Nilichoambiwa nyumbani baada ya kumtambulisha mchumba wangu

Wacha nijikwendee zangu, maana ntaonekana mnoko. Ila ndugu, maneno ya mzazi wako huyo yatathmini na uyafanyie kazi. Kazi gan, utajua wewe. Ila makabila mengine ni ya kuoana wao kwa wao fulu stopu
 
Habari za saa hii wadau,

Hope mko poa na mishe zinasonga hata kama ni kiubishi...

Ni hivi;

Moja kati ya siku chache zilizopita niliamua kumpeleka mchumba wangu kwetu.Mimi najitegemea na ninaishi mbali kidogo na familia yetu kutokana na kazi.Baada ya kufika nae tulikaa pale tukapiga stori mbili tatu mpaka mida ya usiku then tukaenda kulala,kifupi tulikaa pale kwa muda wa siku kama tatu then tukarudi kwenye makazi yetu mi na mwenzangu.

Huyu binti (naomba nimtaje kabila kwa maana ndo msingi wa thread hii) kachanganya kabila, baba ni mtu wa Singida (Mnyiramba) na mama ni wa kusini (Mmakonde).Sasa kilichotokea baada ya kurudi huku nakoishi kesho yake nilipigiwa simu na shangazi yangu nakuniambia haya yafuatayo:-

Binti ni mzuri tumempenda ni mpole na ana sifa nyingi nzuri, ila tatizo kabila lake. Wao (wamakonde) udamaduni wao ni kwamba watoto wote ni wa upande wa mama, hivyo mkipata mtoto tu akishaanza kutembea anakuja kuchukuliwa na bibi yake (mzaa mama) anaenda kulelewa huko we mume huna chako tena.
Vilevile mjomba mtu (kaka wa mwanake utakayemuoa) ndo anakuwa na amri juu ya huyo mtoto kuliko wewe baba yake.

Nikamuuliza shangazi kwanini inakuwa hivyo?
Akanijibu hivi:-
Kwasababu wanaamini mwanaume anaweza kusingiziwa mtoto na mkewe akaambiwa wake kumbe sio. Hivyo kwasababu mtoto wao ni wa kike wanaamini kile alichojifungua ni halali yake kwasababu kimetoka kwenye tumbo lake kabisa kwahiyo yeye ndo mwenye mtoto.

Hivyo kazi kwako baba sisi tunakushauri tafuta binti mwingine au laa!Ukitaka mwenyewe oa ila usije ukarusha ngumi kwa shemeji zako huko mbeleni.Nikachoka!Mpaka sasa nimejaribu kutafuta ukweli wa hili ila bado sijapata majibu ya kuridhisha. Ningependa mwenye kuelewa hili swala hebu anifahamishe je ni kweli wamakonde watoto wote huwa upande wa mama?Na kwanini? Huenda nikapata kitu tofauti hapa.

Natunguliza shukrani karibuni kwa uchangiaji.
Wewe owa tu huyo demu iwapo unampenda na ana adabu,hayo mambo ya jadi za kihanisi achana nazo bhana,sheria dunia nzima inatambua mtoto ni wa baba,huyo ANKO NCHUMALI kama anataka kuleta UNYAMBIZ mwambie na yeye kama anataka azae na wewe alete tigo,eboooo,mtoto niwa baba hata maandiko yote matakatifu yanasema hivyo,Mahakama na sheria za nchi zinatambua hilo,mwanamke yeye ni sawasawa na OVEN tu,yaani unakoroga mchanganyiko wote wa KEKI,ukishamaliza unaweka kwenye OVEN ili KEKI YAKO IIVE,IKIIVA UNAITOA UNAILA.Kwa hiyo mama ni OVEN na baba ni KEKI, Daaaaah hii nchi hii ni balaa,ndio maana OOOOH TUNATUMBUA MAJIPU,HAYA MTUMBUENI NA ANKO NCHUMALI SHWAIIIIIN KENGE BLUU.
 
nikweli kabila za kusini mtwara
mwanammke ndo mwenye watoto.. pia mume akienda kuoa mahala anahamia huko
yani dizaini kama anaolewa.
hio ni asili yao haiwezi kupotea.
japo kwa sasa imepungua hasa kwa tunaokaa mijini (wamakonde,wamakua,wayao,wamwera)

kwa mfano mimi mama angu mmakua baba mtu wa musoma
sisi ni watoto wa baba
japo tunaishi mjini na tumelelewa mazingira ya kimakua sana ...
kama vile tumechezwa, tuna ukaribu sna na ndugu wa mama kuliko baba..

ila mwisho wa siku ni makubaliano yako na huyo dada..
kuhusu kuchukua watt kulelewa na bibi zao wamakonde wanapenda sana watto
kwahiyo ukionyesha huna mapenzi wanamchukua mtoto wanakaa nae...
Watachukua mtoto kwa sheria ipi?,nchi inaongozwa na LAW OF THE LAND na sio TRADITINAL LAW.
 
nikweli kabila za kusini mtwara
mwanammke ndo mwenye watoto.. pia mume akienda kuoa mahala anahamia huko
yani dizaini kama anaolewa.
hio ni asili yao haiwezi kupotea.
japo kwa sasa imepungua hasa kwa tunaokaa mijini (wamakonde,wamakua,wayao,wamwera)

kwa mfano mimi mama angu mmakua baba mtu wa musoma
sisi ni watoto wa baba
japo tunaishi mjini na tumelelewa mazingira ya kimakua sana ...
kama vile tumechezwa, tuna ukaribu sna na ndugu wa mama kuliko baba..

ila mwisho wa siku ni makubaliano yako na huyo dada..
kuhusu kuchukua watt kulelewa na bibi zao wamakonde wanapenda sana watto
kwahiyo ukionyesha huna mapenzi wanamchukua mtoto wanakaa nae...
yaani mtu #AJE kumchukua mwanangu wakati huo nhpo wapi, na ananiambiaje wakati anamchukua?
 
