanaamini mwanaume anaweza kusingiziwa mtoto na mkewe akaambiwa wake kumbe sio. Hivyo kwasababu mtoto wao ni wa kike wanaamini kile alichojifungua ni halali yake kwasababu kimetoka kwenye tumbo lake kabisa kwahiyo yeye ndo mwenye mtoto.
Hivyo kazi kwako baba sisi tunakushauri tafuta binti mwingine au laa!Ukitaka mwenyewe oa ila usije ukarusha ngumi kwa shemeji zako huko mbeleni.Nikachoka!Mpaka sasa nimejaribu kutafuta ukweli wa hili ila bado sijapata majibu ya kuridhisha. Ningependa mwenye kuelewa hili swala hebu anifahamishe je ni kweli wamakonde watoto wote huwa upande wa mama?Na kwanini? Huenda nikapata kitu tofauti hapa.
Natunguliza shukrani karibuni kwa uchangiaji.