Nilichoambiwa nyumbani baada ya kumtambulisha mchumba wangu

Mwanabalagha

Senior Member
Nov 11, 2015
196
235
Habari za saa hii wadau,

Hope mko poa na mishe zinasonga hata kama ni kiubishi...

Ni hivi;

Moja kati ya siku chache zilizopita niliamua kumpeleka mchumba wangu kwetu.Mimi najitegemea na ninaishi mbali kidogo na familia yetu kutokana na kazi.Baada ya kufika nae tulikaa pale tukapiga stori mbili tatu mpaka mida ya usiku then tukaenda kulala,kifupi tulikaa pale kwa muda wa siku kama tatu then tukarudi kwenye makazi yetu mi na mwenzangu.

Huyu binti (naomba nimtaje kabila kwa maana ndo msingi wa thread hii) kachanganya kabila, baba ni mtu wa Singida (Mnyiramba) na mama ni wa kusini (Mmakonde).Sasa kilichotokea baada ya kurudi huku nakoishi kesho yake nilipigiwa simu na shangazi yangu nakuniambia haya yafuatayo:-

Binti ni mzuri tumempenda ni mpole na ana sifa nyingi nzuri, ila tatizo kabila lake. Wao (wamakonde) udamaduni wao ni kwamba watoto wote ni wa upande wa mama, hivyo mkipata mtoto tu akishaanza kutembea anakuja kuchukuliwa na bibi yake (mzaa mama) anaenda kulelewa huko we mume huna chako tena.
Vilevile mjomba mtu (kaka wa mwanake utakayemuoa) ndo anakuwa na amri juu ya huyo mtoto kuliko wewe baba yake.

Nikamuuliza shangazi kwanini inakuwa hivyo?
Akanijibu hivi:-
Kwasababu wanaamini mwanaume anaweza kusingiziwa mtoto na mkewe akaambiwa wake kumbe sio. Hivyo kwasababu mtoto wao ni wa kike wanaamini kile alichojifungua ni halali yake kwasababu kimetoka kwenye tumbo lake kabisa kwahiyo yeye ndo mwenye mtoto.

Hivyo kazi kwako baba sisi tunakushauri tafuta binti mwingine au laa!Ukitaka mwenyewe oa ila usije ukarusha ngumi kwa shemeji zako huko mbeleni.Nikachoka!Mpaka sasa nimejaribu kutafuta ukweli wa hili ila bado sijapata majibu ya kuridhisha. Ningependa mwenye kuelewa hili swala hebu anifahamishe je ni kweli wamakonde watoto wote huwa upande wa mama?Na kwanini? Huenda nikapata kitu tofauti hapa.

Natunguliza shukrani karibuni kwa uchangiaji.
 
Ni vema kupokea ushauri haswa kutoka kwa wakubwa zako ila si kila ushauri unapaswa kuufanyia kazi kama ulivyo....Vema wakati unaangalia kupata historia kutoka kwa watu baki huku ambapo kila mtu atakuja na lake kama mimi nilivyokuja na langu ni vema ukamuuliza na mke wako ukasikia kutoka kwake na sababu mchumba wako baba yake ni Mnyiramba yeye hatokuwa Mmakonde atakuwa ni Mnyiramba na kama shangazi hana shida na mila za kKinyeremba vuta mchumba kwa raha zako..
 
Raha ya kuolea upendwe na wana ukoo! Sasa ukimuoa na wazazi wakajitenga nae itakuwaje? Je bint anasemaje?
Binti hana shida kusema ukweli namuona katulia, labda kama anaficha makucha. ila nimejaribu kumuulizia akasema haiko hivyo. Ukizingatia ye mwenyewe kalelewa na baba, mama aliondoka akiwa bado yupo shule ya msingi hivyo baba yake akaoa mke mwingine kutoka Tanga hivyo amelelewa sana na mama huyu wa kitanga.
 
нeвυ jυѕт тaĸe a тιмe υlιzιa ĸwa wazoeғυ wa нaya мaмвo wa нιlo ĸaвιla.....тнen тυleтee мrejeѕнo
 
Mkuu mimi nathani ukae na wazazi wako muongee. Waombe wakubariki na kukusaidia katika hili maana maneno yao yanajenga na kubomoa. Binti hana hatia kutokan na haya mambo. Isitoshe ukabila na mila hayo ni mambo ya zamani mkuu. Kama umempenda binti muoe.
 
nikweli kabila za kusini mtwara
mwanammke ndo mwenye watoto.. pia mume akienda kuoa mahala anahamia huko
yani dizaini kama anaolewa.
hio ni asili yao haiwezi kupotea.
japo kwa sasa imepungua hasa kwa tunaokaa mijini (wamakonde,wamakua,wayao,wamwera)

kwa mfano mimi mama angu mmakua baba mtu wa musoma
sisi ni watoto wa baba
japo tunaishi mjini na tumelelewa mazingira ya kimakua sana ...
kama vile tumechezwa, tuna ukaribu sna na ndugu wa mama kuliko baba..

ila mwisho wa siku ni makubaliano yako na huyo dada..
kuhusu kuchukua watt kulelewa na bibi zao wamakonde wanapenda sana watto
kwahiyo ukionyesha huna mapenzi wanamchukua mtoto wanakaa nae...
 