Habari za saa hii wadau,

Hope mko poa na mishe zinasonga hata kama ni kiubishi...

Ni hivi;

Moja kati ya siku chache zilizopita niliamua kumpeleka mchumba wangu kwetu.Mimi najitegemea na ninaishi mbali kidogo na familia yetu kutokana na kazi.Baada ya kufika nae tulikaa pale tukapiga stori mbili tatu mpaka mida ya usiku then tukaenda kulala,kifupi tulikaa pale kwa muda wa siku kama tatu then tukarudi kwenye makazi yetu mi na mwenzangu.

Huyu binti (naomba nimtaje kabila kwa maana ndo msingi wa thread hii) kachanganya kabila, baba ni mtu wa Singida (Mnyiramba) na mama ni wa kusini (Mmakonde).Sasa kilichotokea baada ya kurudi huku nakoishi kesho yake nilipigiwa simu na shangazi yangu nakuniambia haya yafuatayo:-

Binti ni mzuri tumempenda ni mpole na ana sifa nyingi nzuri, ila tatizo kabila lake. Wao (wamakonde) udamaduni wao ni kwamba watoto wote ni wa upande wa mama, hivyo mkipata mtoto tu akishaanza kutembea anakuja kuchukuliwa na bibi yake (mzaa mama) anaenda kulelewa huko we mume huna chako tena.
Vilevile mjomba mtu (kaka wa mwanake utakayemuoa) ndo anakuwa na amri juu ya huyo mtoto kuliko wewe baba yake.

Nikamuuliza shangazi kwanini inakuwa hivyo?
Akanijibu hivi:-
Kwasababu wanaamini mwanaume anaweza kusingiziwa mtoto na mkewe akaambiwa wake kumbe sio. Hivyo kwasababu mtoto wao ni wa kike wanaamini kile alichojifungua ni halali yake kwasababu kimetoka kwenye tumbo lake kabisa kwahiyo yeye ndo mwenye mtoto.

Hivyo kazi kwako baba sisi tunakushauri tafuta binti mwingine au laa!Ukitaka mwenyewe oa ila usije ukarusha ngumi kwa shemeji zako huko mbeleni.Nikachoka!Mpaka sasa nimejaribu kutafuta ukweli wa hili ila bado sijapata majibu ya kuridhisha. Ningependa mwenye kuelewa hili swala hebu anifahamishe je ni kweli wamakonde watoto wote huwa upande wa mama?Na kwanini? Huenda nikapata kitu tofauti hapa.

Natunguliza shukrani karibuni kwa uchangiaji.
Kifupi tafuta binti mwingine wa kuoa huyo atapata shida sana kwa upande wa wazazi wako!
Hiyo sababu walio kupa ni moja tuu lakini kuna sababu nyingi tu wanazo lakini hawawezi kukwambia na ukitaka wakwambie lazimisha kumuoa!

Kwa kuwa waafrika tunao kwaajili ya familia zetu basi nakushauri tafuta binti mwingine huyo halufai!
 
.Ndg yangu mm nilioa mke.wa kimakomde nimekaa naye miaka 14 tukafanikiwa kupata watpto watatu lkn ilitokea kugombana tu mke wangu huyo aliamriwa aondoke na watoto wote hadi sasa na wameshachezwa mila za huko. Pia huwa siyo watu wa kudumu katika ndoa.
Aisee!! pole sana mkuu, asante sana kwa ushuhuda wako.
Hivi hao watoto tangu waondoke hukuenda kuwadai? au ulienda mambo yakawaje?
Ningependa unifahamishe hayo kabla nami sijatumbukia huko kusini.
 
Kifupi tafuta binti mwingine wa kuoa huyo atapata shida sana kwa upande wa wazazi wako!
Hiyo sababu walio kupa ni moja tuu lakini kuna sababu nyingi tu wanazo lakini hawawezi kukwambia na ukitaka wakwambie lazimisha kumuoa!

Kwa kuwa waafrika tunao kwaajili ya familia zetu basi nakushauri tafuta binti mwingine huyo halufai!
Sawa mkuu nimekuelewa, asante sana kwa ushauri wako.
 
Hivi bado mpaka generation hii tunaulizana na kufanya judging juu ya makabila tu!?
 
Sio kwl m mwenyw mmakonde tena wa newala karbu na msumbiji
Hayo mambo hakuna ila kilichokuwepo ni mila potofu tu
Kama mnavyoamini pia kuwa mmakonde anakula watu
Hata cc huku tunaamini kuna makabila yanakula mbwa ya huko kaskazi

Kama vp muulizeni mkwichika(mb) wa newala mjini maana ni mmakonde pure
niko chiungutwa sasa sijui nimeongopa nini
 
mambo ya zamani hayo, siku hizi hizo mila tumekwishazipiga ban.. vuta mke huyo kama unampenda kweli story za kina shangazi achana nazo
 
simple tu, mwulize mchumbaako yeye anamilikiwa ujombani au kwa baba ake,of which najua mpaka sasa jibu unalo since the very beginning. kama jibu ni kwa baba basi oa.
 
Back
Top Bottom