Niliamini ananipenda kumbe alinifanya kichekesho

Niliamini ananipenda kumbe alinifanya kichekesho

Muimba SINGELI

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
4,211
Reaction score
10,840
Hii ilikuwa 2015 Kipindi hicho nikiwa Kijana Masikini tu.

Picha linaanza nikiwa na washkaji katika pool table majira ya usiku. hapo mtaa umechangamka sio kitoto unaambiwa, katika stori wana wawili ikawa wanasimuliana kuhusu dada mmoja tumwite LAIMA.

Nitaficha baadhi ya maelezo kwa kuweka maelezo bandia maana ameolewa na mumewe ni mwalimu nahofia asije kuwepo humu akanidaka bila hatia, maana huyo mdada japo yupo mkoa wa mbali lakini hadi kesho huwa ananitafuta akijisikia anataka kucheka.

Baasi bwana muhuni mmoja ambae ndiyo ana ukaribu na Laima ika anamwongelea kuhusu umbo lake chibonge tako laini kama sponji nk nk. ila kuna mwamba akawa anaponda balaa kwamba demu gani, anasura mbovu nk nk.

Mimi baada ya kusikia ni chibonge na ana tako laini machale yakani cheza nikamuuliza yule anaemsifia tumwite Deo.

"Oya deo kwani kazi yenyewe inaishi wapi?"

Deo akanielekeza ilikuwa ni wilaya ya jirani yetu.

Nikamuuliza jina na data nyingine muonekano kazi na vingine vingi, Deo akanipa kila kitu kwani ananijua vizuri
Ninapotaka kumuwinda mwanamke kupitia simu ni lazima nimjue angalau juu juu.
Mwisho nikamwomba anipe namba za Laima nikazisevu.

Baasi bwana... baada ya muda kwenda nikaelekea home, ilikuwa mishale ya saa nne nilipofika nikamtex yule dada.

'Samahi Laima hadi sasa nahisi hali yangu haiko sawa hivyo kesho sitowahi kuja huko, kama unaweza kupata mteja utaziuza tu ila kama hutopata hadi zikaharibika tuteshea hiyo hasara'

Nikakutupa kitochi changu kitandani nikaendelea na mambo mengine, kidogo naskia ngelengenje. Nikaiendea simu haraka kufungua meseji inasema.

'Wewe nani'

MIMI 'Kim hapa kwani namba yangu hukusevu'
Nitajiita KIM kwenye hii stori yaani ufupisho wa Ki-jana M-asikini kwasababu Kipindi hiko ilikuwa kabla sijatoboa.

YEYE 'Mbona sikufahamu unamtaka Laima gani?'

Hapa sasa nikampigia.

YEYE 'haloo'

MIMI 'Naam Laima ni mimi hapa hali yangu haiko vizuri ndiyo maana nikakwambia hivyo'
Niliongea kwa kujikaza kaza kama vile nagugumia maumivu ya homa😂

YEYE 'Samahani kaka Mbona sikufahamu!'

MIMI 'Kwani wewe sio Laima?'

YEYE 'ni mimi'

MIMI 'Sasa mbona unasema unifahamu! Mimi ni Kim ambae unaniuzia nyanya'

YEYE. 'NYANYA??'

Hiyo yote ilikuwa ni kumzingua tu maana yeye anauza Ice cream shuleni.

MIMI 'Ndiyo kwani mbona unashangaa sana'

YEYE 'mimi siuzi nyanya'

MIMI 'kwani wewe si Laima!'

YEYE 'ndiyo ni Laima lakini siuzi nyanya'

MIMI 'Laima acha kunichoresha halafu mimi sipo katika mzaha ujue'

YEYE 'Ha! Nakuchoreshaje sasa huyo mtu siyo mimi'

MIMI 'Laima hiyo sauti ni wewe mwenyewe kwani mimi nimechanyikiwa?'

YEYE 'kwani huyo laima unaemzungumzia wewe anaishi wapi?'

MIMI 'Mtwara mjini'

YEYE 'hahaha! Sasa mimi nipo Newala'

MIMI 'Laima usiwe mpumbavu'
Nikakata simu.

Kidogo anatuma ujumbe.

'Wewe kaka itakuwa hiyo homa ndiyo inakusumbua angalia vizuri hizo namba'

Mimi nikala buyu.

Baasi bwana pakakucha nikawaza nikafanya usafi geto huku wazo likiwa ni leo nitamwingiaje yule dada.
Nikafanya kila kitu home na kuingia Road,
Wakati niko zangu mgahawani Sms hiyo.. kucheki Laima.

'Unaendeleaje na hali yako kaka, vipi ulithibitisha kwamba mimi siyo mtu ambae ulikuwa unamwitaji'

MIMI 'naendea vizuri kiasi, nitakupigia muda kidogo maana sasa nakula ili niende nikajicheki zahanati'

YEYE 'Sawa ugua pole'

MIMI 'asante'

Ni kama ladha ya supu na chapati iliongezeka hivi, nilifakamia huku moyoni nikisema tayaari.. akili yenyewe ilikuwa na kazi ya kuvuta picha tu ya anavyofanania huyo chibonge.

Nitaendelea kesho TAJIRI napumzika sasa.

kama nina baya semeni...
 
FB_IMG_17467225212964101.jpg
 
Dadekiii Uzi mrefu kinomaa
 
NILIPOISHIA.
Baasi bwana pakakucha nikafanya usafi geto huku wazo likiwa ni leo nitamwingiaje yule dada.
Nikafanya kila kitu home na kuingia Road,
Wakati niko zangu mgahawani Sms hiyo.. kucheki Laima.

'Unaendeleaje na hali yako kaka, vipi ulithibitisha kwamba mimi siyo mtu ambae ulikuwa unamwitaji'

MIMI 'naendea vizuri kiasi, nitakupigia muda kidogo maana sasa nakula ili niende nikajicheki zahanati'

YEYE 'Sawa ugua pole'

MIMI 'asante'

Ni kama ladha ya supu na chapati iliongezeka hivi, nilifakamia huku moyoni nikisema tayaari.. akili yenyewe ilikuwa na kazi ya kuvuta picha tu ya anavyofanania huyo chibonge.

ENDELEA
Kipindi hiki nilikuwa natembeza mtumba naenda kulenga mnadani naingia kitaa kutafuta ugali.

Basi nikaingia zangu misele mida ya saa 7 hivi nikamrukia hewani wakati nipo kitaa natembeza nguo.

YEYE 'Halo'

MIMI 'eee mambo vipi'
Hapa nilichangamka sio kitoto.

YEYE 'poa habari za mchana'

MIMI 'amani tu dah samahani hii namba nilipewa na dada mmoja hivi anaitwa Laima, huwa tunafanya biashara ya nyanya sasa kama wiki nyuma aliibiwa simu, nilipofika kwenye biashara yake ndio akanipa hii namba kama namba yake mpya, niliisevu tu sikuwahi kumpigia nimeshangaa jana napiga nakupata wewe. hii asubuhi nimemtafuta mama flani ambae wanafanya biashara pamoja amenitumia namba za huyo dada.
Nilipomcheki
Nikamuuliza kuhusu namba hizi anasema labda alivurugwa tu wakati ananipa maana hazifanani kabisa na namba zake. Kinachonishangaza ni kwamba mmefanana majina hadi sauti yaani anaongea kama wewe'

YEYE 'Ha kweli binadamu wawili wawili!'

MIMI 'kabisa Samahi kwa kukusumbua lakini'

YEYE 'aah ni kawaida hamna shida, vipi umepona mbona umechangamka hivyo'

MIMI 'Hapana ila niko poa nimeenda kucheki ni maralia tu'

YEYE 'Ahaa kwani uko wapi'

MIMI 'Mtwara mjini kuna sehemu inaitwa Mtawanya, umeshawahi kufika Mtwara mjini?'

Nilidanga'nya mtaa ili kumlinda Deo asije julikana kama ameuza namba, lakini pia kuweka uhalisia kwamba homa imenifanya nisiwahi kwenda kuchukua nyanya maana Mtawanya ni sehemu ya Mtwara mjini ila imejitenga kidogo na sehemu zenye huduma kama stendi masoko nk.

YEYE 'Ndiyo nishafika kuna baba mdogo anaishi huko mtaa wa Ligula huwa nakuja kwake'

MIMI 'Ahaa basi kama ni hivyo namba zako sitazifuta pengine kuna siku utakuja huku unibebee ming'oko'

YEYE 'Hahaha vitu vyote vya kuomba zawadi Ndiyo utake ming'oko hata hivyo mimi naishi newala mjini hatuchimbi ming'oko labda kununua'

MIMI 'Ahaa kumbe newala nayo kuna mjini na vijijini!'

YEYE 'ndiyo, hujawahi kufika kwani!'

MIMI ' Ndiyo sijawahi ila nasikia watu wakisifia tu kwamba mandhari yake ni nzuri, natamani kufika lakini siwezi kwenza sehemu ambayo sina ndugu wa kumfikia hata kama kuna Gest'

YEYE 'ni kweli ila ndugu ushapata sasa unaweza kufunga safari utakapo amua'

MIMI 'Hahaha kweli!'

YEYE 'Ndiyo'

MIMI 'dah vizuri, nikitoka hapa naenda kwa seremala kuchonga kibubu nianze kuweka nauli'

YEYE 'Hahahaha! Kuchonga kibubu safari ya Newala? ingekuwa unataka kwenda Ulaya!'

MIMI 'hahaha sawa bhana, nakuacha kidogo nitakucheki mida'

YEYE 'Sawa mchana mwema'

MIMI 'na kwako'

Zikapita kama wiki mbili hivi nikiwa nawasiliana na Laima, kitu nilichokigundua kutoka kwake ni kwamba anapenda kucheka balaa, yaani anapenda kucheka kupindukia.

Mjomba unaesoma kama wewe ni mwalimu na umeoa huku Mtwara na umemwoa chibonge anaependa kucheka kupindukia. Nifate Pm mkuu unatakiwa kunilipa chochote kitu maana nilikuburudishia mwanamke wako bila malipo yoyote, yaani ilikuwa mimi nina kazi ya kumburudisha wewe una kazi ya kum bandua hadi ukaona haitoshi ulipohama Mtwara ukaamua kumchukua jumla jumla.

Baasi bwana... Siku ya kumtongoza rasmi ikafika, Jamani ukiwa huna hela unakuwa na ubunifu mno kwenye kutongoza.

Ilikuwa jioni ya saa moja nikiwa nimetulia tuli home, nilikuwa kitandani nimelala kichwa nimekilaza kwenye mto miguu nimeiwe kwenye ukuta.
Nikamkoli kama ilivo kawaida akapokea.

Baada ya kusalimiana:

MIMI 'Laima kuna kitoto cha ndege nahitaji tukifuge mimi na wewe, hicho kindege ni kichanga kabisa na kitahitaji huduma zetu ili kiweze kukua na hatimae kianzishe vizazi vingine vya ndege ambavyo vitaipamba dunia na kuifanya iwe sehemu nzuri zaidi ya sisi kuishi'

YEYE 'Hahahahaha! Kim umekula lakini? Habari za kufuga ndege umezitoa wapi wakati sisi tupo mbali?'

MIMI 'Nimekula eee, Umbali sio kikwazo kabisa kwa sisi kumfuga huyu kinda, na kama atakosa matunzo hadi akafa wakati sisi tupo itakuwa temefanya dhambi kubwa mno'

YEYE 'Hahahahahahaha..! unavyoweka msisitizo basi utafikili kweli huyo ndege yupo na yupo mikononi mwako'

MIMI 'eee ninacho hapa kipo moyoni kindege penzi sio vizuri tukakihujumu'

YEYE 'hahaha Jamani sasa mimi sihitaji kufuga na wewe hicho kindege penzi tuendelee na huu urafiki wetu, kama utahitaji kumfuga huyo ndege na kuruhusu tafuta mtu ambae atakuwa sahihi kwa wewe kufuga nae'

Jibu hili huwa ninalikumbuka hadi leo na kama ningemaliza maongezi yangu hapa nisingekuwa mtumwa wa mapenzi na mtumwa wa kifikra kwa huyu mwanamke.

Nimesema mtumwa wa kifikra kwa sababu kuna kipindi niliwahi kumwambia anitajie kiasi chochote kile cha pesa nimpatie ili abadilishe namba zake za simu, hii ni baada ya moyo kukubali ukweli kwamba huyu mtu hanipendi.
nilikuwa natamani kumuacha lakini nashindwa na kikwazo kikubwa ilikuwa ni namba zake zilikuwa kichwani.

Japo mwisho alinikubalia lakini hili nahisi ndiyo lilikuwa jibu sahihi.

Naendelea
 
Back
Top Bottom