Ni vema kupokea ushauri haswa kutoka kwa wakubwa zako ila si kila ushauri unapaswa kuufanyia kazi kama ulivyo....Vema wakati unaangalia kupata historia kutoka kwa watu baki huku ambapo kila mtu atakuja na lake kama mimi nilivyokuja na langu ni vema ukamuuliza na mke wako ukasikia kutoka kwake na sababu mchumba wako baba yake ni Mnyiramba yeye hatokuwa Mmakonde atakuwa ni Mnyiramba na kama shangazi hana shida na mila za kKinyeremba vuta mchumba kwa raha zako..
Daah!! we acha tu mkuu.....wanasema japo kachanganya kabila ila bado hawana imani nae.
 
nikweli kabila za kusini mtwara
mwanammke ndo mwenye watoto.. pia mume akienda kuoa mahala anahamia huko
yani dizaini kama anaolewa.
hio ni asili yao haiwezi kupotea.
japo kwa sasa imepungua hasa kwa tunaokaa mijini (wamakonde,wamakua,wayao,wamwera)

kwa mfano mimi mama angu mmakua baba mtu wa musoma
sisi ni watoto wa baba
japo tunaishi mjini na tumelelewa mazingira ya kimakua sana ...
kama vile tumechezwa, tuna ukaribu sna na ndugu wa mama kuliko baba..

ila mwisho wa siku ni makubaliano yako na huyo dada..
kuhusu kuchukua watt kulelewa na bibi zao wamakonde wanapenda sana watto
kwahiyo ukionyesha huna mapenzi wanamchukua mtoto wanakaa nae...
Asante sana mkuu...nimekupata vilivyo
 
Kazi gani tena Evelyn Salt!!! hebu mwaga maeksipiriens basi kama ni kweli.
.... siku hizi mambo yamebadilika sana, muingiliano wa makabila umesababisha kubadilisha mambo mengi, wengi tunazaliwa kimjini tunakua kimjini mjini hizo asili na mambo za makabila hatuzijui tena wamebaki wachache sana wanaofata hayo mambo tena utakuta ni watu wazima kina shangazi, mchumba wako nae usikute hata hajui hizo mambo sasa atakujaje kumiliki watoto wakati hajui kama iko hivi? Muangalie yeye kama yeye ana sifa za mke unaemuhitaji? Unaweza kuishi nae hii yatosha
Habari za kusema watu wasingida sijui wapo vipi, i wanaocheat ndoa zao wote ni wa singida??? Wamakonde wengi tu tunawafahamu mbona hawana hizo
Ushauri wa ndugu zingatia ila pia wewe kama wewe fanya maamuzi
 
Wanakuzingua hao.... Wewe kama mmependana uoaneni... Nani siku hizi atachukua mzigo wa kukulelea watoto? Wakiwachukua mzalishe mtoto wao mitoto kumi .. Uone kama watakuwa na ubavu huo...
.. Ila ungetuambia kwanza kuwa unaishi wapi ??
 
  • Thanks
Reactions: BAK
.... siku hizi mambo yamebadilika sana, muingiliano wa makabila umesababisha kubadilisha mambo mengi, wengi tunazaliwa kimjini tunakua kimjini mjini hizo asili na mambo za makabila hatuzijui tena wamebaki wachache sana wanaofata hayo mambo tena utakuta ni watu wazima kina shangazi, mchumba wako nae usikute hata hajui hizo mambo sasa atakujaje kumiliki watoto wakati hajui kama iko hivi? Muangalie yeye kama yeye ana sifa za mke unaemuhitaji? Unaweza kuishi nae hii yatosha
Habari za kusema watu wasingida sijui wapo vipi, i wanaocheat ndoa zao wote ni wa singida??? Wamakonde wengi tu tunawafahamu mbona hawana hizo
Ushauri wa ndugu zingatia ila pia wewe kama wewe fanya maamuzi
Hio mambo ya sijui kabila flan flan imeshapitwa na wakati. Uongo?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom